Changamoto za kupata mtoto mchanga ukiwa umri wa kustaafu, unakuwa ni Baba Babu. Dawa ni kujipanga kabla, vinginevyo ni kubebesha watu mizigo yako

Changamoto za kupata mtoto mchanga ukiwa umri wa kustaafu, unakuwa ni Baba Babu. Dawa ni kujipanga kabla, vinginevyo ni kubebesha watu mizigo yako

Mkuu taratibu basi, mazingira yenyewe, hayana mwenyewe si tunaambizana hakuna Mungu!
Nimecheekaaah Sana daah! Akili kubwa ndiyo hizi
Kama hakuna Mungu basi ndiyo sisi tuna wajibu mkubwa zaidi wa kutunza mazingira.

Maana hatutaweza kumuomba Mungu atutunzie mazingira.

Na moja ya njia za kutunza mazingira ni kuacha kuzaana kama sungura.

Kuwa na watoto wengi ni moja ya sababu kubwa kabisa zinazoongeza uharibifu wa mazingira.

Ila Afrika hususan kuna watu wengi hawafikirii hili, ni wabinafsi, wanawaza pafupi tu.
 
Kama hakuna Mungu basi ndiyo sisi tuna wajibu mkubwa zaidi wa kutunza mazingira.

Maana hatutaweza kumuomba Mungu atutynzie mazingira.

Na moja ya njia za kutunza mazingira ni kuacha kuzaana kama sungura.

Kuwa na watoto wengi ni moja ya sababu kubwa kabisa zinazoongeza uharibifu wa mazingira.
Bahati mbaya dunia haiongezeki, eneo, iko vile vile!
 
Bahati mbaya dunia haiongezeki, eneo, iko vile vile!
Kwa kasi hii, kila mtu akizaa watoto 9 by the age of 60, ndani ya miaka takriban 250 tutahitaji dunia zingine 400.

Kwanza kuzaa ukiwa mzee ni ukatili kwa watoto.

Mpaka mtoto anaona aibu kusema huyu baba yangu, anadanganya huyu babu yangu!
 
Yale yale ....kila mtoto anakuja na riziki yake...wabongo bwana tuna misemo ya kijinga sana. Ndio yale ya mtoto wa kuzaliwa nje ya ndoa tunasema mtoto ni baraka kutoka kwa mungu.

Tuache ujiinga bwana mtoto haji na riziki yake. Mtoto anaandaliwa mpaka anakuwa mtu wa maana kwenye jamii. Haya mambo ya fyatua and hope for the best tuyaache. Hii misemo yakifala sana
Kuna shule darasani wanakaa watoto 20 tu, ukitaka mtoto apate nafasi unamuandikisha mara tu akishazaliwa. Na uwe na uhakika wa ada yake mpaka anamaliza shule.
 
Leo Ijumaa ya Tarehe 8 April, ni siku yangu ya kuzaliwa, nikiwa nimeipiga mingi nikikaribia 60! ambao ndio umri rasmi wa kustaafu, nikiwa tayari ni father of 8 +1= 9, Grand Pa of 6, and about to retire!.

Sababu ya makala hii ya leo sio kusherehekea siku yangu ya kuzaliwa, bali kutoa mbinu za changamoto za ulezi katika umri mkubwa kwa huku unajiandaa kustaafu, huku vichanga vinaendelea kuzaliwa!.

Naomba kutoa taarifa ya ujio wa mgeni mwingine kwenye familia yangu, ujio wa mgeni huyu, ume concide na tarehe yangu ya kuzaliwa, mgeni huyu mpya, amebisha hodi Duniani Leo, 8 April, 2022 majira ya saa 4:00 asubuhi, katika hospital ya Aga Khan, na kwa vile mgeni mwenyewe ni kidume, hivyo nimetoa jina langu la Pascal, hivyo ataitwa Pascal Mayalla, Jnr na kuanzia leo mimi nimebadili jina na kuwa Pascal Mayalla Snr baada ya ujio wa Pascal Mayalla Jnr.

Kupata mtoto katika umri mkubwa kama huu, kuna changamoto zake, changamoto ya kwanza, ni watoto wangu wakubwa tayari wana watoto, yaani mimi ni Babu, halafu unapata mtoto mdogo kuliko mjukuu, hivyo kwa wajukuu wa watoto wangu wa kiume, huyu Pascal Mayalla Jnr ni baba yao mdogo na wajukuu wa mabinti huyu ni mjomba wao, baba mdogo na mjomba kuwa ni mdogo kuliko wajukuu, haupendezei kivile!.

