Changamoto ya Umeme Newala: Ni Wakati wa Kupata Suluhisho la Kudumu

mike2k

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2016
Posts
1,650
Reaction score
3,655
Nimekuja kikazi Wilaya ya Newala, Kata ya Kitangari, Nilitarajia changamoto za kuzoea mazingira mapya, lakini sikutarajia changamoto kubwa ya umeme.

Kwa kweli, hali niliyoikuta imenikumbusha enzi za mgao wa umeme miaka iliyopita, ambapo umeme ungeweza kukatika kwa saa nyingi bila maelezo ya kutosha. Hapa, kuna siku umeme unapatikana kwa chini ya saa 4 tu kwa siku. Kwa siku kadhaa mfululizo umekuwa ukikatika kwa saa nyingi bila taarifa, jambo linaloathiri maisha na shughuli za wananchi.

Mfano mdogo tu, nimeshindwa hata kunyoa nywele kwa sababu vinyozi wengi hufunga biashara zao kutokana na kukosekana kwa umeme. Wafanyabiashara wengine nao hupata hasara kila siku.

Nilipowauliza wenyeji, waliniambia hali hii imekuwa ya kawaida kwa muda mrefu. Kama ni kweli, basi ni changamoto inayostahili kupewa kipaumbele.

Kinachonishangaza zaidi ni kwamba Mkoa wa Mtwara ndio moja ya maeneo yenye rasilimali kubwa ya gesi asilia nchini. Kwa miaka mingi, serikali inayoongozwa na CCM imekuwa ikieleza kuwa matumizi ya gesi asilia yangesaidia kuboresha upatikanaji wa umeme na kupunguza changamoto za nishati. Ndiyo maana najiuliza: kwa nini wananchi wa maeneo haya bado wanakabiliwa na hali hii ya kukatika kwa umeme mara kwa mara?

Ningependa TANESCO au mamlaka husika watueleze sababu ya tatizo hili na ni lini wananchi wa Newala, hususan Kata ya Kitangari, wanaweza kutarajia huduma ya umeme yenye uhakika.

Na kwa yeyote anayepanga kuja Newala kwa shughuli au kuhamia huku, usisahau kubeba power bank. Inaweza kuwa moja ya vitu muhimu zaidi utakavyohitaji.
 
Hata mimi nilikuwepo huko siku chache zilizopita, nakubaliana na wewe.
Cha kushangaza zaidi ni kwamba wananchi wenyewe wameshaizoea hiyo hali.
 
Habari, Ndugu Mteja.
Pole sana kwa changamoto unazoopata. Tafadhali fahamu kuwa mara tunapolazimika kusitisha huduma ya umeme kwa ajili ya matengenezo yaliyopangwa au hitilafu za ghafla, huwa tunatoa taarifa mapema pamoja na maelezo ya sababu ya usitishaji wa huduma.
Taarifa hizi hutolewa kupitia njia mbalimbali ikiwemo ujumbe mfupi wa SMS (SMS) pamoja na makundi ya WhatsApp yaliyogawanywa kulingana na maeneo.
Iwapo hujapata taarifa hizi, tunaomba radhi na tumepokea ombi kuhusu changamoto za umeme Newala.
Pia, kama ungependa kupata taarifa Tafadhali tutumie namba yako ya WhatsApp kupitia inbox pamoja na mkoa unaoishi, na tutahakikisha tunakuunganisha kwenye makundi husika ili upate taarifa zote muhimu kuhusu huduma ya umeme katika eneo lako.
 
Back
Top Bottom