#COVID19 Chanjo ya Corona iwe lazima kwa baadhi ya makundi yanayotoa huduma za kijamii

#COVID19 Chanjo ya Corona iwe lazima kwa baadhi ya makundi yanayotoa huduma za kijamii

Kumbe udikteta tunaupenda!
I say watu mna mawazo mafupi sana. Hebu niambie, Raisi akisema kuna ugonjwa wa kipindupindu umezuka marufuku mtu yeyote kutengeneza pombe za kienyezi na kuziuza vilabuni, kwako wewe huo ni udikteta?
 
Huyu jamaa aliyeanzisha huu uzi kama siyo mchawi basi ni freemason. Utalazimishaje mtu kufanya unachoamini wewe?. Wasilikizie waliochanja!
Nitawasikilizaje wakati watu wote waliochanja wameshakufa? Si ndio umeambiwa hivyo?
 
I say watu mna mawazo mafupi sana. Hebu niambie, Raisi akisema kuna ugonjwa wa kipindupindu umezuka marufuku mtu yeyote kutengeneza pombe za kienyezi na kuziuza vilabuni, kwako wewe huo ni udikteta?
kwa hiyo kufanya invasive procedures kwenye mwili wa binadamu unafananisha na quarantine? Hivi itoke decree leo kua mashoga wote wafanyiwe chemical castration ,utaunga mkono?
 
kwa hiyo kufanya invasive procedures kwenye mwili wa binadamu unafananisha na quarantine? Hivi itoke decree leo kua mashoga wote wafanyiwe chemical castration ,utaunga mkono?
Kwa hiyo unalinganisha kuchanjwa Corona na chemical castration?

Kama chanjo ya Corona ni chemical castration, nikisha chanja nipe my wife wako anikalie sawa, maana hutakuwa na la kuogopa

Halafu acha kutumia maneno makubwa bila kuyaelewa, hata kuchoma sindano ya malaria ni invasive procedure
 
Ndio tulichanjwa. Lakini chanjo unayopigia debe ni tofauti sana. Hivi hujiulizi juu hii chanjo ambayo hata waliowahi pokea Nobel Prize za sayansi wanatuhadharisha sisi hinadamu dhidi yake?.

Ugonjwa wa kuambukiza dunia yote kwa mpigo haijawahi tokea. Sisi na Mungu Mungu wetu atatuvusha salama. Endelea na kampeni zako una faida unaipata.
Sawa, acha mungu wenu awavushe salama kama alivyomvusha raisi wetu Magufuli. Anza kuimba kabisa mtakutana na Magufuli mtoni.
 
Wakuuwe kwa nini? Hivi kwa nini watu mafukara huwa wanaishi kwa wasiwasi kuwa watu wengine wanawaonea wivu? Hata ukienda kwa waganga wa kienyeji wengi wa wateja ni mafukara wanaodhani wamelogwa ili wasipate maendeleo.
Hahahaha! Mkuu umetisha. Waswahili bwana wako tayari kumwamini mganga wa kienyeji kunyweshwa mavi ya kuku yamechanganywa na mkojo wa mbuzi ili wapate utajiri kuliko kupewa chanjo ya Corona ili wasije wakafa!

Hivi watu wanajua Babu wa Loliondo aliwanyweshwa nini?😂😂😂😂
 
Sawa, ndio maana wakaleta Corona inayowaua na wao wenyewe ili kutukomoa Waafrika na watuuzie chanjo za Corona.

Hivi huko vichwani wengine mmejaza nini hasa?
Watu wa aina hii unapoteza muda tu kulumbana nao. Ni uwezo wao wa kupambanua mambo ndiyo tatizo. Haya mambo hayahitaji akili kubwa sana lakini inasikitisha kuna watu hawaelewi. Mtu vitu anavyotumia katika maisha yake karibu asilimia 80 vimetengenezwa na wazungu halafu anachagua kimoja anasema wanataka kutuua na hiki. Hivi wanajua kuwa kama wazungu wakiamua kutuua tufe kama inzi watapoteza nguvu ku-create njia complicated namna hiyo? Hizi simu tunazotumia wakiweka mawimbi yenye madhara kuna ''kima'' atagundua?
 
