Changamoto za uke wenza

Changamoto za uke wenza

Mimi nisingependa kuongelea swala la kuongezewa mke mwenzie maana tayari ndio ameshaongezwa,nadhani cha kufanya kwanza huyo rafiki yako atueleze vizuri ni ugumu upi anaouzungumzia,ikibidi atuweke wazi kabisa ili tujue jinc ya kumsaidia,mbali na hapo itakuwa ngumu ni sawa na kutafuta kijiwe baharini...halafu nahisi kama mlengwa ni wewe mwenyewe kwa nini usiwe muwazi ili usaidiwe??
 
Jamani samahani kupotea huku nimeanzisha mada kuomba uzoefu wenu.Ntajarribu kujibu maswali yenu kama ifuatavyo:

1.Shosti hakukubali kuolewa mke wa pili.Yeye ndio wa kwanza na walikubaliana pamoja na imani yao kuruhusu mitala, wataishi ndoa ya mke mmoja tu.Wameishi miaka 10 na wana watoto wawili.Shosti ana kazi nzuri tu yenye kumpatia kipato ila siyo cha kutegemea kumudu kila kitu peke yake. Watoto ni wakubwa - miaka 9 na 7 na wanasoma shule nzuri hizi mnazoita "academy" au "international".

2. Mume wake kama kawaida kaoa kumstukiza tu kwa kisingizio cha kuruhusiwa kidini.Hajafuata utaratibu wowote na wala hakuwa na sababu ya msingi kivile ya kumuolea mke wa pili.Shosti alianza kuona mabadiliko tu ndani ya nyumba, mume kuchelewa kurudi nyumbani, matumizi kupungua kwa yale mahitaji aliyokuwa anayatoa yeye mume.Miradi yao ikasinzia.Baada ya kuchunguza ndipo akagundua mume kaoa! Kumuuliza mwanzoni alikataa lakini baadae akakubali tena kwa jeuri ya ajabu akisingizia dini inamruhusu.Mawifi ndio wamekuwa kidomodomo kuchochea maugomvi.

3. Shosti amefikiria sana, akataka hata kuachana na mumewe lakini ndugu zake wanamtia moyo kwamba avumilie maana mume yuko sahihi.Shosti anataka kujua wale wanaovumilia huwa wanajipanga vipi? Na je, kunakuwa na uhakika gani kwamba mke mwenza atakuwa muaminifu hataleta magonjwa kwenye ndoa ?
 
Kazi anayo.
Kumbe hata huyo mke mwenza aliletewa bila taarifa? Mi nilijua hua wanakubaliana. Nwy mpe pole!!
 
Nadhani dini inataratibu zake na hutoa ruhusa sahihi kuoa mke wa pili, na mke wa kwanza ananafasi yake ya kuridhia. Ndoa ya pili sio ya kificho na ya kubalika kidini - si kwa kuwa umependa tu kuoa mke wa pili basi unao. Kwa upeo wangu finyu, unao pale ambapo kuna mahitaji ya kufany hivyo - kupata mtoto au jinsia unayotaka wewe, mkeo mgonjwa, umesafiri uko mbali. Na hiyo yafanyike kwa utaratibu wake na uwe na uwezo wa kuwatosheleza wakeo sawa.

Lakini hapa inaonekana swala sio mke wa pili tena. Maana ameshaingia na shoti kutokana na ushauri wa nduguze anataka kuendelea kuwepo. Kuna mambo mawili hapa, kwanza aache kupambana - hili joto la hasira lipite. Kwa kuwa anakazi yake basi ajaribu kutumia hicho kidogo alichonacho kujikimu - kwahiyo tunaondoa magomvi ya matumizi.

Pili kunaswala la kukubali na kujiwekea taratibu na masharti anayoyaona yanamfaa yeye - ratiba za mambo yao ya ndani na matumizi yao. Maana, asibaki anapambana kwanini kao wakati mtu keshaolewa - sasa yeye aseme mumewe anapaswa kufanya ni na nini kwake.
 
Mimi nisingependa kuongelea swala la kuongezewa mke mwenzie maana tayari ndio ameshaongezwa,nadhani cha kufanya kwanza huyo rafiki yako atueleze vizuri ni ugumu upi anaouzungumzia,ikibidi atuweke wazi kabisa ili tujue jinc ya kumsaidia,mbali na hapo itakuwa ngumu ni sawa na kutafuta kijiwe baharini...halafu nahisi kama mlengwa ni wewe mwenyewe kwa nini usiwe muwazi ili usaidiwe??

