Chanzo cha ulimwengu na Mungu bado ni fumbo kwenye fikra za mwanadamu!

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
36,625
Reaction score
89,385
Natumai mu buheri..

Mada yangu leo nitapenda kuangazia misimamo mbalimbali juu ya uwepo wa Mungu/Miungu pamoja na chanzo cha ulimwengu na kisha nitagusia mtazamo wangu kutokana na mitazamo hiyo..
kumekuwa na mitazamo mbalimbali juu ya hizi hoja mbili lakini binafsi nionavyo katika mitazamo yote hiyo kuna dosari, hakuna iliyoleta majibu stahiki na ndipo hapo linapokuja neno "fumbo".

Dini/imani.

Kama mjuavyo kumekuwa na dini mbalimbali zote zikigusia maswala haya mawili juu ya ulimwengu pamoja na dini lakini bado imani hizi hazijakidhi ama kuthibitisha madai yoyote yahusuyo Mungu, na pia chanzo chake ama chanzo cha ulimwengu!.

Hata hivyo imani hizi zimekuwa zikirithishwa vizazi na vizazi na hii imekuwa hivi kwani binadamu yoyote mwenye ufahamu amekuwa akiuangalia ulimwengu nakufikiri hauwezi kuenenda hivi unavyoenenda pasipo kuwepo muumba wa ulimwengu huu!.

Si fikra mbaya isipokuwa haithibitishi kuwa kuna Mungu!, vivyohivyo imani hizi hazileti majibu yakutosha hata juu ya chanzo cha ulimwengu!. mfano wamekuwa wakiishia kusema kuwa ni fumbo la imani ama fikra za binadamu haziwezi kuelewa maswala ya kimungu na utendaji wake!. kwangu mimi hoja hizi ni dhaifu ni sawa na kujibu maswali magumu kwa hoja nyepesi!.

zipo sababu nyengine ambazo zimekuwa zikinifanya nisiamini katika hizi imani/dini.

Kwanza kutothibitika kwa nguvu wanazosema ni nguvu za mungu zifanyazo miujiza!
wamekuwa wakijinadi kuwa mungu wao ni mponyaji lakini ndo kwanza watu wamejazana hospitalini!.
Mungu mpenda haki na mwenye huruma!, lakini ndo kwanza akaumba dunia nakumuweka shetani!.
zipo hoja kedekede zinazofanya nione dini ama imani hizi haswa uislamu na ukristo kuwa ni janja janja ya watu fulani tu ili watawale watu nakujineemesha huku wao wenyewe wakiujua ukweli kuwa hawamjui Mungu na wala chanzo cha ulimwengu!.

Atheist.
Hawa ni wale wasiokubali uwepo wa Mungu!, hawa wanasema kabisa kuwa Mungu hayupo!.
Hoja zao nyingi nazielewa na wamekuwa ni chachu sana katika kukinzana hoja na watu wa dini wanaoamini uwepo wa Mungu!.

Hawa ninapopata mashaka nao ni sehemu moja tu hapo wanaposema "Mungu hayupo!".
dhana ya Mungu ama umungu ni pana kiasi inahitaji fikra pana katika kuielewa, nami nitaelewesha. kwanza nitaanza kwenye neno Mungu..

Mungu ni kitu chochote ambacho kwayo ndio chanzo cha kila kitu!, hii ndio tafsiri fupi nayakueleweka.
sasa kwenye dunia yetu tumekuwa na Miungu mingi ambayo watu wanaiabudu sasa atheist wanaposema Mungu hayupo vipi kwa wanaoabudu masanamu Miungu yao si inaonekana!, basi ipo!.

shida yangu na wao haipo hapo, shida yangu na wao ipo hapa hivi sijui kama huo usemi wao wanasema in general ama kwa miungu hiyo tu ambayo inafahamika!, vipi je, ikiwa kwenye kanuni za kiulimwengu Mungu akawa yupo..? maana mpaka hivi sasa hakuna alieweza kutafuta Mungu ulimwengu mzima na akamkosa!.. shida kauli yao ni kana kwamba wameshafanya survey nakujua kanuni zote na ndo wakaja na hiyo kauli yao yakusema Mungu hayupo!.

Sayansi..

Kwenye sayansi sitagusia sana maana sayansi bado inatafiti japo wengine wamekuwa wakipotosha wakisema sayansi inasema hakuna Mungu ama chanzo cha ulimwengu ni kitu fulani!.
jibu ni HAPANA, sayansi ni inamapendekezo mfano nadharia ya big bang ni nadharia tu sio kwamba ndio jibu la moja kwa moja.