Chanjo ya Korona inaweza kuwa hiari, lakini usiseme hutaki chanjo halafu uendelee kuwa konda wa basi au nesi hospitali, tafuta kazi nyingine.
Sawa. Lakini, yule aliyepata chanjo kwa nini asijitenge na ambao hawajachanjwa. Ukiona konda hajachanjwa usipande gari lake. Konda akikosa abiria ataitafuta chanjo mwenyewe.

Na yule mgonjwa ambaye anaona daktari hajachajwa, basi mgonjwa huyo atafute chanjo mwenyewe ili awe huru kwenda kwa daktari ambaye hajachanjwa ama amtafute daktari aliyechanjwa. Pia katika hili Daktari mwenyewe akiona wagonjwa wanapungua kwake, na ile fomu ya kupima utendaji wake (OPRAS) ikionekana hayuko "effective" atapangiwa kazi nyingine. Rahisi tu.

Shida iko wapi katika hili, kwani ? Kwa nini mnataka makonda walazimishwe kuchanjwa? Kwa nini mnalazimisha matabibu kuchanjwa? Wakati huo huo hamtaki kushikwa makosa endapo chanjo hizo zitawaletea madhara hao makonda na matabibu? Mjifunge kisheria kuwa endapo konda ama daktari atapata madhara kutokana na madhara ya chanjo kiasi cha kutoweza kuendelea na kazi yake basi, mtakuwa tayari (ninyi ambao mnataka chanjo iwe lazima kwao) kuitunza familia nzima ya konda ama tabibu kwa zaidi ya miaka hamsini. Ni wajibu mdogo sana huu kuutekeleza ninyi mulio mstari wa mbele kuhusu ulazima wa chanjo. Rahisi tu namna hiyo, Mkuu.

Haya sasa shusha nondo zako, tukuelewe Mkuu.
Karibu.
 
Mkuu me nahisi kuna watu wanalipwa kwa kazi ya kuhamasisha huu upuuzi walio uita chanjo.
Haiwezekani me na familia yangu tukatae kudungwa chanjo, alafu anatokea kenge analazimisha tuchanjwe kisa yeye na familia yake wamechanjwa.
Wanatoboa mtumbwi...!!!
 
Hivi wazungu wametushindwa kutuua kwenye ARV NA MA CHANJO kibao waje kutuua kwenye chanjo ya CORONA
 
Sawa. Lakini, yule aliyepata chanjo kwa nini asijitenge na ambao hawajachanjwa. Ukiona konda hajachanjwa usipande gari lake. Konda akikosa abiria ataitafuta chanjo mwenyewe.

Na yule mgonjwa ambaye anaona daktari hajachajwa, basi mgonjwa huyo atafute chanjo mwenyewe ili awe huru kwenda kwa daktari ambaye hajachanjwa ama amtafute daktari aliyechanjwa. Pia katika hili Daktari mwenyewe akiona wagonjwa wanapungua kwake, na ile fomu ya kupima utendaji wake (OPRAS) ikionekana hayuko "effective" atapangiwa kazi nyingine. Rahisi tu.

Shida iko wapi katika hili, kwani ? Kwa nini mnataka makonda walazimishwe kuchanjwa? Kwa nini mnalazimisha matabibu kuchanjwa? Wakati huo huo hamtaki kushikwa makosa endapo chanjo hizo zitawaletea madhara hao makonda na matabibu? Mjifunge kisheria kuwa endapo konda ama daktari atapata madhara kutokana na madhara ya chanjo kiasi cha kutoweza kuendelea na kazi yake basi, mtakuwa tayari (ninyi ambao mnataka chanjo iwe lazima kwao) kuitunza familia nzima ya konda ama tabibu kwa zaidi ya miaka hamsini. Ni wajibu mdogo sana huu kuutekeleza ninyi mulio mstari wa mbele kuhusu ulazima wa chanjo. Rahisi tu namna hiyo, Mkuu.

Haya sasa shusha nondo zako, tukuelewe Mkuu.
Karibu.
Mkuu, katika vitu kama hivi, ambavyo vinaingia kwenye mambo tunayoita public administration, kuna kitu kinaitwa cost of enforcement of directives.

Fikiria, ikiwa tutasema kama konda hajafanyiwa chanjo basi mtu asipande basi lake, kutia ndani daladala nk, utawezaje kuhakikisha hilo linatendeka? - How do you enforce that? Kwa hiyo ni rahisi ku-enforce makonda wachanje kuliko kuratibu watu wasipande basi au daladala lenye konda hajachanjwa.

