TAJIRI MKUU WA MATAJIRI
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 11,999
- 24,328
CHANGAMOTO YA MASOKO KATIKA BIASHARA YA KUNUNUA MADINI:
GEMSTONES VS DHAHABU
Unapoingia kwenye biashara ya kununua madini tambua kuwa hii ni biashara kama biashara zingine, madini ni bidhaa kama bidhaa zingine unazoenda kununua na kuuza kwa wanunuzi hivo hata madini yako hivyo pia...
Kamwe usiwe na mtizamo kuwa chochote kinachoitwa madini ukikinunua ukipeleka sokoni lazima uuze hii sio kweli na wengi walioingia na mtizamo huu kwenye madini wengi wamepoteza pesa wameishia kubeba mimawe ambayo haina wanunuzi huko sokoni haliyakuwa wao washaingiza mitaji yao yote katika kuyanunua na baada ya kupeleka sokoni hakuna anae yahitaji....
Madini yapo aina nyingi sana duniani kuna aina tofauti za madini duniani zaidi ya aina 4000 na hivyo basi katika hizi aina za madini haya kila moja sokoni lina uhitaji wake linalofanya madini husika kutafutwa zaidi au kutohitajika zaidi...
Tukiachana na hizo aina 4000 za madini na tukaelezea tuu changamoto za masoko zilizopo katika kununua MADINI YA VITO VS KUNUNUA MADINI YA DHAHABU ni kwamba:
CHANGAMOTO YA MASOKO KATIKA KUNUNUA MADINI YA VITO:
Tunaposema neno madini ya vito au gemstones 💎 maana yake ni madini yote ambayo yana sifa ya kupitisha mwanga pale ambapo mwanga husika unapopigwa kwenye jiwe husika (ukiona jiwe ambalo ukilimulika na tochi unaona kabisa mwanga unapita kwenye hilo jiwe upande mmoja na mwanga huo unatokea upande wa pili wa jiwe juwa kuwa hilo jiwe lipo kwenye kundi la madini ya vito kwani hiyo sifa ya kupitisha mwanga ni sifa ya madini ya vito tuu)
Tunatakiwa kutambua kuwa madini ya vito/ au gemstones hili ni kundi au group ambalo ndani yake kuna madini ya aina nyingi sana maana tukisema gemstones katika hili kundi kuna aina tofauti za madini ya gemstones hata 1000 yanafika ila sasa katika biashara huwa tunaangalia yale madini ambayo kwanza yanapatikana kwa wingi katika mazingira yetu tunayoishi kwani kuna madini ya gemstones yapo ila kwa tanzania unakuta sisi hatunaga na kama yapo pasi bado hatujagundua yalipo kwa mantiki hii basi tunaposema gemstones unatakiwa kuelewa kuwa hapa kuna aina nyingi za madini zipo kwenye hili kundi...
Katika kundi hili la madini ya gemstones WATAALAMU wameligawanya kundi hili katika makundi MAKUU 3 kulingana na thamani za madini yenyewe yalivyo na makundi hayo ni kama ifuatavyo:
01: PRESIOUS STONES:
kundi hili linajumuisha madini yote yavito ambayo yana thamani kubwa kifedha, na nikupe siri moja madini haya kuwa na thamani kubwa kumetokana na madini haya kutopatikana kwa wingi katika maeneo yetu yaani haya ni madini adimu na kwakuwa na madini adimu kupatikana yamefanya yawe na thamani kubwa kiasi kwamba ukilipata jiwe dogo tuu kama goroli ya kuchezea watoto wewe tayali ni milionea, katika kundi hili kuna madini ya vito kama vile:
02: SEMI-PRESIOUS STONES:
Kundi hili limejumuisha yale madini ambayo yana thamani ya wastani yaani thamani yake sio ndogo sana wala sio kubwa sana yaani yapo kati kwa kati, bei zake au thamani zake sio kubwa kama madini yaliyopo kwenye kundi la precious stones ila bei zake pia sio ndogo kama madini yaliyopo katika kundi la cheap stones, katika kundi hili kuna madini ya vito yafuatayo:
NB: PRESIOUS STONES na SEMI-PRECIOUS STONES masoko yao huwa sio tatizo kikubwa wewe kama mnunuzi tafuta mawe mazuri na ukipata jiwe zuri lenye ubora makundi haya mawili masoko yake walaaa hayasumbuagi kichwa wanunuzi niwapogo tuu kwani ukienda na jiwe zuri soko la madini dar, arusha utauza tuu.