Kuna watu wataona ni ajabu kwa mtu over 50 kupata mtoto, japo nikweli sio kawaida sana, watu wanajenga familia wakiwa vijana, ukifika miaka 50 ni umri wa kujiandaa kustaafu na sio tena kuanza kulea na kuitwaa baba wakati umri ni wa babu, lakini amini usiamini, kupata mtoto at 50 plus ni kawaida sana, tuna mfano mingi tuu, ukitafuta umri wa Chief Burito wakati Julius Kambarage Nyerere anazaliwa, hutashangaa!. Hata Nabii Ibrahim alipomzaa Isaka alikuwa na miaka 90!. Mfano mzuri wa karibu ni yule Mzee wetu fulani, Al maarufu na mashuhuri, alipata watoto twins at 74 years!, hivyo mimi kupata mtoto at 50 plus, mimi ni bado sana!, ila huyu ni last born!.

lengo la makala hii ya leo ni kutoa somo la kujiandaa kustaafu, ili ustaafu bila stress. Kitendo tuu cha mstaafu mtarajiwa kupata mtoto at 50 +, hiyo peke yake tayari ni stress tosha, kwasababu mtoto anatakiwa kutimiza the age of majority, akiwa total dependant. Pesa za mstaafu, haziwezi kumlipia shule nzuri mtoto, unless nikubali akasome St. Kayumba!. Kama hao wenzake 8, hakuna aliyesoma St. Kayumba, hivyo huyu kitinda mimba wa Baba Babu, needs a little bit kujipanga zaidi. Hivyo makala hii, itakuwa ni msaada mkubwa sana kwa wale wote wenye umri mkubwa, huku wakikabiliwa na changamoto za ulezi.

Kutokana na maandalizi duni ya kustaafu, wastaafu wengi hujikuta hawana vitega uchumi vya kutosha kuwa sustain baada ya kustaafu, hivyo kuishi maisha ya stress, wengine kusumbua watoto kwa kupiga muzinga, hali inayopelekea ikiona tuu simu ya dingi, unahisi ni mzinga, hivyo ukijiona uko apeche alolo, unaogopa hata kupokea simu ya dingi ukidhani ni mzinga!, kumbe simu nyingine wala sio mizinga, ni dingi amekukumbuka tuu na anakupigia ili kukusalimia tuu.

Kitu kinacholeta stress kubwa Kwa wastaafu wengi, ni wengi kutofanya biashara yoyote wakati wa utumishi wao, halafu akiisha staafu yale malipo ya pensheni ya mkupuo kuyatumia kama mtaji wa kuanzisha biashara, biashara isipokwenda vizuri, matoi yake ni kupata stress, kuchoka mapema na kuchakaa, na hapo hapo maradhi ya depression na mwisho ni kufa mapema kwa ma pressure, heart attacks, maumivu ya viungo, organ failure etc.

Ili kuzuia stress za kustaafu, kama unapanga kufanya biashara fulani baada ya kustaafu, start small!, anza kidogo kidogo ukingali kazini kupata uzoefu wa kutosha ukiona unaweza ndipo ukistaafu ujikite zaidi.

Ushauri wangu wa the best way ya kustaafu, ni zile fedha za mafao yako ya kustaafu ambayo umelipwa kupitia benki, wastaafu wengi huziweka fedha hizo Benki kama akiba, na kuzitumia kidogo kidogo.

Kitendo cha fedha hizo kukaa Benki kwenye account ya savings, faida yake ni kiduchu Sana. Zingekaa kwenye a fixed deposit account, FDA, zingezalisha faida kubwa kidogo, lakini mpango mzima wa ukweli na wa uhakika wa uwekezaji wa mafao yako ni Kwa kuwekeza Kwa ununuzi wa dhamana za serikali, yaani Government Bonds, ambazo huuzwa na Benki Kuu ya Tanzania ambapo hutoa riba ya mpaka asilimia 16%!.

Sasa tupige hesabu ya Pamoja.
Tuseme mafao yangu ya kustaafu ya mkupuo ni milioni 100. Nikinunulia Government Bonds za miaka 25, kila mwaka nitapata shilingi milioni 16. Bonds wanalipa gawio mara 2 Kwa mwaka, kila baada ya miezi 6. Hivyo nitalipwa shilingi milioni 8 kila miezi 6.

Ukiisha nunua bonds zile Bondi certificate ni dhamana ya uhakika ya kupata mkopo Benki yoyote kufanyia biashara yoyote.

Nakushauri, fanya utaratibu na Benki yako, badala ya kusubiri kupokea gawio lako la milioni 16 kwa mwaka, unaomba ulipwe shilingi milioni 1,300,000 kila mwezi kwa muda wa miaka 25, bado wewe mstaafu utakuwa na stress au kusumbua kupiga mizinga watoto?.

