Changamoto za kumiliki gari "unique"

Changamoto za kumiliki gari "unique"

Tunakosa sana fursa. Kuna nchi ndogo na za kishamba tu watu wanaendesha ndinga za Europe kinyama tu. Tanzania tuna ushamba sana yaani kila mtu IST, Harrier, Rumion, Rav4, Hillux, Prado, Corolla, Mark x, Premio, Vanguard. Yaani ni kero. Ukiingia mtandaoni leo gari kali za Europe ni bei chee sana kuliko hizo za Kijapan ambazo nyingi ni mabati matupu, hazitulii barabarani, lakini tunalazimika wote kununua hizo za Japan. Hivi unajua BWM kali kabisa mtandaoni used unapata kwa bei rahisi kuliko Vanguard au Rav4 Miss Tanzania? Likewise, Audi, Volvo, VW Tiguan, VW Tuareg, Ford Escape, Benz nyingi ni bei affordable kuliko Toyota. Botswana tu hapo watu wako na ndinga kibao za Europe, kwa Tanzania utajuta, spea hakuna!
Na unajua Ni kwanini hizo Gari za Mjerumani Ni Bei ndogo kuliko za mjapan?Go figure 😄😄
 
Mwanzo Kabisa ilikua inapasua pipe, yaani ikichemsha maji yantokea kwenye pipe ikiziba inatoboa sehemu nyingine tukabadilisha thermostat, water pump ikatulia kidogo nimeitumia kama miezi miwili Juzi Tar 18 natoka asubuhi nimeikagua kama kawaida maji yapo sawa natoka napandisha kimlima kidogo naona inakosa nguvu, nikamaliza mlima nikaweka pembeni kufungua bonet mvuke unatoka.

Baada ya Hapo Ikakosa Nguvu Kabisa, Ukiwasha Kuondoka Haiondoki. Kuipeleka Garage ilibidi kuivuta.
Mambo ya Germany Engineering hayo, pambana mkuu.
 
Offer nilizokuwa napewa ni za laki 2 wengine laki 4 ila ukienda kuulizia bei kwao ni 900K bila gearbox yake. Ukiweka na gearbox wanaongeza laki 4.5 juu 😂😂😂 nikitazama engine ni nzima haijawahi kufunguliwa gari iliungua na moto yote ikapona engine tu. Maana moto haukufika kuiharibu kabisa mbele.

Nilikaza moyo tu ikafikia wakati nilikata tamaa njaa ilinikamata vibaya mno. Mungu si Rashidi sina hili wala lile napigiwa simu kuna mafundi wanakuja kukagua.
Wauza ma spare ya kukata Ni makumar Sana wale,sitakagi hata kuwasikia.
 
Sijajua kuna nini kilichojificha kwenye punda..
Ukimgonga mtu anaweza kudhani umegonga mti au umegonga trailer kwa nyuma..
Asee hii no kweli kabisa. Kuna Ist moja hizi new model niliiona imegonga punda barabara ya Mombo asee imeisha huwezi kuamini. Mbele hapo hakuna kitu na ma airbag imefua yote mawili ni balaa.
 
Duh isijekuwa cylinder head gasket.

Spark plug zina hali gani?

Muonekano wake, at least ndio kitu cha kwanza kuangalia kama engine inaingiza maji ndani.,
Fundi Pia Aliniambia inawezekana cylinder head gasket imepinda.

spark plug mbili zilikuwa za zamani zingine zilikuwa mpya.
 
Back
Top Bottom