Changamoto ya upatikanaji wa nguo bora za ndani za kiume(boksa)

Changamoto ya upatikanaji wa nguo bora za ndani za kiume(boksa)

Kilangi masanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
4,495
Reaction score
5,025
Habari za mda wadau natumaini mko poa na mnazisubiri per diem za mama kwa shauku kubwa.

Kwa kuzingatia kichwa tajwa hapo acha nijikite kuelezea kero ninayokumbana nayo.Binafsi mimi kwa maisha yangu yote ya ukubwani (kuanzia baleghe)nimekua ni mtu ninayevaa boksa moja kwa siku, hivo sikuifuatayo siigusi tena mpka ifikiwe zamu yake pengine si kumi hivi (mwanaume hutaki kuwa na bosa mia bwana kama dadazetu😁).

Changamoto niliokumbana nayo kwa hiki kipindi cha hivi karibuni miaka miwili iliopita mpka sasa ni je nipate wapi nguo ya ndani iliobora na inayodumu?

Nimekua nikibadili aina mbali za boksa ila ufanisi wake umezidi kupungua siku hadi siku,Kuna zile bosa zinakua tatu kwenye kifuko na wanaweka kalamu ndani yake kutoka kwa ndugu zetu PRC( Uchinani huko).Hizi awali zilikua poa lakin leo hii zimekua ovyo kwangu ukiivaa mara ya kwanza ukifua ukija vaa tena tayari ishaanza aidha kutatuka nyuzi ama kuchanika hasa sehem ya chini inakozibeba korodani na kichwa cha chini kwa ujumla .

Adha hii imekua kwa kila brand nayokutana nayo mkoani kwangu boksa hazidumu na huwez toboa nazo miezi miwili , pengine uvae tu kuonesha ufito wake (pindo la juu) ambalo ndilo gumu kuisha ila ndani uko uchi.

Napata ukakasi je ni kweli hakuna brand ambayo ni affordable kama hizi za kichina ambayo inarange kwenye price ya 5000Tshkwa boksa moja na inatoa boksa bora?Je turudi zama za kuvaa mibukta mikubwa au turudie tu mitumba ya wazungu?

Wadau tusaidiane kwa hili ila hizi brand zinanikera last weekendnimenunua boksa tisa @3tsh 1,2000 so Tsh 3,6000 imenitoka ila leo kila nilioivaa inaonesha hatufiki sherehe ya mtoto wa afrika.

Wadau mnanunua wapi nguo zenu? Je ubora mnaoupata ni tofauti na wangu?
 
Nunua boxer ya mturuki, CNT au Bersel utasahau hizo shida unazolia lia hapa.
Bei zina range 10000, 11000 mpaka 12000 kwa pc moja kwenye maduka ya reja.
Kwa mkoa niliopo ni mtihani heri mnipe sample na duka kama ni town au nje niagize nimechoka mie mazee
 
Mbona zipo nyingi tu.....

1653655110468.png
 
Unaweza ukanunua kisha ukaenda kwa fund(wa kushona) ukazrudshie uzi kabla ya kuzivaa, hii itasaidia kwa kias fula.
 
Boksa moja elfu 12. Hapo ndipo nasema wanaume tumeumbwa mateso tuvumilie tupambane kuwa mwanaune ni mateso. Hapo mwanamke kwenye elfu 12 kapata dozen au nusu dozen ya pichu. Huwa najiuliza wanaouza nguo za kiume wanapataje faida imagine mwanaume anaboksa 7 hadi 10 za materio magumu anakaa nazo miaka au mwaka.
Hata mavazi mengine ya kiume hutumika muda mrefu bila kuchakaa wala kupitwa fashion. Njoo kwa hawa akina HAWA kila siku kuna miundo mipya na mbaya zaidi nguo zao hutengenezwa na materio mepesi mnoo yanayoweza chakaa haraka.
Hivi wanaouza nguo za kiume hupataje faida au ndo maana wanatupiga bei kubwa kiivo
 
Unaweza ukanunua kisha ukaenda kwa fund(wa kushona) ukazrudshie uzi kabla ya kuzivaa, hii itasaidia kwa kias fula.
Inshu ni kua zinachanika pale mzee baba anapokaa na sio kutatuka nyuzi nimeshapokea mzigo wangu wa turkey kupitia silent ocean so sina neno najigaragaza
 
Back
Top Bottom