Chanzo cha B. Dozen kuhama Clouds

TinyMonster

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2009
Posts
242
Reaction score
154

B. Dozen kuondoka Clouds wengi wanadhani ni sababu za marupurupu au kumsifia Diamond waziwazi ila ukweli ni kuwa chokochoko zilianza mwaka juzi baada ya marehemu Ruge kumchukua Kennedy toka East Africa Radio na kumuweka kwenye XXL akiwa na lengo la kumfanya awe sura ya kipindi.

Kwa miaka zaidi ya 10 XXL imekuwa ni kipindi kinachopendwa zaidi na vijana wa kuanzia miaka 17-25 kwa hiyo Ruge alitaka kuhakikisha sura ya kipindi inabaki vilevile ila isingewezekana wakati watangazaji tayari umri ulikuwa unakwenda na new generation ilikuwa inaanza kupoteza touch na kipindi.

Mwanzoni walitaka Meena Ally na Kennedy wahamie XXL ili BDozen awe phased out ila wakaona ingevuruga utaratibu ikabidi Meena apelekwe Amplifaya apate uzoefu. Baada ya Ruge kufariki ilikuwa kama imesahaulika ila kitendo cha Meena kupelekwa XXL kilimshtua B Dozen akajua anakuwa replaced ikabidi ajiwahi mwenyewe kwa kukataa kusaini mkataba mpya na kukubali ofa ya Majizo kujiunga E FM.

Kwa hali ilivyo inaonekana E FM anajipanga kubadili vipindi vyake toka mambo ya Uswahili na singeli kuwa redio ya vijana corporate media nyingine inabidi zijipange.

================

Jinsi Clouds walivyomuandaa Kennedy

===============

 

Hii kauli aliizungumza wiki iliyopita kwa 90% inaweza kuwa sababu ya kuhama.

Mngt baada kusikia kauli yake labda wakaamua waifanyie kazi kali yake.
 
Perfect Crispin the mnyama mkali atashika usukani

Sijui wengine huwa mnaangalia vipi uwezo wa watangazaji.

Iko hivi kwa show za mchana Tanzania yote hakuna kama Twangala.

Hao kina crispin ni wapiga kelele tu hawajui kitu.

Mtu aliyekuwa anamuweza Dozen kwa show za mchana alikuwa Kidbway na mwamba mmoja nimemsahau wa RFA miaka hiyo now days namuona yupo na online radio.
 
Mbowe hilo swala alishaliweka sawa kuwa B12 atahamia Kwa Majizo nadhani sahivi ni implementation tu .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…