Changamoto za kupata mtoto mchanga ukiwa umri wa kustaafu, unakuwa ni Baba Babu. Dawa ni kujipanga kabla, vinginevyo ni kubebesha watu mizigo yako

I wish ungemuona utatupilia mbali hizo fikra potofu.
Kumuona sura au akili huyo mtoto wa Pascal Mayala? Sura aweza kuwa vizuri shughuli kwenye akili .Toto la baba mzee na Mama mzee changamoto hata akizaliwa mzima iko kwenye akili mbele utaliona performance shule kuwa kuna walakini hata ulipeleke shule nzuri
 
Hongera sana; Kwa sie watu wa poti kuzaa kwenye umri mkubwa ni kawaida sana.Kuzaa kwenye 50 - 60 ukanda wa ziwa wala haishtui hio ni moja ya mila na desturi za u poti! Happy birthday Mayalla Snr na Happy born day Mayalla Jnr. Nguvu ya mamba kumai.
Kwa mwanaume it is ok.

Huyo mzaaji mwanamke ana umri gani awe hawara au mke whatever .Shida iko hapo

Pascal atueleze huyo mwanamke mzaaji ana umri Gani? Issue sio kumwita Pascal Mayala Junior
 
Happybirthday bro,
Hebu nipigie hesabu kama nikiwa na 25mil na kununua bond.
 
Wanasema huwezi kua bingwa milele...if it's true amefulia inakuhusu nini...? Au wewe una uhakika wa kudumu ulivyo milele?
 
Yatakusaidia nini?
 
Happy birthday brother, Mungu akupe maisha marefu kaka. Wewe ni moja ya watu mnastahili kuwa na kitabu cha kuelezea maisha yako ya uandishi/utangazaji.

Guru wa mahojiano, Respect brother!
 
Wengine wanakua bright sana wazaz wakiwa na umri mkubwa. Usikariri
 
Mungu kampa mwanadamu kuishi miaka 70, mingine bonus, yangu ni hayo Tu!
Hongera kwa kuitikia wito wa kuijaza dunia!
Umepokea zawadi nzuri, Una watoto na wajukuu, hawa wajukuu watamuitaje bamdogo junior?! Wamemzidi umri!
 
Mbona mnasahau withholding tax?
 
All the best brother Pascal. Mungu akufanyie wepesi kwenye malezi ya Pascal jnr, na afanye njia pale panapoonekana kama hapana njia.
 
Bandiko refu lakini linakutia stress mwenyewe!

Hofu hii ya kuogopa watoto wa kustaafia huwapata wastaafu watarajiwa walio wengi bila kuwa wamefanya utafiti wa kina.

Lakini acha nikupe angalizo la upande mwingine wa shilingi ambao wewe haujauangazia!

Kuna point moja tu hapo inayokusaga roho, ni ile hofu ya kushindwa kumsomesha shule ghali mwanao baada ya kustaafu!

Nitakuuliza kwa nini uhofie jambo dogo kiasi hicho wakati mchanganuo wako wa kutumia mafao yako upo vizuri, kama kweli umejipanga katika uwekezaji wa namna hiyo?

Mtoto wa kustaafia wala asikuhofishe bure, ni faraja aliyokuletea Mwenyezi Mungu unapoyakaribia maisha rasmi ya upweke!

Ukiisha kustaafu, urafiki wa maofisini hukoma rasmi, mke naye ashakuwa mbibi kachoka, inabidi umsaidie majukumu yake mengine!

Umri huo uliofikia na kwa kukiri mwenyewe, ushasomesha watoto zako hao na pengine washajitegemea kimaisha, hauishi nao hapo nyumbani.

Utakapostaafu, utabakia hapo wewe na "shemeji" tu jumba lote bila kitegemezi wa kuwafariji!

Ukiwa kazini, ulikuwa boss kuanzia ofisini hadi nyumbani ambapo ulikuwa umezungukwa na familia kubwa ya mke na watoto, sasa mmebakia wawili, uboss haupo tena mkuu kuanzia ofisini hadi nyumbani.

Kupata zawadi ya huyo mtoto sasa, mshukuru sana Mungu kwa kuwa umepata "pakushika" na mfariji wako mkubwa.

Cheo na hadhi ya mwanao huyo mchanga iko pale pale, ni "bwana mdogo", "ba'mdogo", "babu mdogo" nk nk, heshima yake haina mjadala na kwako ni utajiri wa familia, ambapo hautakosa kabisa watoto vyumbani mpaka mwisho wako.

Umepata faraja itakayokulinda mpaka ukikongwe wako ama mpaka kudaja!

60 kwa 20 utakuwa na 80 Mungu akikupa uhai.

Na shemeji anaonekana bado ni kijana kwa kukuletea hiyo faraja uzeeni isee!

Kumlisha mtoto mmoja, kumsomesha utakavyo na mahitaji mengine hayatakushinda maana vyanzo vya mapato rasmi unavyo.

Nimeitamani sana baraka hiyo uliyoipata wewe kama ingelikuja kwangu singelijuta, ningelishukuru sana Mungu.

Nimeandika nikiwa na uzoefu wa adha ya kuishi bila mtoto nyumbani baada ya kustaafu.

Pokea hongera za dhati kabisa na hofu ondoa, mtoto atakua kama kawaida na mahitaji umtakiayo atapata , Mungu ni mkubwa omba tu uhai.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…