KERO Changamoto za rushwa na ukiritimba wanaokutana nao Wajawazito katika Kituo cha Afya cha NYASUBI , Kahama

KERO Changamoto za rushwa na ukiritimba wanaokutana nao Wajawazito katika Kituo cha Afya cha NYASUBI , Kahama

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Joined
May 30, 2025
Posts
47
Reaction score
71
Ndugu Watanzania, kumekuwa na malalamiko kuhusu ukiukwaji wa haki za wajawazito kupata huduma za afya, ambapo baadhi yao wanalazimishwa kulipia vipimo ambavyo vinapaswa kutolewa bila malipo.

Vipimo vinavyodaiwa kulipishwa ni pamoja na:
  1. Hemoglobin (HB) – kipimo cha kiwango cha damu.
  2. ABO/Rh – kipimo cha kutambua kundi la damu.
  3. Syphilis – kipimo cha kaswende.
Kwa mujibu wa mwongozo wa Wizara ya Afya, huduma za afya kwa wajawazito zinapaswa kutolewa bila malipo. Hata hivyo, kumekuwa na baadhi ya wajawazito na watoto walio chini ya miaka mitano kulazimika kulipia huduma ambazo zinapaswa kuwa bure kwa makundi hayo.

Pia, kumekuwa na vitendo vya rushwa na ukiukwaji wa taratibu katika maeneo ya malipo. Kwa mfano, mgonjwa anaweza kuambiwa huduma au dawa fulani inagharimu Sh10,000, na anapopewa control number anaelekezwa kulipa kupitia kibanda cha wakala kilichopo ndani ya kituo hicho. Baadhi ya walalamikaji wanadai kuwa baada ya kufika kwenye mfumo wa malipo wa Serikali, kiasi kinachoonekana kinaweza kuwa Sh5,000, lakini wanaelekezwa kulipa Sh10,000.

Ikiwa madai haya yatathibitishwa, yanaweza kuashiria ukiukwaji wa taratibu za malipo na matumizi mabaya ya fedha za wananchi.

Kwa hiyo, naiomba Wizara ya Afya na mamlaka nyingine husika kufanya uchunguzi wa kina, kubaini ukweli wa madai haya na kuchukua hatua dhidi ya watakaobainika kukiuka taratibu, ikiwemo kuwawajibisha au kuwafutia leseni watoa huduma wanaohusika.

Wananchi wanastahili kupata huduma za afya kwa haki, uwazi na bila kulazimishwa kulipa fedha zisizostahili.
 
Naomba mamlaka husika zichukue hatua za haraka kudhibiti vitendo vya rushwa na udanganyifu vinavyodaiwa kufanyika katika maeneo ya malipo na mapokezi ya baadhi ya vituo vya afya, ambavyo vinawaweka wagonjwa katika mazingira ya kunyanyaswa na kupoteza fedha zao.

Inadaiwa kuwa wakati mwingine mgonjwa anaambiwa huduma inagharimu Sh50,000, lakini anapofika mapokezi anaelekezwa kulipa Sh60,000 kupitia wakala wa huduma za fedha aliye ndani au karibu na kituo. Hii inaibua mashaka kwamba tofauti ya Sh10,000 inaweza kugawanywa kati ya wahusika.

Tatizo hili linaonekana kuwaathiri zaidi wananchi ambao hawajui kutumia mifumo ya malipo kwa njia ya mtandao kama M-Pesa, Airtel Money na huduma nyingine za kidijitali. Inadaiwa kuwa mfumo wa Serikali unaweza kuonyesha kiasi cha Sh5,000, lakini mgonjwa akaelekezwa na mtoa huduma kulipa Sh10,000 kwa wakala. Baadaye, risiti inayotolewa huonyesha kiasi cha Sh5,000 pekee.

Ikiwa madai haya yatathibitishwa, ni udanganyifu mkubwa unaopaswa kuchunguzwa na kuchukuliwa hatua. Naomba mamlaka zifanye uchunguzi wa kina, hasa katika maeneo yafuatayo:
  1. OPD
  2. Dirisha la mapokezi
  3. Maabara
Ni muhimu kuhakikisha mfumo wa malipo una uwazi na wagonjwa hawatozwi zaidi ya kiasi kinachoonekana kwenye mfumo rasmi wa Serikali.

Naiomba mamlaka husika kuchunguza madai haya na kuwawajibisha watakaobainika kuhusika. Wananchi wanastahili huduma za afya zenye uwazi, uadilifu na bila udanganyifu wa kifedha.

Natumaini suala hili litashughulikiwa ipasavyo. Asante JamiiForums.
 
Nyabusi au Nyasubi??Hebu fafanua... NYABUSI ni kama unataja- Mbususu- vile...!😛🥰
Poleni lakini ..CCM wako busy na Simu za Nchimbi kwa sasa.. na kuwabambikizia CHADEMA kesi za Ugaidi....muwe na subira ...mtafikiriwa....
 
Nyabusi au Nyasubi??Hebu fafanua...
Poleni lakini ..CCM wako busy na Simu za Nchimbi kwa sasa.. na kuwabambikizia CHADEMA kesi za Ugaidi....muwe na subira ...mtafikiriwa....
Itakuwa Nyasubi,aombe moderators wahariri hiyo heading.
 
Namba ya mganga mfawidhi wa NYASUBI health center, anayefadhili ukilitimba wa kuwatoza wajawazito,0785401957 naaminia Jf italeta matokeo haraka zaidi
 
Nyabusi au Nyasubi??Hebu fafanua... NYABUSI ni kama unataja- Mbususu- vile...!😛🥰
Poleni lakini ..CCM wako busy na Simu za Nchimbi kwa sasa.. na kuwabambikizia CHADEMA kesi za Ugaidi....muwe na subira ...mtafikiriwa....
Moderate hariri iwe NYASUBI badala ya nyabusi
 
Back
Top Bottom