Jasusi Mbobezi
Senior Member
- May 17, 2020
- 195
- 851
Siku moja nilimsikia mheshimiwa sana waziri wangu wa Afya akisema watu wanajitokeza kwa wingi kudungwa kuliko walivyo tarajia, siku nyingine nikamsikia mheshimiwa sana Rais Samia Suluhu akisema kuwa kinacho muumiza kichwa kwasasa ni wapi watapata chanjo zaidi, maana kwa jinsi hizi za awali zilivyo changamkiwa ni wazi kuwa hazitoshi.
Swali langu ni jepesi tu, endapo watu wanajitokeza kwa kasi hiii, mbona haziishi? Yaani pamoja na kuziandalia siku maalumu pale uwanja wa taifa, pamoja na timu zetu kuhamasisha mashabiki wake, pamoja na vyombo vya habari kuzipa promo, pamoja na viongozi wa Bunge kuhamasisha, pamoja na wasanii kuzitungia nyimbo lakini hazijaisha mpaka leo.
Nini tatizo? Waziri wa Afya na naibu wako mnakwama wapi?