Pia haijui chochote kuhusu Mungu, nashindwa kuelewa kwanini wengi wao wamekuwa wakiisakama sayansi nawakati sayansi ni uchunguzi wa kibinadamu ambao haujaelekea popote yani yenyewe ni inachunguza nakutoa majibu yanayothibitika kama haina uthibitisho inakaa kimya!, na sayansi haina kiongozi ya mtu yoyote anaweza kuanza tafiti wakati wowote ila tu usilete madhara kwa wengine!, so mi naona kila binadamu ni mwanasayansi muache ile dhana yakufikiri sayansi ni dini!.

Nini mtazamo wangu..?
Mimi sifungamani na atheist ama watu wanaoamini dini au Mungu wa waislamu na wakristo!.
msimamo wangu ni kuwa bado hatujui chochote kuhusu Mungu na kanuni zoote za ulimwengu.
kwamaana kanuni zote za ulimwengu hatujazijua!, Hatujui hata Mungu anamipaka au hana, ana ufahamu au hana ni kiumbe hai au sio hai, tumebakiza kuwaza kuwa yupo hivi ama vile hizo fikra sio kwamba ndio ukweli yupo hivyo tunavyodhani!..

Hapa tunajadili kuhusu chanzo chake na chanzo cha ulimwengu vipi kama kwenye kanuni za ulimwengu hakuna chanzo..? najua ni ngumu kuelewa lakini binafsi nahisi kuna kanuni zitakuja kutushangaza endapo tukija kuzigundua na vile ufahamu wetu mara nyingi hufikiri zaidi kwa yale mambo ambayo tumeyaona na kuishi nayo na ndio maana inakuwa ni rahisi sisi kuwaza kuwa kuna chanzo kwasababu nasisi kuzaliwa kwetu tunaona kuwa ndio mwanzo!, so hizo zinaweza kuwa ni kanuni zetu ktk mazingira yetu lakini isiwe ni kanuni yakiujumla ya ulimwengu!.

Binafsi sijui kama Mungu yupo ama hayupo kwasababu sina hakika na sijui chanzo cha ulimwengu kwasababu sijui hata kama kuna hiyo kanuni yakuwepo chanzo ama kutokuwepo!.

Hili swala la chanzo na Mungu vitaendelea kuwa fumbo, mpaka pale tutakapokuja kugundua kweli yake, ni heri kama binadamu tujibidiishe kwenye tafiti katika kuutafiti ulimwengu huko ndio kuna majibu, hizi kanuni tunazoona kama hazina majibu mimi ndio naona zinaweza kuleta mwanga wa nini ni nini!!.

Nafikiri nitakuwa nimechokoza kitu fulani kwenye ufahamu wako, mwenye hoja swali unakaribishwa.
 
Mimi huwa naunganisha sayansi na dini sehemu ambapo sayansi inasema kuna mystery force inayosabisha kitu hapo ndio na link hyo force itakuwa ndio mungu kama force inayosababisha expansion ya universe, force iliyosababisha the bing bang force inayofanya sehemu nyingine kwenye ulimwengu kwenda kinyume na kanuni za ulimwengu, hiy force ndio na hitimisha itakuwa ndio Mungu
 
Hiyo bado inakuwa haileti jibu!
 
Nashukuru sana kwa kutuandikia kwa uzito na uzuri wa kipekee kwenye mjadala huu wa kina na changamoto. Maandishi yako ni tafakuri ya dhati na ya kihalisia juu ya masuala ambayo yamekuwa yakizungumzwa kwa karne nyingi—uwepo wa Mungu, chanzo cha ulimwengu, na nafasi ya dini, sayansi, pamoja na mitazamo tofauti kama ya atheists.

Ningependa kutoa mchango wangu mdogo kwenye kila kipengele ulichogusia, na pia kukujibu kwa heshima ya hoja bila upendeleo wa upande wowote—kwa sababu mazungumzo haya ni ya kiakili na ya wazi, sio ya kishabiki wala kimapokeo.

1. Dini na Imani​

Umegusa hoja nzito—kwamba dini nyingi hazijatoa ushahidi wa moja kwa moja kuhusu Mungu wala chanzo cha ulimwengu. Ukweli ni kuwa dini nyingi hazijajikita sana kwenye ushahidi wa kisayansi, bali zaidi kwenye imani, urithi wa kiroho, na mfumo wa kijamii.

