cold water
JF-Expert Member
- Oct 6, 2021
- 238
- 954
Naomba nianze kwa kujieleza,
Nitaelezea changamoto katika mahusiano ninayoyapitia, hasa upande wa tofauti ya umri. Mimi ni mwanamke, nimezaliwa mwaka 1993.
Mahusiano yangu ya kwanza yalikuwa na mwanaume aliyezaliwa mwaka 1992. Kama nilivyoeleza mwanzo, tulipishana mwaka mmoja tu, yeye akiwa mkubwa kwangu kwa mwaka mmoja. Hata hivyo, hatukudumu kwenye mahusiano yetu kutokana na tabia zetu kutowiana.
Sasa, baada ya kuachana naye, wanaume ninaowapata ni wale waliozaliwa mwaka 1998. Ninapata changamoto kubwa kuhusiana na suala la umri. Nashindwa hata kufikiria kubeba mimba kwa sababu nawaona wadogo kwangu, na pia ninaogopa kuchekwa na jamii inayonizunguka.
Hata hivyo, utakuta tunapendana vizuri, na tatizo pekee linakuwa umri. Naomba ushauri kwa sababu nina mtoto mmoja wa miaka kumi, na ninatamani kuanzisha familia nyingine. Umri unazidi kwenda, lakini wanaume ninaowapata naowapenda ni wadogo kwangu.
Sijabahatika kupata mwanaume wa umri mkubwa ambaye nitampenda. Si kwamba hawapo, lakini hawanivutii kabisa!