SoC02 Changamoto ya Uwajibikaji wa Viongozi Ngazi ya Kata

SoC02 Changamoto ya Uwajibikaji wa Viongozi Ngazi ya Kata

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Aug 11, 2022
Posts
7
Reaction score
2
Uwajibikaji wa viongozi ngazi ya kata ni suala ya kuzingatiwa hasa kwa watu waliopewa mamlaka ya kuongoza bila kubagua dini au itikadi ya vyama.Viongozi kutokuwajibika katika utozaji wa tozo ndogo ndogo katika kata kama vile

Ulipiaji taka hii ni mojawapo ya changamoto inayonikumba mimi binafsi na watu wanaonizunguka hasa katika ulipiaji wa taka. wanaokusanya fedha hizi za taka hawana eletronic mashine za kutolea risiti bali wanakuja na risiti zilizotolewa tarehe za nyuma .Hili swala husababishia serikali kukosa kodi maana kikawaida unapolipa unahimizwa kudai risiti halisi sio iliyotoka jana na haionyeshi jina lako wewe mlipaji wala namba ya nyumba.

Kulipia fedha ya ulinzi(ulinzi shrikishi)Hii ni moja ya changamoto katika kata hasa .Hii fedha inakusanywa hasa na wenyeviti wa serikali za mtaa na wajumbe .Wanakusanya fedha hizi bila kutoa risiti halisi za eletronic sasa sisi kama wapenda maendeleo tuona hili halipo sawa. katibu kata inabidi kufuatilia jinsi ya ukusanyaji wa tozo hizi na kujua zinaenda wapi.

Usawa katika ulipaji wa tozo mfano katika kata ya karakata ilala dar es salaam hakuna usawa katika ulipaji. ikiwa nyumba moja unalipa tsh 5000 kwa mwezi ikiwa wewe ni mpangaji unalipa tsh 2500 kwa mwezi. Hii haipo sawa kama kunawapangaji 4 inamaana utalipa tsh 10,000 .hii inatuumiza hasa wapangaji ukizingatia tunakipato cha chini. viongozi wa kata wanawajibika kufuatilia hii sheria na kuibadilisha.

Viongozi kutokuwajibika hasa katika ufuatiliaji wa sheria na changamoto zinazowakumba wananchi anaowaongoza kama vile miundombinu na kutokufuatilia tozo zinazokusanywa katika kata yake .Ufuatiliaji ni jambo zuri sababu linaweza kujua changamoto ni nini na jinsi ya kuitatua changamoto hiyo. Ufuatiliaji uendane na changamoto husika mfano.

Ufuatiliaji wa miundombinu hii ni njia mojawapo ya kutatua changamoto sababu unapofuatilia miundombinu iliyomo katika kata yako itakusaidia kujua
bora na isiyo bora .mfano watu kuziba miferiji ya maji, kujenga kwenye njia ya maji au kutupa takataka kwenye vyanzo vya maji. hii isipofuatiliwa itasababisha milipuko ya magonjwa na mafuriko maana mifereji itakuwa imezibwa na takataka . kama kiongozi unawajibika kufuatilia swala hili ili kuepuka madhara zaidi .

Ufutiliaji wa ratiba ya uzoaji taka kama kiongozi unawajibika kufuatilia kwa ukaribu kampuni au taasisi uliyoipa idhini ya ukusanyaji taka .Kwa kawaida taka kwa wiki hukusanywa mara tatu lakini kampuni nyingi huwa hazifuatilii sheria hiyo ..Hii upelekea mrundiko wa takataka nyingi barabarani zilizokusanywa kwa ajili ya kwenda kutupwa .Hali hii husababisha magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu kutokana na taka kuoza hasa taka laini .hili swala la kuchelewa kukusanywa kwa taka ni kutokana na viongozi kutoa tenda kwa kampuni zisizo na sifa .Hasa katika vifaa vya kutendea kazi pia kuwa na magari chakavu na pia yanakua hayana uwezo wa kuhimili ukubwa kieneo .Hii usababisha usumbufu hasa kwa wananchi wa eneo husika.

Kuwajibika kufuatilia fesha zinazokusanywa katika kata yako ili kujua usahihi katika ukusanyaji. kuwajibika kufuatilia fedha zinakusanywa kama serikali ilivyoidhinisha bila kuwa na ubadhilifu wowote katika ukusanyaji. Hii itapelekea kuwa na uzingatiaji katika kutoa risiti na kupokea ili kuepuka ubadhilifu.

Ushirikishwaji wa wananchi katika maendeleo na utoaji wa maamuzi.ukiwa kama kiongozi wa kata unawajibika kushirikisha wananchi katika maamuzi ili kuepuka migogoro itakayotokana na maamuzi ya watu wachache.hii itasaidia kuleta mawazo ya watu mbalimbali ambayo yatasaidia kutatua changamoto zinazowakabili na nichachu ya maendeleo katika kata.

Ufutiliaji wa viongozi walio chini yako kujua uwajibikaji wao katika utendaji kama ni mzuri au mbaya .Hii itakusaidia kujua viongozi ambao hawawajibiki au ambao hawana sifa za uongozi na ambao wanatumia uongozi kama fimbo ya kuwaadhibu watu ..Hata kama wanahaki ya kuhoja ila wanachukuliwa hatua bila kusikilizwa.

Ufuatiliaji wa watu wanaotozwa faini walioshindwa kulipia mfano taka .Faini iendane na kosa alilolifanya na kuepuka kutokumbambikiziwa kesi zingine zisizo muhusu .Inabidi kuwe na ufuatiliaji kabla ya kutoa hukumu ya faini ili kiongozi anawajibika kulifuatilia.Hii itasaidia kutokufunja haki za binadamu na kuepusha migogoro ambayo ingeweza kujitokeza kutokana kuonewa kwa wananchi.

Yote kwa yote serikali inapaswa kuwachunguza viongozi wa chini ili kubaina ubadhirifu changamoto zinazowakabili hasa katika sekta ya maendeleo na miundombinu afya , elimu na barabara .hii itasaidia kuondoa changamoto zilizokua zinawakabili raia .

mwandishi ni issa shabani
 
Upvote 0
Back
Top Bottom