Relief Mirzska
JF-Expert Member
- Jun 13, 2017
- 13,992
- 22,396
Tena hoja nyepesi mno mkuu.HesabuKali
Huyu atakuwa ni mvulana ambaye bado anashikiwa akili na kulishwa maneno na mama yake kuchukia uke-wenza, tumkumbushe kitu kimoja, kwenye maisha ya ndoa, au hata maisha ya kawaida, migogoro ipo hata ukiwa pekee yako (migogoro binafsi) na hata ukiwa na mke mmoja.
Hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya migogoro hiyo na wake wengi, nimezaliwa na kukulia katika familia ya aina hiyo, nazongwa tu na mafundisho ya kidunia (dini) ila nafsi inanisuta nikioa mke mmoja.
Labda kwa sababu ya maradhi ambukizi, naweza kuhofia ndoa hizi, ila kamwe sio kwa hoja nyepesi za Financial Analyst.
Yaani mimi nikipata safari ya kikazi kwa wiki tu kuja hapo jijini Dar imekuwa tabu sana maana wengine haiwezekani kukaa siku tatu bila bila, kipindi chote hicho cha wiki moja naishije???
cc: Mishil