Chanzo cha Mafuriko Morogoro mjini ni tuta la SGR, mamlaka zishughulikie hili

Lakini EIA hufanywa kabla ya mradi husika kuanza. Hii husaidia kuelewa athari ambazo zinaweza kujitokeza iwapo mradi huo utatekelezwa. Hivyo kabla hata ya kuanza mradi wa Ujenzi wa reli hiyo ilitakiwa EIA report itolewe ili hatua sahihi zichukuliwe. Yawapasa warudi sehemu hiyo na kuirekebisha kabla hayajatokea Maafa ikiwa ni pamoja na tuta hilo la reli kubomoka wakati mvua zikinyesha kwa wingi.
 
Inaonekana hata jiografia ya Morogoro huijui , tunaongelea kihonda
 
Ila twende na ule ukweli, kama kweli wameweka tuta katika manispaa ya Morogoro huo ni ushamba hata kama tuta halisababishi mafuriko mana leo viongozi wa SGR wamekanusha kupitia gazeti la Mwananchi kwa kusema kuwa tuta halijasababisha mafuriko kwa sababu mafuriko yalikuwa yakitokea hata kabla ya tuta.

Hivi kweli unaweka matuta mjini kweli wakati nguzo zipo? Duh! Kwani huko Uturuki na penyewe wameweka matuta miaka ya hivi karibuni? Matuta si ya enzi za mkoloni, au matuta ni imara sana kuliko nguzo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…