03: CHEAP STONES:
kundi hili linajumuisha madini yote yenye thamani ndogo au bei ndogo ambayo mara nyingi huwa yanauzwa kwa makilo na matani, na sababu kubwa kilichopelekea madini haya kuwa na thamani ndogo hadi kufikia kuuzwa kwa makilo na mengine kwa matani ni madini haya kupatikana kwa wingi kila sehemu ya mkoa wa Tanzania yaani tuchukulie mfano mdogo madini ya QUARTZ yale meupe ya kuchongoka ni madini ambayo kila mkoa yapo yanapatikana yaani hapa pale posta dar kungekuwa hakuna magorofa pakichimbwa huenda yakapatikana hii ndio imepelekea madini haya kutokuwa na thamani kubwa maana wewe wa Dodoma ukisema huuzi quartz yako wenzako wa Sumbawanga, Tanga, Manyara wanauza quartz zao sasa bei itapandaje na mizigo kila siku sokoni inaingia.?? Madini ya cheap stones ni kama vile:
JE, VIPI MASOKO YA HAYA MADINI YA VITO??
soko la precious stones na semi- precious stones..
ni kwamba kwa wewe mgeni unaetaka kuanza biashara ya kununua madini ya vito tambua kuwa madini ya VITO ambayo siku zote soko lake halina SHIDA lipo STABLE/LIPO IMARA ni madini ya kundi la PRESIOUS STONES na kundi la SEMI PRESIOUS STONES haya madini ya vito ya makundi haya mawili siku zote masoko yake hayasumbui kiasi kwamba ukiwa na madini mazuri ya madini haya muda mwingi wanunuzi wake wapo kikubwa na cha kuzingatia unatakiwa kununua madini yenye ubora sio kwamba umeambiwa madini PRESIOUS STONES NA SEMI PRESIOUS STONES ni madini ambayo soko lake muda wote lipo ukaenda kuzoa zoa wakati wa kununua hii HAPANA, madini ya vito hata ruby yenyewe kuna ruby ambayo sokoni inauzika na kuna ruby ambayo sokoni haiuziki kwa hiyo unatakiwa kununua madini yenye ubota mzuri ubora wa hali ya juuu na tukisema ubora wa madini ya vito tunazungumzia kuwa yawe na rangi iliyoiva, yasiwe na mikatiko, yasiwe na magonjwa kwa ndani na yawe kiooo na yawe na umbo zuri umbo lenye unene uliojitosheleza...
Soko la madini haya ya precious (ruby,sapphire, Emerald)na SEMI precious (spinel, green garnet, tanzanite) huwa liko wazi sana na hata ukiwa na jiwe zuri leo ukipeleka soko la madini la serikali pale arusha unauza muda huo huo na kuondoka zako na pesa zako, kikubwa zingatia ubora madini haya usipojuwa jiwe lipi bora nilinunue na jiwe lipi sio bora sitakiwi kulinunua yaani katika biashara hii utapata hasara kila leo..
Soko la madini ya CHEAP STONES:
Haya ndio madini ambayo wageni wengi ambao hawajui madini ndio wanakopotezeaga mitaji yao na unajuwa kwa nini wanapoteza mitaji yao huku?? Ni kwamba siku zote haya ndio madini ambayo YANAPATIKANA KIRAHISI SANA NA KWA WINGI SANA NA NDIO MADINI AMBAYO YANAPATIKANA KWA BEI NDOGO NDOGO SANA YAANI MFANO ukienda pale Gairo ukitana feldspar utauziwa kilo kwa tsh 2,000/= na ukianza kununua leo wiki ikiosha umepata tayari kilo 200 umejaza mzigo, sasa wageni wengi kwa kuwa wengi wetu tuna mitaji midogo ya chini ya milioni tunaona huku ndio kuzuri kwakuwa kwanza yanapatikana kirahisi na kwa mtaji mtu alio nao ana mudu kununua haya mawe hivyo wengi wanakimbiliaga huku maana kule kwenye madini ya PRESIOUS NA SEMI PRESIOUS kule bana pasua kichwa kule jiwe DOGOOO la gram 2 (mfano la spinel) mchimbaji anakwambia nataka milioni 15 wakati wewe mtaji wako una milioni tuu umekuja nayo na muda huo huo hilo jiwe la gram 2 ni adimu sana kulipata unaweza kukaa miezi usiletewe jiwe la hivo kwakuwa mawe ya makundi hayo licha tuu ya kuwa ya garama kubwa ila pia kuyapata ni kazi ni adimu, hivyo basi wengi kule hawakuwezi wanaona huku kwenye madini ya makilo ndio kwa kuchangamkia maana yanauzwa bei NDOGO na UPATIKANA ni rahisi kama vile unavyonunua mahindi wakati wa mavuno...