Laiti ingelikuwa ni mimi maana najua haswa kile ambacho ningefanya.Kwa kuanzia ndoa yangu ni ya serikali na haina cha mke wa pili wala wa tatu.
Pili ninajua haswa ninachotaka.Uke wenza ni NO!NO!NO! Ingetokea wala simpi nafasi kuja kunisukasuka na huyo mke wake wa pili.

Tatu, nisome vizuri kwenye mada yangu hii hapa :https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...nafasi-ya-mahakama-ya-kadhi-kwa-wanawake.html

Utanielewa vizuri kwamba najua kinachotakiwa na kinachonipasa.Shosti tumeshaongfea sana na sababu ya kunitaka ushauri ni kwa vile anajua ninachojua.Ushauri wangu utakuwa too radical for her na kwa sababu hiyo ametaka kujua wengine waliokubali hali wanaishi vipi.Anachohitaji siyo kupewa pole bali kupewa mbinu na mikakati ya kujaribu kuishi hayo maisha mapya.
 
Ndo shida ya uvivu wa kufanya proof reading! Wakati wa honeymoon kamata hiyo cheti tik chwaa! Kama walitiki huenda ikawa ya wengi unatiki boksi zote afu kura inakuwa imeharibika!
daah siwezi kugawana mapenzi huku nikijua!

Hivi ukiwa unaolewa, kile cheti cha ndoa si kuna mahali unajaza ndoa ni ya mke mmoja ama wengi.....sasa kama yeye alikubalina na kuwa itakuwa ya wake wengi basi she volunteered her own injury!
Btw; kwa wale wenye kuruhusiwa mke zaidi ya mmoja, si unaweza pia kusema ni ya mke mmoja kama huna lengo la kuoa wengi! Black Rose hapa utanisaidia najua hapa una uelewa ziadi yangu.
 
Enyi makundi ya vijana, Mnapofikia umri na kutaka kuoa, basi oeni wa4, wa3 w2, Lakini kwa ajili ya uadilifu basi owa 1. Swali hapa ni kama ano uwezo wa kiafya kuwamudu wote basi kwa duwa na sala vingine kama mali watoto na maisha mazuri inawezekana. Rudi kwa mwenye enzi mungu na asali itikhara na ataonyeshwa njia ya utatuzi wa shida alizo nazo Hazina ya mwenye enzi mungu haijapunguwa.
 
Naona hakuna mtu anayeishi na mkemwenzie humu! Mwambie afuate moyo wake; that's all l can say!
 
Ina maana hakuna wenye kuishi kwenye mitala humu JF?
Au hii mada imetonesha vidonda kiasi kwamba watu wameamua kukaa kimya?
 
Maisha ya ukewenza, sio maisha bali bp.
hata siku mja mtu huwezi kuridhika kutoka moyoni,kugawana mapenzi.
kitendo cha kumuoa mwanamke mwingine kwa uwazi na kukujulisha na pengine kumleta kwenye nyumba unayoishi w, tayari hapo mapenzi yamekwisha.
hakuna dawa yoyote hapo zaidi ya kusepa.
 
Afanye kazi kwa bidii....anachoweza kufanya ni yeye kama yeye kujaribu kubadili hali ya kipato ilivyo.

Pole yake....mke wa pili si hawara,ana haki sawa,ipo kazi hapo!
 
Ndo shida ya uvivu wa kufanya proof reading! Wakati wa honeymoon kamata hiyo cheti tik chwaa! Kama walitiki huenda ikawa ya wengi unatiki boksi zote afu kura inakuwa imeharibika!
hahaha muda wanao, watu wanamwaga tu wino bila kujali, alimradi ni cheti cha ndoa. Ngoja siku wasaini karatasi za kunyongwa!!
 
Kwa vile shosti wako ameridhia huo ukewenza k?akubaliane na hali halisi.

