Pole kwa mkwamo huo ulio kupata mkuu, mtu yeyote anayetafuta kitu bora hata kama vipo vingi lazima utajiuliza njia sahihi ya kumsaidia kupata kitu chake, lakini pia yawezekana wakati hujafikia wazo la kuoa ulikuwa unawaona wengi, lakini sasa wanaweza kuwa hawaonekani kwa sababu ndani ya jicho lako unatafuta mke na sio wanawake. kwa hiyo uko sahihi kabisa kutoana kirahisi.
Lakini pia mafundisho mengine, namaarifa ulijipatia juu ya mke na utafutaji wake unaweza kuwa kikwazo kwako, pengine unaweza hisi utaota, utakuja na kukwambia nakupenda, au takuwa tofauti sana na hawa unaowaona, hii sio kweli utamuona mwenyewe na kumwambia mwenyewe nakupenda atakubali na maisha yataanza.
Wewe unakazi mbili tu, ni kuomba sana Mungu akusaidie kumpata Mke mwema, na pili kumtafuta umuone. Kuomba mi lazima lakini kujibidiisha ili umuone ni vyema pia. kwa maeneo ya mjini kama unatafuta mke wengi wanaanzi miaka 25, 26,27, 28, 29 na kuendelea, hawa mawazo ya kuolewa yanakuwa ya kweli na hisia zao zimekaa kindoa na wapo tiyari kuvumilia maisha, kadiri umri unavyakuwa mkubwa mawazo yao juu ya maisha ni bora zaidi kuliko wenye umri mdogo.
Nijichoandika hapo sio sheria ya upekee, kunaweza kuwepo tofauti za uelewa wa maisha chini ya umri huo. Jambo la msingi ni kujua tu kuwa umri nifactor ya maamuzi ya kuolewa kwa mwanamke.
Ukimweka Mungu akusimamie, usijiulize sana mtakutana wapi, paweza kuwa popote, jambo la msingi ukihisi unaona mahali kama ni penyewe endelea kumwomba Mungu akusaidie, wakati mwingine shetani hujipenyeza kuharibu mwenendo wa kimungu, hivyo kila hatua muulize Mungu.
Jihadhari na haya, Usidhani kwa kuwa umeomba atakuja geto, usifikiri Mungu atamleta kwenye daladala au rafiki atakwambia vipi huyu, au utaota mnakwenda shopping, yaweza kuwa ndiyo lakini ondoa kabisa akilini, kuomba ni nyenzo ya kurahisisha mambo lakini application lazima ifanyike ili upate kazi. lazima utumie utashi wako, lazima uangalie wapi unapata hisia.
Hivyo jiweke sokoni kila wakati saa na dakika, najua unanielewa nikesema jiweke sokoni.
Jioni Njema.