Hivyo basi wageni wengi wa baishara ya kununua madini ya vito huku ndio walikokimbilia kuja kuanza nako na shida iko wapi???
Shida ni kwamba wengi wamekimbilia huku wakiwa na mitizamo kuwa kila madini ukiwa nayo ni pesa na kuuza ni uhakika sasa unapokuja kwenye biashara ya madini ya vito hususani katika hili kundi la madini ya vito la CHEAP STONES habari inakuwa tofauti kidogo maana masoko yake sio kama madini mengine haya madini masoko yake yanakuja na kupotea yaani ndio mana utasikia madini ya ODA MAALUM basi ndio haya yani inaweza kutokea wiki hii kila myu anatafuta QUARTZ kwakuwa kuna mgeni kaja anayataka huko mjini ila mgeni huyo akijaza mzigo na akaondoka tayali soko la QUARTZ linazima na kudorora tena yaani wewe kama hujauza mzigo wako uweke ndani subiria hadi mgeni mwingine aje tena yakihutajika ndio uuuze tena ambapo hatujui lini atatokea mwingine.....
Hivyo basi madini haya huwa hayana soko la uhakika siku zote, unaweza kubeba madini haya ukapeleka soko la madini arusha ila kila ukiingia maofisini kuuliza kama wanayanunua utasikia haya HATUNUNUI hapa tunanunua ruby /sapphire/ na spinel tuu hivyo utabaki na mawe yako hadi usikie kuna mnunuzi kaja anayatafuta ndio sasa upeleke ukauze....
JE, WEWE MGENI UNASHAURIWA NN??
Kwanza kikubwa na cha msingi ni kujuwa na kuelewa madini unayoyanunua ni madini ya aina gani na sokoni madini hayo uhitajiwake uko vipi, kama umeamua kudili na madini haya ya cheap stones basi unatakiwa kutambua kuwa umechagua kundi zuri ambalo hata hupati shida kupata mzigo ila kisaikolojia uwe tayali kuingiza pesa na kuisimamisha maana itafika mahala umenunua mzigo ila mnunuzi hakuna hivyo itakubida ungoje hadi mnunuzi atokee hapa huenda ukasubiria miez 3 miezi 6 au mwaka hivyo kisaikolojia ulijue hilo ili usije ukajiona umepoteza pesa hapana bali ndio nature la hayo madini soko lake lilivyo.... ila pia ukidili na madini haya jitahidi sana kutafuta mitandao ya KUTOSHA ya masoko ili usiwe unakaa na madini ndani kwa muda mrefu sana hakikisha unatafuta channel za masoko kila kona ili mzigo wako usidode maana masoko yapo sema kujuwa yako wapi ndio tatizo unaeza kaa na mawe ndani kumbe wenzako daa huko wanauza kila.siku hayo mawe ila wewe hujui...
KWA NINI KATIKA NCHI YETU MADINI YA CHEAP STONES HAYANA MASOKO YA UHAKIKA??
hatuna masoko ya uhakika ya madini haya kwakuwa nchi yetu bado hajiaweka mikakati ya kufungua viwanda vya kuongeza thamani za madini haya....
