SoC01 Changia damu, okoa maisha"Ukweli kuhusu zoezi la uchangiaji damu"

SoC01 Changia damu, okoa maisha"Ukweli kuhusu zoezi la uchangiaji damu"

Stories of Change - 2021 Competition

abelauthor

New Member
Joined
Jul 19, 2021
Posts
4
Reaction score
4
UTANGULIZI
"Changia Damu,Okoa Maisha"hii ni kauli mbiu ya mpango wa taifa wa damu salama inayotumika kuhamasisha uchangiaji wa damu ili kuokoa maisha.

Watu wengi,watoto kwa watu wazima wanahitaji damu kila panapoitwa leo kutokana na ajali,maradhi,baada ya kujifungua n.k
Moja ya taarifa Iliyochapishwa kwenye tovuti ya mpango wa damu salama Tanzania (www.nbts.go.tz)inaonyesha kuwa kuna makundi makubwa manne ya wahitaji,
(a)Watoto chini ya umri wa miaka 5, wanatumia zaidi ya asilimia 50 ya damu inayokusanywa.
(b)Wajawazito na wanawake wenye matatizo ya uzazi,wanatumia zaidi ya asilimia 30 ya damu inayokusanywa.

(c)Waathirika wa ajali wanatumia zaidi ya asilimia 15 ya damu inayokusanywa
(d)Watu wenye maradhi mengine kama kansa wanatumia zaidi ya asilimia 5 ya damu inayokusanywa.
Licha ya uhitaji huo mkubwa ukusanyaji wa damu bado upo chini licha ya jitihada kubwa zinazofanywa na Mpango wa damu salama.

Taarifa kutoka kwenye tovuti ya mpango wa damu salama Taifa(www.nbts.go.tz)zinaonyesha kuwa hukusanywa asilimia 30 tu ya mahitaji ya damu kwa mwaka ambayo ni zaidi ya chupa 400,000 ,Kwa lugha nyepesi tunaweza kusema mpango wa damu salama kitaifa hukusanya chupa 120,000 tu kwa mwaka badala ya chupa 400,000 zinazohitajika.

Baada ya kuona taarifa hizo kama mdau wa sekta ya afya niliamua kufanya tafiti ili kujua sababu ya kuwa na makusanyo madogo ya damu chini ya kiwango kinachohitajika na nikagundua moja ya sababu kubwa inayopelekea jambo hilo ni Uelewa mdogo na dhana potofu kwa jamii juu ya zoezi la uchangiaji Damu.
Jamii inataarifa nyingi zisizo sahihi/Kweli.

Andiko hili limejibu baadhi ya maswali ambayo yanawatatiza wanajamii wengi na kuwafanya wahofie kuchangia damu na ni matumaini yangu kila atakayesoma andiko hili atajifunza mengi na kuwa mchangiaji hodari wa damu,Karibu ujifunze hapa chini:

UKWELI KUHUSU ZOEZI LA UCHANGIAJI DAMU

1.Damu haiuzwi.
Unapochangia damu unaokoa maisha ya mtu anayehitaji.
Unapochangia damu atapewa mtu anayehitaji.
Hairuhusiwi kuuza wala kununua damu na ukiombwa kufanya hivyo toa taarifa kwa mamlaka inayohusika ikiwemo Takukuru kwa kupiga simu namba 113.

2.Kabla mtu mwingine hajaongezewa damu uliyochangia,Damu hiyo huchunguzwa magonjwa mbalimbali ikiwemo virusi vya ukimwi,kaswende,homa ya ini B na C.Hivyo damu anayoongezewa mhitaji ni Damu salama.

3.Damu ya binadamu haiwezi kuzalishwa nje ya mwili wa binadamu,hivyo mgonjwa akihitaji damu lazima aongezewe damu ambayo imetoka kwenye mwili wa binadamu.

4.Zoezi la Uchangiaji Damu ni salama hivyo hauwezi kupata maambukizi ya ukimwi wala magonjwa mengine wakati wa zoezi.

Zoezi hili huendeshwa na wataalamu wenye ujuzi na vifaa vinavyotumika ni salama.
5.Sio kweli ukichangia damu,Utaishiwa damu mwilini.

KWA SABABU:
(a)Kabla ya kuchangia damu ni lazima upimwe wingi wako wa damu ili kujua kama kiwango cha damu ulichonacho kinatosha kumuongezea mtu mwingine au la.
(b)Mtu mwenye afya njema ana wastani wa lita 6-7 za Damu na anaweza kuchangia mara kwa mara(Kila baada ya miezi 4 kwa wanawake na miezi 3 kwa wanaume),Chupa moja ya damu inaujazo usiozidi mililita 450.
6.Hakuna madhara yoyote unayoweza kupata kwa kuchangia damu.

Kuna watu ambao wameweza kuchangia damu zaidi ya mara 50,60,70, na wengine mpaka mara 100 katika maisha yao.
7.Watu wengi huhofia maumivu ya sindano,Ni kweli yapo lakini husikika kwa kiwango kidogo wakati wa kuingiza na kutoa sindano.

HITIMISHO
Dunia inamtambua mtu mmoja anaitwa James Harrison,Raia wa taifa la Australia kama mchangia damu mfano wa kuigwa,kupitia rekodi za Guinnes World Records tarehe 19 May mwaka 2003.

James Harrison amechangia damu zaidi ya chupa 1,173 zilizookoa maisha ya watoto zaidi ya milioni mbili na nusu.
Chupa yake ya mwisho aliichangia tarehe 11 May mwaka 2018 akiwa na umri wa miaka 81.
Alipata maradhi makubwa akiwa mtoto mdogo yaliyopelekea aongezewe damu zaidi ya lita 10, na toka hapo alijiapiza ni lazima aokoe maisha ya wengine kupitia kuchangia damu kama yeye alivyookoka.

Maisha ya James Harrison aliyeokoka maisha yake kwa kuongezewa damu za watu asiowajua na yeye kuokoa maisha ya watoto milioni mbili na nusu asiowajua kwa damu yake yanatufundisha kitu kikubwa sana.
Jambo la kujiuliza wakati wa kuhitimisha andiko hili ni:Je,Mimi na wewe,tunayagusa vipi maisha ya wengine??

Nakuacha tu utafakari huku nikikukumbusha"Hukuzaliwa bila chochote, Usikubali kufa bila kufanya chochote"
CHANGIA DAMU, OKOA MAISHA
 
Upvote 5
Inapendeza sana, ila huko tunapelekea na hizi chanjo za Uviko kutakua hakuna tena kuchangia damu...

Maana damu itakua haifai...
 
Mpaka Sasa hakuna facts zozote za kisayansi zinazoonyesha mtu aliyepewa Chanjo,yoyote ikiwemo hiyo unayoisema anazuiwa kutoa damu kwa ajili ya mwingine kuongezewa,
 
Back
Top Bottom