Wastaafu wenzangu watarajiwa, ni muhimu sana kupanga uzazi, ni muhimu kupanga familia, ni muhimu kujipanga kustaafu bila stress, ila ikitokea umepata ugeni kama wa Pascal Mayalla Jnr, mida ya machweo, mpokee tuu mgeni with positivism after all kila mtoto anakuja na rizki yake,
Karibu Pascal Mayalla Jnr.
Happy Born Day Pascal Mayalla Jnr
Happy Birthday Pascal Mayalla Snr
Paskali
Update ya Kilichopelekea Kuendelea Kutengeneza Watoto Post 50 Years!.

Mkuu Goldschmidt , kwanza asante sana kwa kuwa mkweli, bonafide genuine, watu huwa hatupendi kuambiwa ukweli mchungu, hiki ulichosema hapa ni ukweli mchungu!.

It's true watoto 8, now 9 ni wengi. Mimi ni a modern man, niliao a classmate sweetheart Mimi nikiwa at 25 years mwenzagu 21, tukahama nchi kwenda UK tukapata mtoto wa kwanza a girl then tukahamia US tukapata mtoto wa pili, a boy tukaamua that is it. Hatuhihitaji tena kuongeza watoto.

Wife akapata full sponsored fellowship ya 4 years US mimi ndio niwe house husband na babysitter wa watoto wetu wawili. Very unfortunately, nilishindwa nikamwacha wife US na kurudi Bongo.

Long distance relationships doesn't work well Kwa baadhi ya makabila, so does maisha ya u Marioo, yaani mke ndio mwenye kazi, pesa, mimi niwe Marioo. Wasukuma ni one of such tribes.

Hivyo niliporudi kuishi bongo huku wife US, nikajikuta wametokelezea watoto 3. 2 boys and a girl hivyo I had 5 kids. (naomba usiulize ufafanuzi wowote kuhusu hawa watoto 3).

Wife baada ya kumaliza shule with news ya uwepo wa watoto 3, wife akaamua kugomea US hivyo mimi nikawa sina jinsi bali kurudi Bongo na kuendeshea na life.

Mwaka 2008 I suffered a bad motor accident, I was confirmed to a wheelchair!. Hapa akajitokeza kabinti fulani with a heart of gold, she came with love and care , kiukweli mtu ukiwa invalid confined to a wheelchair, akatokea mtu kupenda hivyo ulivyo, ni very rare and amaizing love.

She told me something was telling her tukijaribu pengine, nitaweza kupona. She made some efforts tukahangaika huku na kule, tukaenda South gharama zikatushinda , tukaenda India, ndiko nilikoponea na kusimama tena!.

Baada ya kupona na kurudi Bongo,
kwanza nitoa shukrani kwa yote niliyopitia

nikajikuta zawadi pekee kwa huyu binti ni ndoa, hivyo 2010 nikaoa tena, by then nikiwa over 40!.

Kabinti kakanizalia 3 beautiful daughters the number was 8, ilipotokea tena dalili ya ugeni, we didn't say no, then ndio hiyo jana kaleta kidume, na kiukweli hapo sasa ndio mwisho.
P
Mbona husifii mkuu mayala .. sikuon ukisema kauli ile ya anau..... Mwing
 
Happy birthday PM Snr Mungu akuweke Sana umlee kijana PM jnr vizuri
Sijui kwann? Nmetoka kukuappriciate Sana jinsi ulivyo mkweli hongera brother
Asante Sana Mkuu Hon Nkundwe , mimi hivi ndivyo nilivyo, niko very honest, frank, trustful, truthfully, very open and very transparent.

P.
 
Amen mama D , asante sana, tena tulipokwenda US, when we were a young married family, baada ya mimi kushindwa kuwa Marioo, mimi ndio nilirudi na watoto, na kuwalea as a single parent father!. Most single parents ni mothers, ukiwa ni single parent father, na una mtoto wa kike anapoturn from a girl to binti, ni mtihani sana!. I passed this, hivyo kwa binti yangu wa kwanza, humwambii kitu kumhusu baba yake, wengine wananiita Mzee, Baba, lakini kwake I'm always Daddy!.
P
Huyu mke wa Marekani yuko wapi kwa sasa?
Hao watoto mliozaa nje ya nchi wameamua kuchagua uraia wa nchi gani?
 
Kwa kasi hii, kila mtu akizaa watoto 9 by the age of 60, ndani ya miaka takriban 250 tutahitaji dunia zingine 400.