Swali lako la msingi lina mantiki: “Kwa nini dini hazijathibitisha kile zinachodai?”
Na jibu linaweza kuwa: Kwa sababu dini hazikuundwa kama taasisi za kisayansi, bali kama njia za kujibu maswali ya ki-kiroho na maadili katika jamii. Ila pale zinapojitokeza kudai kuwa zina ukweli wa ulimwengu mzima, ndipo zinapokutana na changamoto kubwa ya kuonyesha ushahidi wa wazi.

Kwa mfano:
  • Kauli ya "Mungu mponyaji" inaweza kuwa na uzito wa kiimani, lakini inaposhindwa kudhihirika katika mazingira ya kweli (kama wagonjwa kuendelea kuteseka), inapoteza mantiki ya kisayansi.
  • Swali lako la "Kwa nini Mungu mwenye huruma aumbe Shetani?" ni hoja ya mantiki inayowachanganya wengi, hata ndani ya dini husika. Inaibua changamoto za dhana ya "uhuru wa mapenzi" dhidi ya uweza wa Mungu.

2. Atheists (Wasiomwamini Mungu)​

Umegusa vizuri sana: Atheism ina nguvu sana katika kupinga hoja za kidini, lakini inapofikia kusema kwa uhakika “Mungu hayupo,” ndipo inajikuta katika matatizo yale yale ya watu wa dini: inadokeza uhakika usio na ushahidi kamili.
Unaposema:
“Vipi kama kwenye kanuni za kiulimwengu Mungu yupo?”
Hapo umetoa hoja muhimu—kwamba kusema Mungu hayupo ni kama kufunga mjadala kabla hujajua kanuni zote. Ni kama kusema “hakuna samaki baharini” kwa sababu hujawahi kuona kila kona ya bahari. Atheism inapopitiliza mipaka ya kutokuwa na imani hadi kufikia uhakika wa kutokuwepo kwa kitu kisichojulikana, inageuka kuwa imani nyingine—ya kukataa.

3. Sayansi​

Hongera kwa kueleza vizuri kwamba sayansi haina lengo la kutoa majibu ya kiroho. Sayansi ni chombo cha utafiti, na siyo dini wala mfumo wa kuabudu.

Mfano wa "Big Bang" ulivyogusia—ni nadharia, si ukweli wa mwisho. Nadharia zote ni za muda, zinaweza kubadilika endapo ushahidi mpya utapatikana. Sayansi hujihoji yenyewe—na hilo ndilo jambo zuri kwake.
Na kama ulivyosema:

“Kama haina ushahidi, inakaa kimya.”
Huu ni uaminifu wa kisayansi ambao dini nyingi hazina.

4. Mtazamo Wako (Agnosticism ya Kiakili)​

Nimevutiwa sana na msimamo wako wa kati—ambao kwa tafsiri ya jumla unaweza kuitwa “agnosticism ya kiakili”. Umesema wazi:

“Sijui kama Mungu yupo ama hayupo kwa sababu sina hakika...”
“Hatujui hata kama Mungu ni hai au hana mipaka...”
“Vipi kama kwenye kanuni za ulimwengu hakuna chanzo?”
Hizi ni hoja za utafiti, si za ushindani. Hoja ambazo hazifungamani na itikadi bali zinafungamana na bidii ya kutafuta. Huo ni msimamo wa heshima na wa ujasiri, kwa sababu si rahisi kuukubali kwa wengi ambao wanataka jibu rahisi—“ndiyo yupo” au “hapana hayupo.”

5. Hitimisho la Mawazo Yako:​

“Ni heri binadamu tujibidiishe katika tafiti, huko ndiko kuna majibu...”
Hii ni sauti ya mwanga, si mashaka. Ni aina ya ufahamu unaochochea mjadala na kuhamasisha tafakari ya kina, badala ya kukariri vitabu au misimamo.

Kama Hoja au Maswali:​

  1. Unadhani kutokujua ni hatua ya wapi kuelekea kujua?
  2. Je, unaamini kwamba ukweli wa ulimwengu huu unaweza kufikiwa na binadamu kwa asilimia 100?
  3. Vipi kama "hakuna ukweli mmoja", bali kila mtu ana ukweli wake kulingana na uwezo wake wa kufikiri?
 