Suala la matabibu kuchanjwa kwa mfano, ni kwamba hadi unapoenda hospitali, tayari una weakness katika immunity yako. Na watu wenye weakness katika immunity sio tu ni rahisi kuambukizwa Covid-19, bali pia ni rahisi wao kufa wanapoambukizwa. Mtu mwenye weak immunity kutokana na tatizo fulani la kiafya, akiambukizwa Covid-19 huwa mara nyingine atakufa baada ya siku mbili tu. Sasa nesi mmoja tu aliye na Covid-19 ambaye haonyeshi dalili za ugonjwa (asymptomatic) anaweza kuambukiza wodi zima la wagonjwa ambao wamelazwa kwa tatizo nje kabisa ya Covid-19. Ndio maana ni rahisi kudhibiti hilo kwa kumchanja huyu nesi. Au fikiria dokta anapiga round hospitali yote, kumbe ana Covid-19. Kuna siku utasikia wagonjwa wote wa hospitali ya Mwananyamala wameambukizwa Covid-19.

Wewe utajisikiaje pale baba yako amelazwa hospitali kwa tatizo la BP, halafu unaambiwa amepata Covid-19 kutoka kwa nesi na sasa hali yake ni mbaya? Kumbuka ukiwa na kitu kama kisukari , ukipata Covid-19 uwezekano wa kufa ni zaidi ya 80%. Sasa utalindaje watu kama hawa wakiwa hospitali, kwa kumwambia nesi au dokta ana hiari ya kuchanja au kutochanja?

Natumaini somo limeeleweka.
 
....watu ambao wanavi-host. Sasa kadiri ambavyo watu hao wanaendelea kuwapo, na virusi vinaendelea kuwatumia kujibadilisha, hata nyie mliochanja itafikia mahali vile virusi wanavyosambaza vimebadilika na chanjo mliyofanya haiwazuii tena.
Hao watu ni mazimwi? Kiasi wana weza kukabili mziki wa covid SA, covidUK, covidIndia, covidDelta, sijui kovid alfa...bila kutingishika!? Vipi kuhusu malarai, si kuna tiba, mbona bado hali tete...! Vipi kuhusu mafua, na ule ugonjwa wa upungufu wa kinga za mwili, si bado hali ni tete...ni 'cha umaalumu' kuhusu kovid hapa nchini ambao hatukuweka lock down na walioweka lockdown na kuchanjwa? umaalumu upo ukivua miwani ya upendeleo kutokana mambo yasiyowekwa wazi.

Tuchukue hatua. Tufuate masharti ya wataalamu wetu toka wimbi hili lilipotufika hapa nchini. Kila aina ya zana itumike kadri nafsi inavotaka hili mradi hauhatarishi maisha ya mwezako. Tuondoe hofu baina yetu, tuache tabia ya kuwatenga wagonjwa wa korona, bali tuchukue tahadhari zote kuwatunza wawapo kwenye matibabu. Stigmatization inaua, kwa sababu inasababisha msongo wa mawazo!
 
Chanjo ya Korona inaweza kuwa hiari, lakini usiseme hutaki chanjo halafu uendelee kuwa konda wa basi au nesi hospitali, tafuta kazi nyingine.

Katika hali ya haki za binadamu, kila mtu ana uhuru wa kufanya analotaka ili mradi asivunje sheria au kuingilia au kuathiri haki za watu wengine katika kuwa kwao huru na kutofanyiwa bugudha za kimaisha.

Sasa wapo wanaotaka kwamba suala la chanjo za Korona liwe la utashi wa mtu, watu kama kina Aunt Fatuma Karume. Na wapo wanaotaka chanjo za Korona liwe lazima, watu kama kina Mbowe. Wote hawa wapo sawa, lakini kuwa kwao sawa kuna mipaka.

Nikianza na kina Fatma Karume, ni sawa watu kuwa huru kuamua kuchanja au kutochanja dhidi ya Korona. Lakini sasa, wewe unapoamua hutaki kuchanja basi msimamo wako usiathiri au kuhatarisha maisha ya wengine.

Kama utakataa kuchanja na ukaamua kujifungia nyumbani kwako hilo ni hiari yako. Lakini usikatae kuchanja halafu uje unipumulie virusi vya korona sugu mimi ambaye nimekubali kuchanja, au hata watoto ambao wako chini ya umri wa kuchanja, au watu ambao wameambiwa wasichanje kwa sasa kwa sababu mbalimbali kama ujauzito.

