Mkuu, katika vitu kama hivi, ambavyo vinaingia kwenye mambo tunayoita public administration, kuna kitu kinaitwa cost of enforcement of directives.
Fikiria, ikiwa tutasema kama konda hajafanyiwa chanjo basi mtu asipande basi lake, kutia ndani daladala nk, utawezaje kuhakikisha hilo linatendeka? - How do you enforce that? Kwa hiyo ni rahisi ku-enforce makonda wachanje kuliko kuratibu watu wasipande basi au daladala lenye konda hajachanjwa.
Suala la matabibu kuchanjwa kwa mfano, ni kwamba hadi unapoenda hospitali, tayari una weakness katika immunity yako. Na watu wenye weakness katika immunity sio tu ni rahisi kuambukizwa Covid-19, bali pia ni rahisi wao kufa wanapoambukizwa. Mtu mwenye weak immunity kutokana na tatizo fulani la kiafya, akiambukizwa Covid-19 huwa mara nyingine atakufa baada ya siku mbili tu. Sasa nesi mmoja tu aliye na Covid-19 ambaye haonyeshi dalili za ugonjwa (asymptomatic) anaweza kuambukiza wodi zima la wagonjwa ambao wamelazwa kwa tatizo nje kabisa ya Covid-19. Ndio maana ni rahisi kudhibiti hilo kwa kumchanja huyu nesi. Au fikiria dokta anapiga round hospitali yote, kumbe ana Covid-19. Kuna siku utasikia waginjwa wote wa hospitali ya Mwananyamala wameambukizwa Covid-19.
Wewe utajisikiaje pale baba yako amelazwa hospitali kwa tatizo la BP, halafu unaambiwa amepata Covid-19 kutoka kwa nesi na sasa hali yake ni mbaya? Kumbuka ukiwa na kitu kama kisukari , ukipata Covid-19 uwezekano wa kufa ni zaidi ya 80%. Sasa utalindaje watu kama hawa wakiwa hospitali, kwa kumwambia nesi ana hiari ya kuchanja au kutochanja?
Natumaini somo limeeleweka.