Nashukuru sana kwa kutuandikia kwa uzito na uzuri wa kipekee kwenye mjadala huu wa kina na changamoto. Maandishi yako ni tafakuri ya dhati na ya kihalisia juu ya masuala ambayo yamekuwa yakizungumzwa kwa karne nyingi—uwepo wa Mungu, chanzo cha ulimwengu, na nafasi ya dini, sayansi, pamoja na mitazamo tofauti kama ya atheists.

Ningependa kutoa mchango wangu mdogo kwenye kila kipengele ulichogusia, na pia kukujibu kwa heshima ya hoja bila upendeleo wa upande wowote—kwa sababu mazungumzo haya ni ya kiakili na ya wazi, sio ya kishabiki wala kimapokeo.

1. Dini na Imani​

Umegusa hoja nzito—kwamba dini nyingi hazijatoa ushahidi wa moja kwa moja kuhusu Mungu wala chanzo cha ulimwengu. Ukweli ni kuwa dini nyingi hazijajikita sana kwenye ushahidi wa kisayansi, bali zaidi kwenye imani, urithi wa kiroho, na mfumo wa kijamii.

Swali lako la msingi lina mantiki: “Kwa nini dini hazijathibitisha kile zinachodai?”
Na jibu linaweza kuwa: Kwa sababu dini hazikuundwa kama taasisi za kisayansi, bali kama njia za kujibu maswali ya ki-kiroho na maadili katika jamii. Ila pale zinapojitokeza kudai kuwa zina ukweli wa ulimwengu mzima, ndipo zinapokutana na changamoto kubwa ya kuonyesha ushahidi wa wazi.

Kwa mfano:
  • Kauli ya "Mungu mponyaji" inaweza kuwa na uzito wa kiimani, lakini inaposhindwa kudhihirika katika mazingira ya kweli (kama wagonjwa kuendelea kuteseka), inapoteza mantiki ya kisayansi.
  • Swali lako la "Kwa nini Mungu mwenye huruma aumbe Shetani?" ni hoja ya mantiki inayowachanganya wengi, hata ndani ya dini husika. Inaibua changamoto za dhana ya "uhuru wa mapenzi" dhidi ya uweza wa Mungu.

2. Atheists (Wasiomwamini Mungu)​

Umegusa vizuri sana: Atheism ina nguvu sana katika kupinga hoja za kidini, lakini inapofikia kusema kwa uhakika “Mungu hayupo,” ndipo inajikuta katika matatizo yale yale ya watu wa dini: inadokeza uhakika usio na ushahidi kamili.
Unaposema:

Hapo umetoa hoja muhimu—kwamba kusema Mungu hayupo ni kama kufunga mjadala kabla hujajua kanuni zote. Ni kama kusema “hakuna samaki baharini” kwa sababu hujawahi kuona kila kona ya bahari. Atheism inapopitiliza mipaka ya kutokuwa na imani hadi kufikia uhakika wa kutokuwepo kwa kitu kisichojulikana, inageuka kuwa imani nyingine—ya kukataa.

3. Sayansi​

Hongera kwa kueleza vizuri kwamba sayansi haina lengo la kutoa majibu ya kiroho. Sayansi ni chombo cha utafiti, na siyo dini wala mfumo wa kuabudu.

Mfano wa "Big Bang" ulivyogusia—ni nadharia, si ukweli wa mwisho. Nadharia zote ni za muda, zinaweza kubadilika endapo ushahidi mpya utapatikana. Sayansi hujihoji yenyewe—na hilo ndilo jambo zuri kwake.
Na kama ulivyosema:

4. Mtazamo Wako (Agnosticism ya Kiakili)​

Nimevutiwa sana na msimamo wako wa kati—ambao kwa tafsiri ya jumla unaweza kuitwa “agnosticism ya kiakili”. Umesema wazi:

Hizi ni hoja za utafiti, si za ushindani. Hoja ambazo hazifungamani na itikadi bali zinafungamana na bidii ya kutafuta. Huo ni msimamo wa heshima na wa ujasiri, kwa sababu si rahisi kuukubali kwa wengi ambao wanataka jibu rahisi—“ndiyo yupo” au “hapana hayupo.”

5. Hitimisho la Mawazo Yako:​

Kama Hoja au Maswali:​

  1. Unadhani kutokujua ni hatua ya wapi kuelekea kujua?
  2. Je, unaamini kwamba ukweli wa ulimwengu huu unaweza kufikiwa na binadamu kwa asilimia 100?
  3. Vipi kama "hakuna ukweli mmoja", bali kila mtu ana ukweli wake kulingana na uwezo wake wa kufikiri?
  • Unadhani kutokujua ni hatua ya wapi kuelekea kujua?
Kwa jibu jepesi ni ndio, kwasababu utafiti ama dukuduku la kutafuta huwa linaanzia kwa kutokujua hapo ndipo kiu cha kutaka kujua huanzia!.
kuhusu wapi ni kujikita kwenye mifumo yote ya ulimwengu binafsi nahisi hii mifumo ita tupeleka kwenye jibu!.