Na kwa kina Mbowe, kinyume cha hili la kina Fatma kinatumika kwako. Ikiwa sitaki kuchanja na hata niko tayari kuacha kazi yangu ambayo inaweza kuhatarisha maisha ya wengine kwa sababu sijachanja, basi usiniingilie, niache nijifungie nyumbani kwangu, kwa kuwa sina haja ya kujichanganya na watu wengine.

Tukielewana katika haya basi tutakuwa sawa.
Kila mtu afanye maamuzi kwa faida zake mwenyewe. Kama Ni huduma za kijamii kila mtanzania anawajibika kuzitoa directly au indirectly.
Watu mnachanja halafu bado mnaogopa kuambukizwa, Basi hiyo si chanjo.
Eti mi nisiwe nimechanjwa halafu mtu akanipumulia virusi, Kwani Kama umechanjwa na chanjo inafanyakazi kweli virusi vitakufanya Nini.
Kila mtu alindwe au aangamie kwa kill anachokiamini. Kama unaamini chanjo itakulinda Basi uwe tayari kwa matokeo yake, na Kama huamini kulindwa na chanjo Basi ulindwe na kile unachokiamini.
 
Soma hapo juu utapata jibu la issue yako unayoeleza hapa. Labda kwa kukusaidia;

Tatizo ni kwamba, watu wasiochanjwa wanasababisha virusi kuendelea kusambaa na kubadilika (mutate), kwa kuwa kunakuwa na watu ambao wanavi-host. Sasa kadiri ambavyo watu hao wanaendelea kuwapo, na virusi vinaendelea kuwatumia kujibadilisha, hata nyie mliochanja itafikia mahali vile virusi wanavyosambaza vimebadilika na chanjo mliyofanya haiwazuii tena.

Kwa hiyo naweza nikawa nilichanja kabla ya kuwapo kwa Covid-19 Delta variant, ambayo imebadilika kutokana na kuwapo na kupitia kwa watu ambao hawakuchanja mie nilipochanja, matokeo inaweza kuwa mtu mwenye Covid-19 Delta anaweza kuniambukiza japo nilichanja, kwa kuwa chanjo yangu hainikingi dhidi ya hii variant ya Covid-19 ambayo imejigeuza (mutate) na kusambazwa kupitia kwa watu ambao walikataa kuchanja.

Ideally, ikiwa leo variant iliyopo ni Covid-19 Delta, ni vema watu wote wapate chanjo ili sasa kusiwe na watu ambao wataisambaza na kuipa nafasi ya kujibadilisha tena

Na kuna watu kama watoto chini ya miaka 12 na wajawazito, wenye BP kali nk, hawaruhusiwi kuchanja. Kwa hiyo kuchanja ni kulilinda hili kundi pia.
 
Si katika kila jambo tunapaswa kuishi kwa imani. Mengine yanahitaji ukweli wa kisayansi.
Hatuna imani na wanasayansi katika corona, wao wenyewe wamechemsha, Kama sivyo ama corona ingekuwa imepotezwa, au ingebaki tu kwa nchi zenye uwezo na weledi mdogo wa kisayansi na kitechnolojia.
 
Utaki chanjo nenda Burundi, unataka kubaki tanzania lazima uchanje pumbafu msiwe wabishi kila kitu.
 
KY unayojivunia katika kulainisha njia yako inatengenezwa na hao hao watengeneza chanjo
Narudia Tena, 'hatuna imani na wanasayansi katika maswala ya corona' . Umeelewa mkuu?
Wao wenyewe wanakufa na corona Kama Nini..
Binafsi siwezi kumuamini mtu aliefeli, hata mwalimu anaenifundisha , nikigundua kwamba alifeli, ndo Basi Tena siwezi kumuamini..
 
Hatuna imani na wanasayansi katika corona, wao wenyewe wamechemsha, Kama sivyo ama corona ingekuwa imepotezwa, au ingebaki tu kwa nchi zenye uwezo na weledi mdogo wa kisayansi na kitechnolojia.
Sasa mambo ya imani katika mambo ya kisayansi bwana, subiri kina Charles Darwin wakifufuka ukaongee nao. Maana mie siamini huko nyuma tulikuiwa sokwe, na kama unaamini tulikuwa sokwe nikisema sokwe wewe au ukoo wenu mnafanana na sokwe usikasirike.
 
Back
Top Bottom