Tetesi: Chanjo za Corona zimetua nchini rasmi

Tetesi: Chanjo za Corona zimetua nchini rasmi

Huko tuendako chanjo haikwepeki kama shughuli zako ni za kwenda mabara mengine mara kwa mara. Kama sisi hatuumwi na ndugu zetu hawafi kwa idadi kubwa tujue tu huko nje bado hali ni mbaya.

Huwezi kuipinga chanjo mbele ya wananchi wa Brazil, huwezi kuiponda chanjo mbele ya wananchi wa India, watakuchapa makofi.
 
Hakuna sehemu niliyosema alikuwa na shida na mabeberu,ila nimekuelewa,vipi lile swala la mkataba wa kuuza vitu na kununua toka huko kwa mabeberu ambalo Kenya walilishikia bango ila Mkapa mpaka akaandika makala,tunaendelea nalo kuwasapoti Kenya
 
Ukweli ni kwamba chanjo zilishingia inchini way before hili tangazo...balozi nyingi tu zilishaanza kuwapa chanjo wafanyakazi wao...hii barua ni validation tu ya ambacho kimeshatokea kimya kimya...
Wanaofanya kazi kwenye balozi wanalijua hili.
 
Vipi, mbona zimeingizwa kinyemela sana?

Wamesubiri wakati ambapo sakata la sabaya limekolea na wao wakachomekeamo na chanjo humo humo!

Kama chanjo ni kitu chema, mbona wanakificha ndani ya habari za akina sabaya? ili watu wasitilie maanani ama?

Mimi nilifikiri ujio wa chanjo ulipaswa kuwekwa wazi ili kila mtu atambue kwamba Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN ameridhia kuchanja watu wake!

Hii ingewapa watu ari ya kudungwa hizo chanjo kutoka ulaya ili tudhibiti gonjwa hatari la corona.

Kwanini wameamua kuziingiza chanjo kupitia vichochoroni tena wakati ambapo umma wa watanzania umejikita na drama za sabaya?

Hakuna japo kavideo cha Rais kutoa tamko na kuhimiza watanzania wadungwe chanjo?View attachment 1808167
Magufuli alimtuma kabudi sense Madagascar, akafika akanywa mataputapu Yale, mengine akampelekea magufuli kule rubondo mafichoni
Ingawa ilionyeswhwa kwenye tv bado corona ilimtafuna pakubwa
 
Hata Matibabu ni hiyari

Kulazimisha watu kuchanja Chanjo ya Corona si sahihi kama ilivyokuwa kulazimisha watu wasijichanje pia sio sahihi

Weka ukiona sahihi kuchanja , basi chanjwa, ukiona sio sahihi acha

Kwa ufupi tusilazimishane wala kupangiana

Mie sichanji lakin pia naunga mkono kuletwa chanjo ili wenye kutaka kuchanja na wachanjwe
 
Sisi wazalendo tutapata chanjo ili t tujilinde na na tuwalinde wengone wasiambukizwe
 
Hata Matibabu ni hiyari

Kulazimisha watu kuchanja Chanjo ya Corona si sahihi kama ilivyokuwa kulazimisha watu wasijichanje pia sio sahihi

Weka ukiona sahihi kuchanja , basi chanjwa, ukiona sio sahihi acha

Kwa ufupi tusilazimishane wala kupangiana

Mie sichanji lakin pia naunga mkono kuletwa chanjo ili wenye kutaka kuchanja na wachanjwe
Lakini Kuna Sheria ya kudhibiti magonjwa ya mlipuko ( pamdmic) inalazimisha watu wote kupata chanjo, labda tunengie Sheria kwanza
 
C
Chanzo ni lazima mkuu hakuna namna.
Chanjo si lazima!! Ni hiari ya mtu! Labda itakuwa lazima kwa anayelazimika kusafiri nje ya nchi. Lakini sisi ambao hatuna mpango wa kwenda kwa nchi za wenzetu waliohalalisha hata ngon* za jinsia moja, hizo chanjo ni sawa na tak*tak*.
 
Ukweli huu hausemwi, watu wengi sana waliambukizwa corona lakini hawakupata dalili zozote za çorona. Na kwa njia hiyo watu hao walipata kinga ya asili dhidi ya corona! Huo ndio muujiza aliotufanyia Mungu hapa Tanzania!! Hatuhitaji chanjo!! Anayetaka kusafiri njè ya nchi huyo ndiye atalazimika kuchanjwa ili kuridhisha matakwa ya mabeberu na si kwa ajili ya kinga maana kinga ya asili anayo tayari.
 
Wa Tanzania tuna shida na vitu vikubwa viwili.
1. Maandishi
2. Vitu vyenye ncha kali.
 
Back
Top Bottom