Ajijenge mwenyewe, kiuchumi awe na mali zake bila kumtegemea mume, hata mahitaji yake ya nyumbani, la sivyo mwanaume atamsumbua, ahakikishe anakuwa na uwezo wa kuwasomesha na wanae, nk

Ndugu wa mume ni vishanshada siku zote inajulikana, awaignore, afocus kwenye maisha yake na wanae

Kuhusu maradhi, hapo kuna mawili amuombe Mungu amwepushe na maradhi huku aende kupima, na amwambie mumewe na ,ke mpya wakapime, au amwombe Mungu amuepushe na maradhi na azungumze namumewe kujikinga /kutumia condom(ambalo mume hatoafiki), au wasingonoke kabisa na mumewe(na ndoa yenyewe ndo itakua imeishia hapo)

Kiufupi mwambie mwenzio ajipange ajenge maisha yake nawanae, awatafutie wanae chao, kuepuka migogoro, asimtegemee sana mumewe na aji-tune kuwa mume ni wa kushare


mpe pole, inawa ingekuwz mie ningevuta nyumba ndogo ya kuniliwaza mume akiwa zamu kwa bi mdogo lohhhh
 
Uke wenza siyo maisha,
mapenzi hakuna,
hujui hata mwanaume kalala wapi,
dharau huwa nyingi,
hata uwezekano wa kupata marazi ni mkubwa sana.
kama anajiweza aanze mdogo mdogo.
si kweli ulichoandika. unaweza ukawa na wake wawli na wote ukawapenda bila kubagua.
 
Sasa matatizo yako wapi? kwani mwanaume akioa mke wa pili ndo matatizo yanakuja, hata kama angekuwa na yeye tu matatizo yatakuja tu.

Mimi naona atulizane tu huyo shost wako, mana akifanya fujo atatwanga talaka mambo yataisha.

 
hmmmmm......mie naona sononi na hasira mtu aliyempenda kachukuliwa ndilo linalomsumbua,lol mwambie ajikeep busy mind yake na mwili kwa kufanya mazoezi kutafuta new hobbies kama swimming,kulima bustani ndogo ndogo etc this way she wont feel much pain!!!........,kuhusu kipato avumilie kutumia chake, na kidogo anachopata kutoka kwa mumewe,kama hakitoshi atafute source ya income kwa kufanya ujasiriamali lol.........mpe moyo hili lisisumbue aconsetreti kny malezi ya wanae na future yao.....maanake kama hili limemsumbua,basi ujue watoto limewasumbua zaidi.....they need someone they can turn to.......mwambie asiloose focus...future ya watoto ikaharibika.............agangamale for the sake of their kids.
 
kuhusu maradhi, hapo kuna mawili amuombe Mungu amwepushe na maradhi huku aende kupima, na amwambie mumewe na ,ke mpya wakapime, au amwombe Mungu amuepushe na maradhi na azungumze namumewe kujikinga /kutumia condom(ambalo mume hatoafiki), au wasingonoke kabisa na mumewe(na ndoa yenyewe ndo itakua imeishia hapo)

YAANI! Utadhani ulikuwepo akihadithia madhila yanayomkuta. Kinachompa shida kuliko vyote siyo pesa, wala nini,Ni hapo tu pa kushare hiyo kitu! Bwana kutumia condom kagoma katakata hadi imebidi bi dada akapime na kujihakikishia salama.Mwisho wa mchezo umeishia hapo.Hata zamu haoni haja maana hamhitaji huyomume kwa lolote isipokuwa kuwa kwenye maisha ya wanawe ambao bado wadogo.


mpe pole, inawa ingekuwz mie ningevuta nyumba ndogo ya kuniliwaza mume akiwa zamu kwa bi mdogo lohhhh
Hapo sasa...mhhhh...hebu tusikie wengine watasemaje lol
 
Sasa matatizo yako wapi? kwani mwanaume akioa mke wa pili ndo matatizo yanakuja, hata kama angekuwa na yeye tu matatizo yatakuja tu.

Mimi naona atulizane tu huyo shost wako, mana akifanya fujo atatwanga talaka mambo yataisha.


Kutwangwa talaka wala haogopi kamwe! Mwanaume naye hofu anayo kwa vile atakosa mengi anayoyapata kwa huyo mkewe ikiwa ni pamoja na nyumba waliyojenga tena ya kifahari.Mdada wala haogopi hiyo talaka kwani itamsaidia sana kutafuta makubwa zaidi.
 
Back
Top Bottom