Tulipaswa kuwa na viwanda vya kukata haya madini ya vito ya bei nafuu na kuyachonga kisha kutengenezea mapambo kama vile rozali, shanga, heleni, Pete, n.k na kama tungekuwa na viwanda vingi wa staili hii basi wanunuzi wote wa haya mawe wangekuwa wanapeleka kuuza mawe yao katika hivyo viwanda yaani watu wangekuwa wapewa oda kiwandani....,
Mpaka sasa kwa haraka haraka kwa tanzania ni kiwanda kimoja tuuu kikubwa kinafanya hii kazi ya kununua madini ya vito ya cheap stones na kuyaongeza thamani kwa kuyakata na kuyachonga na kiwanda hicho ni cha wachina kipo pale KIBAHA MADAFU...., laiti kama tanzania tungepata viwanda kama hivi walau 15 katika nchi yetu tayali soko la madini haya lingebadilika sana mana hata kwa hawa wanunuzi wamilikinwa viwanda wangeshindana bei kununua malighafi za madini ya cheap stones hivyo wamiliki migodi ya cheap stones wangenufaika ila leo hii mtu ana madini ila soko hana kayaweka tuu ndani....HII NI CHANGAMOTO ILA PIA NI FURSA WA WEWE MWENYE MTAJI....., milioni 70 hadi 100, zinatosha kabisa kununua mitambo ya kuongeza thamani madini ya vito na kutengeneza mapambo kwa taarifa zaidi juu ya hilo wasiliana na Madini Yetu Tanzania Limited
SOKO LA MADINI YA DHAHABU
siku zote kwa upande wa madini ya dhahabu changamoto ya soko sio kitu cha kuumiza kichwa sana kwani muda wote masoko ya kununua dhahabu yapo wazi na yanafahamika kwani kila mkoa ambao unachimba dhahabu tayali serikali imefungua masoko katika mikoa hiyo na kwenye hayo masoko kuna maofisi ambayo yana wanunuzi wa uhakika na muda wote wanakungoja wewe upeleke mzigo wako ukapewe pesa hivyo changamoto kwenye huu pande naweza sema sio shida tena....

>> Diamond 💎 (almasi) (yapo Shinyanga, Maganzo)
>> Ruby (yapo Morogoro, Mahenge)
>> Sapphire (yapo Ruvuma, Tunduru)
>> Emerald (yapo Rukwa/ Mpamda)
02: SEMI-PRESIOUS STONES:
Kundi hili limejumuisha yale madini ambayo yana thamani ya wastani yaani thamani yake sio ndogo sana wala sio kubwa sana yaani yapo kati kwa kati, bei zake au thamani zake sio kubwa kama madini yaliyopo kwenye kundi la precious stones ila bei zake pia sio ndogo kama madini yaliyopo katika kundi la cheap stones, katika kundi hili kuna madini ya vito yafuatayo:
>> Spinel Morogoro (Mahenge/Matombo)
>> Tanzanite Manyara (Mererani)
>> Green garnet Lindi (Ruangwa lindi/Lemshuku)
NB: PRESIOUS STONES na SEMI-PRECIOUS STONES masoko yao huwa sio tatizo kikubwa wewe kama mnunuzi tafuta mawe mazuri na ukipata jiwe zuri lenye ubora makundi haya mawili masoko yake walaaa hayasumbuagi kichwa wanunuzi niwapogo tuu kwani ukienda na jiwe zuri soko la madini dar, arusha utauza tuu.
03: CHEAP STONES:
kundi hili linajumuisha madini yote yenye thamani ndogo au bei ndogo ambayo mara nyingi huwa yanauzwa kwa makilo na matani, na sababu kubwa kilichopelekea madini haya kuwa na thamani ndogo hadi kufikia kuuzwa kwa makilo na mengine kwa matani ni madini haya kupatikana kwa wingi kila sehemu ya mkoa wa Tanzania yaani tuchukulie mfano mdogo madini ya QUARTZ yale meupe ya kuchongoka ni madini ambayo kila mkoa yapo yanapatikana yaani hapa pale posta dar kungekuwa hakuna magorofa pakichimbwa huenda yakapatikana hii ndio imepelekea madini haya kutokuwa na thamani kubwa maana wewe wa Dodoma ukisema huuzi quartz yako wenzako wa Sumbawanga, Tanga, Manyara wanauza quartz zao sasa bei itapandaje na mizigo kila siku sokoni inaingia.?? Madini ya cheap stones ni kama vile:
>> moonstone
> quartz
>>amethyst
>>rhodolite
>> feldspar
>> Green aventure
>> appetite n.k