#COVID19 Chanjo ya Corona iwe lazima kwa baadhi ya makundi yanayotoa huduma za kijamii

#COVID19 Chanjo ya Corona iwe lazima kwa baadhi ya makundi yanayotoa huduma za kijamii

Utakufa mwenyewe kenge ww.

Usitishe watu kwa kifo ,as if Hakuna aisyejua kufa.Isitoshe hukumpangia yeye azaliwe, halikadharika humpangii yy afe lini.
Bado tu upo hai? Subiri, haitachukua muda mrefu. Uwe mvumilivu, Corona inakujia kwa kasi!
 
Mbona unaongea Hadi mishipa ya shingo inakusimama.TUNAJUA UMELIPWA KWA KAZI HIYO NA WENYE COVID.

Sasa km umechanjwa, si umejikinga na covid tayari.

Asiyechanjwa si akiambukizwa atakufa?na wewe KWA kuwa una chanjo kirusi hakitakudhuru Sana.

Shida iko wapi sasa?ww unayeogopa kuambukizwa ndo ujifungie huko ndani mwako, na ambao hawajachanjwa wao waendelee kuambukizana huko mtaani na kupukutika km unavyopotosha hapa.
Na wewe si muda tutasema ulikuwa mtu mzuri lakini mbishi. Corona inakujia kwa kasi!
 
Hicho kidawa wanachowachoma sijui ni kirusi ni hatari sana maana kila aliyechoma amekua na kauli za ajabuajabu na anatamani kila mtu achanjwe kama yeye huku wanasema ni hiari, sasa najiuliza hiari hii mbona kama hiarilazima hivi?
 
Chanjo ya Korona inaweza kuwa hiari, lakini usiseme hutaki chanjo halafu uendelee kuwa konda wa basi au nesi hospitali, tafuta kazi nyingine.

Katika hali ya haki za binadamu, kila mtu ana uhuru wa kufanya analotaka ili mradi asivunje sheria au kuingilia au kuathiri haki za watu wengine katika kuwa kwao huru na kutofanyiwa bugudha za kimaisha.

Sasa wapo wanaotaka kwamba suala la chanjo za Korona liwe la utashi wa mtu, watu kama kina Aunt Fatma Karume. Na wapo wanaotaka chanjo za Korona liwe lazima, watu kama kina Mbowe. Wote hawa wapo sawa, lakini kuwa kwao sawa kuna mipaka.

Nikianza na kina Fatma Karume, ni sawa watu kuwa huru kuamua kuchanja au kutochanja dhidi ya Korona. Lakini sasa, wewe unapoamua hutaki kuchanja basi msimamo wako usiathiri au kuhatarisha maisha ya wengine.

Kama utakataa kuchanja na ukaamua kujifungia nyumbani kwako hilo ni hiari yako. Lakini usikatae kuchanja halafu uje unipumulie virusi vya korona sugu mimi ambaye nimekubali kuchanja, au hata watoto ambao wako chini ya umri wa kuchanja, au watu ambao wameambiwa wasichanje kwa sasa kwa sababu mbalimbali kama ujauzito.

Na kwa kina Mbowe, kinyume cha hili la kina Fatma kinatumika kwako. Ikiwa sitaki kuchanja na hata niko tayari kuacha kazi yangu ambayo inaweza kuhatarisha maisha ya wengine kwa sababu sijachanja, basi usiniingilie, niache nijifungie nyumbani kwangu, kwa kuwa sina haja ya kujichanganya na watu wengine.

Tukielewana katika haya basi tutakuwa sawa.
Mabaa medi wachome sindano:
 
Back
Top Bottom