Kwanza kuzaa ukiwa mzee ni ukatili kwa watoto.

Mpaka mtoto anaona aibu kusema huyu baba yangu, anadanganya huyu babu yangu!
Miaka 60 siyo mchezo, huyu Paskali siyo Mayalla, hakuna njaa hapo!
Mwenye shibe pekee ndiyo aweza kufanya hivyo!
Wengi siku hizi umri huo, anywe panadol, betri wabust na sulphuric acid! Taabu tupu
 
Umepanga.

Hata kuwa kwako Catholic leo ni kupanga.

Na unaweza kupanga kutokubali ujinga unaofundishwa na kanisa.

Usisingizie hilo.

Kwani kila Mkatoliki ana watoto 9?
Kiukweli kuwa M Catholic sikupanga imetokea tuu nimezaliwa nikanikuta nimezaliwa kwenye I Catholic.

Pili nakubalina na wewe, kuna ujinga mwingi kwenye baadhi ya mafundisho ya dini ya baadhi ya madhehebu tukiwemo sisi Wakatoliki.

Catholics, haturuhusiwi kutumia any birth control zozote, hivyo wa Catholics wowote wanaotumia kinga yoyote, including withdrawal ni dhambi!.

Hivyo kuna Catholics wengi wanatenda sana dhambi za mauaji ya watoto watarajiwa wakiwa kwenye stage ya mbegu.

Kwangu ni afadhali kuangamiza mbegu ili kuzuia kuliko kuua kiumbe baada ya kutungwa!.
Hivyo kwetu it just happened and we had choice to terminate it, but sisi, both of us, mimi na wife wangu ni ma pro life sio ma pro choice.
P
 
Huyu mke wa Marekani yuko wapi kwa sasa?
Hao watoto mliozaa nje ya nchi wameamua kuchagua uraia wa nchi gani?
She is a US subject, both of them ni US Subject, wa kike ni like mother like daughter, hana mpango na bongo, my boy ni like father like son, nasubiria uraia pacha atimbe Bongo.

Somo jingine zuri Kwa wapenzi wapya it's very good to be friends with opposite sex before you becomes lovers, yaani jenga kwanza urafiki, so that you are friends before you are lovers, such that, even if you can't be lovers anymore, you can still be friends. She is now, a very good friend of mine.
P
 
Belated wishes to you & Jr.
Have a wonderful year ahead filled with gorgeous moments.
Article imetulia.
Jamani my dearest BelindaJacob!, long time!. Kiukweli you are my first JF love nilipojiunga jf nilikupenda, na ile zawadi ulioniletea siku ya birthday yangu Ile, sijabahatika kukutana nayo popote!.

Ukija tena Bongo, let's hook around, enzi zile Samaki Samaki was the only place, now Dar kuna hundreds places to hook around, ukija nitakupeleka Kidimbwi.

Glad to hear from you after such a long time!.
P
 
Pasco, umezaa na mkeo? Watoto 8 ni wengi sana. Wanatumia financial, physical and emotional resources nyingi sana kuwahudumia na kuwalea. I think it wasn’t the wisest decision for you to have a baby at this point in your life. Hapo umefulia mzee. Big time.
Mbona kaeleza Kila kitu, hujasoma Uzi wote uncomment. Kasema :
US ana 2
Bongo one kapiga 3
Bongo two kapiga 4
Haya jumlisha uone kama kazaa na mke mmoja watoto 8.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Paschal kweli uzee umefika, umeacha kukimbizana na 'totoz'?
HBD
Mkuu platozoom , kuniambia nimeachana na kukimbizana na totoz, ni kunionea, kiukweli kwa Bongo, ukiwa nazo, good looking, well dressed, good job, gari zuri, kiukweli kabisa totoz ndio zinakuja zenyewe, wewe ndio unawakimbia!.
Naomba nikupe ushuhuda
Nimejiunga UDSM fol nikiwa 'loaded' just imagine vile videmu bomba vya chuo vinavyotegemea boom!. Nilikuwa naishi Block F, Mabibo Hostel, single room!. Hivyo ningekuwa ni kweli ni mzee wa totoz, ningewatafunaje?!. Amini usiamini, nimemaliza miaka yote 4, bila bila!. Yaani bila kutafuna kifaranga chochote cha UDSM!.
P
 
Asante kwa somo zuri!
Lakini hata hivyo huwezi kuzuia mpango wa Mungu wa kuleta mtu anayemtaka duniani hata kama ungekuwa na miaka mingapi! Kwa hiyo hongera kwa kupata mtoto,mengine mwachie Muumba.
 
Back
Top Bottom