Changamoto za kupata mtoto mchanga ukiwa umri wa kustaafu, unakuwa ni Baba Babu. Dawa ni kujipanga kabla, vinginevyo ni kubebesha watu mizigo yako

Happy birthday kaka Paskali
Hongera kwa familia kubwa na hongera zaidi kwa kuwa baba bora kwao

Uishi miaka mingine 50 yenye furaha zaidi👑🙏
 
Paskali hajajibu huyu junior, ni wa kutokea mke yupi??

Waliyepata naye watoto walio na watoto?? Waliyeishi naye miaka yote?!

Wanayeishi naye sasa!?
Ni wa wife wa Bongo yule cheupe. No.1 aligomea US, pale kati kukatokea watoto 3, ndipo akaolewa mama Junior, ana vibinti vitatu, na tuliisha amua watoto 8 ndio mwisho wetu and we were very careful, but it just happened, na sisi wote wawili ni devout Christians, Catholics, ni pro life and not pro choice, if it just happened, let it be.
P
 
Happy birthday kaka Paskali
Hongera kwa familia kubwa na hongera zaidi kwa kuwa baba bora kwao

Uishi miaka mingine 50 yenye furaha zaidi👑🙏
Amen mama D , asante sana, tena tulipokwenda US, when we were a young married family, baada ya mimi kushindwa kuwa Marioo, mimi ndio nilirudi na watoto, na kuwalea as a single parent father!. Most single parents ni mothers, ukiwa ni single parent father, na una mtoto wa kike anapoturn from a girl to binti, ni mtihani sana!. I passed this, hivyo kwa binti yangu wa kwanza, humwambii kitu kumhusu baba yake, wengine wananiita Mzee, Baba, lakini kwake I'm always Daddy!.
P
 
Watoto 9 dunia ya leo ni uchafuzi wa mazingira.
 
Hongera sana kaka Pascal Mayalla Sasa inabidi uanze Kwa kubadili ID ya JF isomeke Pascal Mayalla Sr.

Pili hongera sana Kwa ugeni, kwangu itabidi tutafutane kidume changu na chenyewe 08 April ndio siku yake ya kuzaliwa na tukio likitokea hapo hapo Aga Khan. Mama yao ni yule yule Dada Yako tulikutana pale Kontena, tukipata Maakuli.

Tatu na muhimu zaidi, ni wito na ushauri ulioutoa wa maandalizi ya kustaafu. Mwenye sikio na asikie.
 
Hongera sana mkuu,maisha ni safari ndefu,cha muhimu ni kumshukuru Mungu katika kila jambo.Hizi ni moja wapo ya nyuzi zako bora sana,hasa kwa siye tuliokula chumvi nyingi...
 
Watoto 9 dunia ya leo ni uchafuzi wa mazingira.
Mkuu Kiranga, sio kwamba tulipanga ,Mimi ni Catholic, haturuhusiwi kutumia birth control zozote zaidi ya natural ways, hivyo tumeiachia fate ndio imetupangia, hivyo kwa sisi pro life, iki happens, we let it be, ila ma pro choice ndio huchagua, kwao its about choice, hata iki just happens, wao wanaua, be it kuulia mbegu kwenye zile naniliu, au kuulia viumbe pale Marrie Stoppes!.
P
 


Ha haa! We mzee unatoa shule

Ha ha haa!.. nilichojifunza we mzee umejipanga watu wana ku criticize humu kwa wivu tu!..

Asante kwa shule ya mahusiano, malezi, uwekezaji, masomo, mapenzi etc. HAPPY BIRTHDAY MWANAHABARI USIE NA KINYONGO
 
Nimefarijika sana kusoma andiko lako, achilia mbali kucheka Kwa nguvu kutokana na maudhui yake. Mzima ndugu yangu?
Mimi mzima tu.

Vipi wewe?

Nimefikiria sana kuhusu exponential population growth itakayotokea ikiwa kila mtu atataka kuzaa watoto 9, na hao watoto 9 watake kuzaa watoto 9.

Ukianza na wazazi wawili, katika vizazi vinne tu unafikisha watoto wa kizazi cha mwisho 729.

That is.

2,9,81, 729.

You are talking about a 400 fold increase in population in just 4 generations!
 
Umepanga.

Hata kuwa kwako Catholic leo ni kupanga.

Na unaweza kupanga kutokubali ujinga unaofundishwa na kanisa.

Usisingizie hilo.

Kwani kila Mkatoliki ana watoto 9?
 
Hongera braza Pascal, umenipa fundisho kubwa tu, kwanza since I'm over 40, kutafuta watoto haipo kwenye mipango yangu, niliomba kuwa nikifika 40 niwe nimeshamalizana na habari za watoto.

Pili uwekezaji, very important hii kitu. Hizo gov't bond naona wengi sasa wanazikimbilia, elimu imeongezeka. Tatizo ni pesa tu.

Happy birthday kwako na kwa jnr!
 

Nipo salama kabisa kaka. Japo amejitahidi kujieleza jinsi ilivyotokea Hadi kuwa na watoto 9 lakini Bado haikua lazima iwe hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…