  • Je, unaamini kwamba ukweli wa ulimwengu huu unaweza kufikiwa na binadamu kwa asilimia 100?
Ndio unaweza kufikiwa, nimejibu hivyo kwasababu umeniuliza kuwa ninaamini!, lakini sijajua kama sheria za kiulimwengu zinaruhusu hilo kwenye ufahamu wa binadamu!. ila iwe inaruhusu ama hairuhusu kwasababu hatujui yote hayo basi hatutakiwi kukaa tu kama mazwazwa kusubiri lakutokea!, mi nachojua akili ya binadamu huwa inakiu ya maarifa hata leo hii akigundua kitu kipya bado kesho atataka kugundua chengine ambacho hakijui!. lolote laweza kuwa jibu.

  • Vipi kama "hakuna ukweli mmoja", bali kila mtu ana ukweli wake kulingana na uwezo wake wa kufikiri?
sidhani kama swali lako umeuliza katika usahihi!, kwa maana hapa hatuangalii ukweli wa mtu kutokana na uwezo wake wakufikiri, hapa tunaangazia mazingira yanatuambia nini na sidhani kama mazingira yanaweza kutugeuka maana kama mkifanya tafiti iliyo sawa sidhani kama itawaletea jibu moja lenye majibu mchanganyiko!.
kama kuna hio kanuni yakuleta jibu moja ila inaleta majibu mchanganyiko basi itakuwa ni kanuni ya ajabu kuwahi kuwepo..😅
Na kama mtavutana juu ya jibu lipi ni sahihi basi bado hamjafikia jibu hapo nikuendelea na tafiti mpaka moja dhahiri ifahamike kwanini itokee mbili dhahiri!.
kama ni nyeusi ijulikane ni nyeusi na kama ni nyeupe ijulikane ni nyeupe!.
 
Kitabu pekee kinachoelezea habari za Mungu ni Biblia.

Na unaambiwa HAPO MWANZO MUNGU ALIUMBA MBINGU NA NCHI..

Aliziumba akiwa wapi?
Hapo tu anakwambia kabla mbingu ma hii dunia unayoitumia kumchunguza Mungu, alikuwepo
 
Mh!
 
  • Unadhani kutokujua ni hatua ya wapi kuelekea kujua?
Kwa jibu jepesi ni ndio, kwasababu utafiti ama dukuduku la kutafuta huwa linaanzia kwa kutokujua hapo ndipo kiu cha kutaka kujua huanzia!.
kuhusu wapi ni kujikita kwenye mifumo yote ya ulimwengu binafsi nahisi hii mifumo ita tupeleka kwenye jibu!.

  • Je, unaamini kwamba ukweli wa ulimwengu huu unaweza kufikiwa na binadamu kwa asilimia 100?
Ndio unaweza kufikiwa, nimejibu hivyo kwasababu umeniuliza kuwa ninaamini!, lakini sijajua kama sheria za kiulimwengu zinaruhusu hilo kwenye ufahamu wa binadamu!. ila iwe inaruhusu ama hairuhusu kwasababu hatujui yote hayo basi hatutakiwi kukaa tu kama mazwazwa kusubiri lakutokea!, mi nachojua akili ya binadamu huwa inakiu ya maarifa hata leo hii akigundua kitu kipya bado kesho atataka kugundua chengine ambacho hakijui!. lolote laweza kuwa jibu.

  • Vipi kama "hakuna ukweli mmoja", bali kila mtu ana ukweli wake kulingana na uwezo wake wa kufikiri?
sidhani kama swali lako umeuliza katika usahihi!, kwa maana hapa hatuangalii ukweli wa mtu kutokana na uwezo wake wakufikiri, hapa tunaangazia mazingira yanatuambia nini na sidhani kama mazingira yanaweza kutugeuka maana kama mkifanya tafiti iliyo sawa sidhani kama itawaletea jibu moja lenye majibu mchanganyiko!.
kama kuna hio kanuni yakuleta jibu moja ila inaleta majibu mchanganyiko basi itakuwa ni kanuni ya ajabu kuwahi kuwepo..😅
Na kama mtavutana juu ya jibu lipi ni sahihi basi bado hamjafikia jibu hapo nikuendelea na tafiti mpaka moja dhahiri ifahamike kwanini itokee mbili dhahiri!.
kama ni nyeusi ijulikane ni nyeusi na kama ni nyeupe ijulikane ni nyeupe!.
Hii mijadala ni mizito na ya kuvutia sana!
1. Kuhusu “Kutokujua ni hatua ya kuelekea kujua”:

