KERO Changamoto ya course ya Clinical Nutritions and Dietetics inayotolewa UDOM

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Clinical Nutritions and Dietetics (Utabibu lishe na Chakula) hii ni Faculty mpya iko pale UDOM.

Miaka kadhaa sasa imekua na changamoto ya mtaala(Curriculum), hadi sasa tuliopo internship tunaona madhara ya curriculum bado haijitoshelezi.

Tumekuwa tukiomba ipitiwe na kuundwa upya bila ya mafanyikio na bila uongozi wa chuo kushughulikia. Pia hata tuliopo internship hatulipwi kama wenzetu waliosoma miaka 4 mfano, pharmacy na nursing.

Tunaomba mamlaka husika hususani Chuo na Wizara ya Afya ishugurikie hizi changamoto.

Mwanzo tuliambiwa hatukuwepo kwenye bajeti ya malipo ya internship, tunaomba mwaka huu tuone mabadiliko kwa wenzetu watakao kuja internship.
 
Wasomi wa Bongo bure kabisa. Hata kutatua matatizo yanaowazunguka hawezi. Wanasali sala ile ile ambayo watanzania karibu wote wanasali i.e. ''tunaomba mamlaka husika....''. Yaani hii sala imekuwa kama ile ya ''baba yetu uliye mbinguni'' ya wakatoliki. Bure kabisa. Nchi imejaa raia wasiojitambua muda wote ni ''kuomba mamlaka isadie''. Raia hawajui kuwa wao ndiyo wanatakiwa kuogopwa na kuombwa na mamlaka!
 
Kumbuka amekuambia kozi ni mpya ,pili kila jambo la kielimu linapokuwa na changamoto ,ili upate ufumbuzi lazima mamlaka husika ipate malalamiko ili ifanye marekebisho kwenye mapungufu ,sasa unavyomwambia asilalamike yeye ni katibu mtendaji wizara husika?
 
Mkuu, vyuo vina serikali za wanafunzi na ndiyo kazi zao. Infact, kila chuo ni lazima kiwe na utaratibu wa kutatua matatizo ya wana chuo. Mimi najaribu kuonyesha umuhimu wa nchi kuwa na watu wanaojibika na kila sehemu inayowajibika. Tatizo kubwa ni kwa watanzania tumezoea kuacha mifumo rasmi ya kutatua matatizo, na kujenga utamaduni wa kulalamika kitu ambacho kimefanya malalamiko yasipewe tena umuhimu. Na athari zake zinaenda mbali... unakuta eti waziri mkuu yuko mtaani anatatua matatizo ya viwanja na mirathi wakati kuna watu wamepewa hiyo kazi. Nadhani umepata point yangu
 
Daaah first step is hardest let us wait but binafsi nilijua mtaala wa BSC CND upo strong than OUT BSC FND kumbe challenge everywhere
 
Back
Top Bottom