#COVID19 Chanjo ya Corona iwe lazima kwa baadhi ya makundi yanayotoa huduma za kijamii

#COVID19 Chanjo ya Corona iwe lazima kwa baadhi ya makundi yanayotoa huduma za kijamii

Jamani wilaya niliopo sijashudia kisa chochote cha Covid 19, sio wimbi la kwanza, lapili wala hili la tatu, kwahiyo huwa na jiuliza hiyo Corona inatuogopa watu wa maeneo haya niliyopo?
Ni wapi huko?
 
Na kuna watu wanalipwa kusema chanjo zinaua na kutengeneza video hadi kuonyesha ukichanja ukibandika balbu mwilini itawaka.

Haiwezekani mimi na familia yangu tukubali kudungwa chanjo halafu anatokea kenge analazimisha kutupumulia usoni na virusi vyake sugu vya korona kisa yeye na familia yake wamekataa kuchanja
Kaa karantini wewe na familia yako. Kwani lazima uchangamane na wasiochanjwa.? Kama ni mwajiriwa chukua likizo ama uache kazi (kama ulivoshauri wasiochanjwa waache kazi) ili ujilinde dhidi yao
 
Inasikitisha sana kuona watu wanavyobisha kwa furaha na kicheko bila kuelewa lolote kuhusu Covid-19.

Tatizo ni kwamba Covid-19 wana mutate kupitia watu ambao hawajachanjwa, kiasi kwamba inafikia wakati msiochanjwa mnawapa uwanja wa Covid-19 ku-mutate hadi wanafikia kuwaambukiza tena wale waliochanjwa kwa kuwa chanjo yao ilikuwa ni kwa Covid-19 ambaye alikuwa haja-mutate.

Kwa hiyo dawa ni watu wote kuchanja ili kutowapa Covid-19 hosts watakaowatumia ku-mutate. Ndio maana mnasikia juu ya South Africa variant, UK variant etc.

Tulipoanza na Covid-19, hatukuwa na Delta variant ya Covid-19. Delta ni Covid-19 ambaye ame-mutate kupitia wajinga ambao hawataki kuchanja. Kama dunia nzima tunhechanja kwa wakati mmoja, tusingekuwa na Covid-19 Delta. Na kadiri watu wanavochelewa ndivyo tutazidi kuwa na mutations zaidi za Covid-19, na kufikia ambapo chanjo zitakuwa hazisaidii tena.

Siku wakifa mama, baba, watoto, dada, kaka zenu, ndio mtajua uchungu wa Covid-19. Kwa sasa chekeni sana.

Kwa nini mnakuwa wabishi bila kusumbua akili zetu kuelewa mambo kwanza?
Chukulia assumption watu wote duniani ama Tanzania kwa mfano mdogo wangekubali kuchanja unajua serikali haina uwezo wa kuwafikia wote ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, sasa ungeweza tumia utaratibu gani kuwabagua watu hawa kiajira walio tayari kuchanja ila uwezo mdogo wa serikali kuwafikia umesababisha wao kutochanjwa? Ungewalipa mishahara ya bure ili wakae nyumbani hadi watakapopata chanjo? Ungewapelekea mahitaji yao ya kutosha milangoni mwao kwa sababu hutaki wachangamane sehemu za public wasije kusambaza virus?
 
Kaa karantini wewe na familia yako. Kwani lazima uchangamane na wasiochanjwa.? Kama ni mwajiriwa chukua likizo ama uache kazi (kama ulivoshauri wasiochanjwa waache kazi) ili ujilinde dhidi yao
Yaani niache kazi kwa ubishi wa kujinga kama wako wa kukataa chanjo? Hamna kitu kama hicho kutokea. Tutakupata tu na kukuchanja, la sivyo jifungie chumbani na mkeo tusikuone hadharani.
 
Moderators

Mie niliandika kichwa cha thread chenye kuvutia watu kusoma, Moderators mkabadilisha kuwa " Chanjo ya Corona iwe lazima kwa watoa huduma za kijamii".

Sasa Moderators sijui mnataka kutuambia nini. Hivi hamjui kuwa mtu anaweza akawa anatoa huduma za kijamii akiwa amejifungia nyumbani kwake? Sio huduma zote za kijamii lazima zikukutanishe na watu, ndio maana nikaweka mfano wa konda wa basi na nesi kwenye kichwa cha thread ili mtu akisoma aelewe kirahisi. Kwa mfano, Moderators mnafanya kazi za huduma za kijamii kwa kuwa JF ni social forum, lakini hakuna ulazima wa nyie kuchanjwa Corona kwa sababu kazi mnayofanya, pamoja na kuwa ni huduma za kijamii, mnaweza kufanyia nyumbani. Vivyo hivyo watangazaji redio nk.

Injinia wa mitambo ya kusambaza maji, dereva wa gari ya takataka, fundi umeme wa Tanesco, zote hizo ni huduma za kijamii - lakini hazihitaji ulazima wa kuchanjwa. Kwa hiyo Moderators mmeondoa kichwa changu kilichoeleweka vizuri mkaweka chenu kinachopotosha.

Nilisha waambia huko nyuma, msi-moderate kwa kujifanya mnajua zaidi kuliko sisi wengine, kwa kuwa mara nyingine mnaharibu badala ya kurekebisha.

Wewe ni nani kuwapangia Moderators cha kuedit katika heading?

Wewe ni nani kuwataka watu wachanjwe?

Wewe ni nani kuwataja baadhi ya watanzania waache kufanya kazi zao kiss hawajachanjwa?
 
Kwani ukichanjwa halafu ukapata maambukizi unakuwa hauambukizi wengine?
 
Back
Top Bottom