Ni kweli kutokujua ndio chanzo cha kutaka kujua — lakini si kila kitu kisichojulikana kinaweza kujulikana. Katika falsafa, tuna kitu kinaitwa epistemic limitation — mipaka ya maarifa. Je, kama akili ya binadamu ina mipaka ya asili (intrinsic limits), kuna uwezekano kabisa kwamba baadhi ya mambo, kama chanzo cha ulimwengu au asili ya Mungu (ikiwa yupo), hayawezi kufikiwa kwa uelewa wa binadamu wa kawaida.
Hoja: Sio kila fumbo linafunguka. Kama kuna mipaka ya maarifa, basi hata kuamini kuwa kila kitu kinaweza kujulikana ni aina ya “imani”, si hakika.
2. Je, ukweli unaweza kufikiwa kwa 100%?
Hili swali linahitaji mjadala mpana sana. Tunaweza kufikia "ukweli wa muda" (provisional truth), au "ukweli wa mazingira" (contextual truth) lakini si lazima tuufikie ukweli wa mwisho (ultimate truth).
Mfano: Sayansi yenyewe hutegemea nadharia zinazoweza kupingwa (falsifiable). Nadharia ya Newton ilikuwa "ukweli" hadi Einstein alipoleta relativity. Sasa hata relativity ina changamoto zake kwenye kiwango cha quantum. Hii inaonyesha kuwa "ukweli wa kisayansi" ni wa muda tu — unakua kwa hatua, na pengine hatutawahi kupata 100%.
Hoja: Kama historia ya maarifa inaonyesha mabadiliko ya dhana, basi tunapaswa kuwa na unyenyekevu katika kudai tunaweza kufikia asilimia 100 ya ukweli.
3. Kuhusu “ukweli mmoja au ukweli wa kila mtu”
Hapa kuna tofauti kati ya ukweli wa kibinafsi (subjective truth) na ukweli wa jumla (objective truth). Mleta hoja anachanganya kati ya haya mawili. Ukiwa na kichwa kinauma, huo ni ukweli kwako (subjective), lakini joto la mwili kuwa 37.2°C ni ukweli wa jumla (objective).

Lakini hata katika ukweli wa jumla, kuna matatizo:
Mfano: Quantum mechanics inatuambia kuwa hali ya kitu inaweza kuwa na nafasi mbili kwa wakati mmoja (superposition). Hii inatufanya tujiulize — je, ukweli ni mmoja, au ni muktadha unaobadilika kulingana na mwelekeo wa mtafiti?
Hoja: Kama hata sayansi inatufundisha kuwa hali ya kitu inaweza kutegemea namna tunavyokichunguza, basi “ukweli mmoja” sio rahisi kama kusema nyeusi ni nyeusi, na nyeupe ni nyeupe — hasa kwenye masuala ya msingi kama asili ya Mungu au chanzo cha uhai.
4. Kuhusu mifumo ya ulimwengu kama njia ya kupata jibu
Ni hoja nzuri kusema mifumo inaweza kutupeleka kwenye majibu. Lakini je, hiyo mifumo ni ile tunayoielewa sasa? Au ni ile bado hatujui hata ipo?
Mfano: Kama kuna mifumo inayofanya kazi kwa mantiki tofauti kabisa na ile ya binadamu, je tutaitambua kwa kutumia akili hii hii?
Hoja: Kama kuna mifumo ambayo haifanani kabisa na mantiki yetu ya sasa, basi hata kuitambua itakuwa changamoto — tusipate kiburi cha kudhani kila kitu kitakaa mezani kwa akili ya mwanadamu.
5. Mwisho – Ushauri wa kifalsafa:
Ni busara kuendeleza tafiti na kuuliza maswali. Lakini pia ni busara kukubali kuwa baadhi ya maswali ni “maswali ya milele” — hayajibiwi haraka, na pengine majibu yake sio “ndiyo au hapana”, bali “inategemea”.:peepoPogStrip:
 
Back
Top Bottom