Changamoto ya usafiri kila ifikapo mwezi Disemba

Changamoto ya usafiri kila ifikapo mwezi Disemba

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
📖Mhadhara (62)✍️
Kumekuwa na changamoto ya usafiri kipindi cha mwezi Disemba hasa karibia na tarehe za sikukuu ya X-Mass na Mwaka mpya. Hiki ni kipindi ambacho watu wengi wanasafiri kwa ajili ya kwenda kula sikukuu mikoa mbalimbali. Sikatai kuwa kipindi hiki vyombo vya usafiri vinazidiwa nguvu na abiria, lakini kunakuwa na changamoto za kutengenezwa kwa makusudi.

✍️CHANGAMOTO ZA KUTENGENEZWA:
1. Baadhi ya wamiliki wa vyombo vya usafiri na/au waliokabidhiwa kuendesha vyombo vya usafiri hupandisha nauli kiholela katika kipindi hicho cha sikukuu.

2. Baadhi ya madereva wa magari ya abiria hawazingatii sheria za usalama barabarani. Wanataka kuwahi kushusha abiria kisha warudi wachukue abiria wengine. Nahisi pia kipindi hiki hakuna services ya gari, ni mwendo wa "Shusha-Geuza-Pakia".

✍️MAONI YANGU KWA MAKUNDI MATANO;
1. KWA:- WAMILIKI & WALIOKABIDHIWA KUENDESHA VYOMBO VYA USAFIRI - Ninawaomba waache tamaa mbaya ya kupandisha nauli bila utaratibu (kiholela) katika kipindi hicho, kwani wanaumiza abiria wa hali ya chini. Si abiria wote wanakwenda kula sikukuu, wengine wanakwenda misibani.

2. KWA:- WAKATISHAJI WA TICKETS NA WAPIGA DEBE - Ninawaomba waache tabia ya kujaza majina bandia kwenye mikeka ya Mabus ili kuwadanganya abiria kuwa Bus limejaa hivyo abiria wajiongeze "cha juu" ndo wapate seat.

3. KWA:- MAMLAKA YA UDHIBITI USAFIRI ARDHINI (LATRA) - Ninawaomba LATRA muendelee kuwa wakali na kuwabana watu wenye tamaa ya kupandisha nauli kiholela kipindi cha sikukuu za X-Mass na Mwaka mpya ili kuondoa unyanyasaji wa wazi kwa abiria.

4. KWA:- MSAFIRI (ABIRIA) - Abiria pia wana jukumu la kudhibiti changamoto ya upandishwaji wa nauli kiholela kipindi cha sikukuu za X-Mass na Mwaka mpya. Abiria ukikubali kujipandishia nauli (kutoa cha juu) ili upate seat unamtesa mwenzako ambaye anasafiri kwenda msibani.

5. KWA:- JESHI LA POLISI TANZANIA - Ninaomba Jeshi la Polisi Tanzania waendelee kuwa macho, kuwa wakali, na kuwabana madereva ambao hawatozingatia sheria za usalama barabarani.
__________
RIGHT MARKER
DAR ES SALAAM
 

Attachments

  • images (23).jpeg
    images (23).jpeg
    52.5 KB · Views: 4
Back
Top Bottom