Changamoto ya upatikanaji kwa njia za mawasiliano zitolewazo na Taasisi za Umma, makampuni na sehemu zote zitoazo huduma

Changamoto ya upatikanaji kwa njia za mawasiliano zitolewazo na Taasisi za Umma, makampuni na sehemu zote zitoazo huduma

Kilangi masanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
4,495
Reaction score
5,025
Habari wadau kwa ujumLa.Naimani mu wazima wa afya.

Ni jambo la kawaida kwa kizazi hiki cha sayansi na teknolojia kuhakikisha tunaenda sambamba na mataifa yalioendelea kupitia nyanja hizo.

Changamoto imekua kubwa na kama wahusika hawaioni au hufanya makusudi yasio na sababu yeyote ile basi waache au mamlaka husika wachukue hatua stahiki.

Namba nyingi za huduma kwa wateja (Taasisi zote za umma na hata NGOs) na hata ofisi za watu binafsi pia, si jambo geni tena kukuta kuna namba za huduma kwa wateja ,emails ,baruapepena hata apps kabisa.

Kimbembe ni kua kwa asilimia kubwa mawasiliano yanayowekwa hapo kwa hizo ofisi husika hua ni aidha hayapatikani, na kama zinapatikana kujibiwa au kupokelewa simu imekua suala gumu sana.

Adha hii tunaoipata ni sisi wahitaji wa huduma kwani kuna mda inasababisha kupoteza muda , na hata fedha kwa kufunga safari pengine ndefu sana kuhangaikia jambo ambalo pengine kwa simu moja tu au email moja tu au barua moja lingekwisha.

Wanajamii forum kupitia uzi huu hebu tupaze sauti na ikiwezekana tuweke na majina ya idara husika ambazo kupitia njia za mawasiliano tajwa hapo juu zimekua kero na kusababisha taflani katika maisha yetu ya kila siku.

Kwa kuanza NHIF ( mikoani ), PSSSF, na zingine nyingi badilikeni
 
Back
Top Bottom