Changamoto za mfumo wa maombi ya ajira za Elimu na Afya 2022

Wakuu mkijaribu kufungua vyeti vyenu huko inakuaje? Mimi nimejaribu wanaandika failed to read file
 
Mkuu mimi nimechagua kwanza shule nikasave kwa pamoja ndio nikaweka barua.

Sasa nilikuwa nataka nibadilishe barua niweke nyingine maana kuna sehemu nimegundua makosa.

Je nikiweka barua mpya nitatakiwa na shule nichague upya?
Hakuna mtu anayesoma barua Tamisemi narudia hamna anayesoma barua 120k
 
Kwa upande wa taarifa za chuo kama umekosea unaweza kubadilisha?
kwa computer ndio rahisi....
utabonyeza hapo kama picha inavyoonyesha...



ukishabonyeza hapo itafunguka....kama kiambata kitakavyoonyesha hapo chini...kisha utabonyeza hiyo alama iliyozungushiwa duara
utabadilisha taarifa zako kama unavyo taka kisha unasave...
au....unaingia
kwa kubonyeza kama picha inavyoonyesha
harafu unaondoa hiyo taarifa kwa kubonyeza sehemu ya ondoa...baada ya hapo unaweka taarifa zako upya
ukishindwa niambie haraka iwezekanavyo...ila usisahau kuwa hayo yote yanawezekana kwa urahisi ukitumia computer...kwenye simu sina uhakika
 
weka geography...baada ya hapo chaguo shule zako 2 au tatu kisha rudi kaifute geography...harafu nenda kaongeze shele zako za economic...mpaka hapo utakuwa umewaweza..awawezi kutuzingua
 
tatizo sugu kwa ndugu zangu wa kada ya afya...kwakweli hili tatizo nimehangaika nalo ili niweze kuwasaidia baadhi ya marafiki zangu mnao jaribu kuomba ila nimeshindwa...tutegemee kudra za mwenyezi Mungu...tamisemi walitatue hili tatizo mapema....mikoa haifunguki...kwa baadhi ya kada
 
Ukishindwa wewe usiseme ni tatizo sugu. Ulizia kwa anaejua mbinu mbadala uelekezwe huwezi jua vyote kwenye hii Dunia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…