Nimependa hitimisho lako, tukirudi kwenye hoja yakuweza kujua kujua kwa 100%, si kitu ambacho tunatakiwa tukiangazie sana maana majibu hukosekana kwa muda tu haijalisha ni miaka mingapi itapita!, na ikiwa kanuni za ulimwengu hazitaki tujue hivyo basi inatakiwa walau tujue ya kwamba kanuni za kiulimwengu hazituruhusu sisi kujua ukweli kwa asilimia mia!, kuliko kuketi kusubiri ya kwamba mambo yataenda tu!.Hii mijadala ni mizito na ya kuvutia sana!
1. Kuhusu “Kutokujua ni hatua ya kuelekea kujua”:
Ni kweli kutokujua ndio chanzo cha kutaka kujua — lakini si kila kitu kisichojulikana kinaweza kujulikana. Katika falsafa, tuna kitu kinaitwa epistemic limitation — mipaka ya maarifa. Je, kama akili ya binadamu ina mipaka ya asili (intrinsic limits), kuna uwezekano kabisa kwamba baadhi ya mambo, kama chanzo cha ulimwengu au asili ya Mungu (ikiwa yupo), hayawezi kufikiwa kwa uelewa wa binadamu wa kawaida.
2. Je, ukweli unaweza kufikiwa kwa 100%?
Hili swali linahitaji mjadala mpana sana. Tunaweza kufikia "ukweli wa muda" (provisional truth), au "ukweli wa mazingira" (contextual truth) lakini si lazima tuufikie ukweli wa mwisho (ultimate truth).
3. Kuhusu “ukweli mmoja au ukweli wa kila mtu”
Hapa kuna tofauti kati ya ukweli wa kibinafsi (subjective truth) na ukweli wa jumla (objective truth). Mleta hoja anachanganya kati ya haya mawili. Ukiwa na kichwa kinauma, huo ni ukweli kwako (subjective), lakini joto la mwili kuwa 37.2°C ni ukweli wa jumla (objective).
Lakini hata katika ukweli wa jumla, kuna matatizo:
4. Kuhusu mifumo ya ulimwengu kama njia ya kupata jibu
Ni hoja nzuri kusema mifumo inaweza kutupeleka kwenye majibu. Lakini je, hiyo mifumo ni ile tunayoielewa sasa? Au ni ile bado hatujui hata ipo?
5. Mwisho – Ushauri wa kifalsafa:
Ni busara kuendeleza tafiti na kuuliza maswali. Lakini pia ni busara kukubali kuwa baadhi ya maswali ni “maswali ya milele” — hayajibiwi haraka, na pengine majibu yake sio “ndiyo au hapana”, bali “inategemea”.![]()
Hivi curiosity ni infinite au finite ?Nimependa hitimisho lako, tukirudi kwenye hoja yakuweza kujua kujua kwa 100%, si kitu ambacho tunatakiwa tukiangazie sana maana majibu hukosekana kwa muda tu haijalisha ni miaka mingapi itapita!, na ikiwa kanuni za ulimwengu hazitaki tujue hivyo basi inatakiwa walau tujue ya kwamba kanuni za kiulimwengu hazituruhusu sisi kujua ukweli kwa asilimia mia!, kuliko kuketi kusubiri ya kwamba mambo yataenda tu!.
Napendezwa na mfumo wa akili ya binadamu huwa haiishiwi kiu cha kutafuta maarifa!, ukitaka kulijua hilo binadamu yoyote ukikifunika kitu na ukamuambia usifunue atakuuliza kwanini..?
hilo swali tayari linatosha kukuashiria kitu, vilevile hata ukimuacha pekee atafunua ili ajue kwanini!.
so kama ulimwengu uliweza kuleta kiumbe cha namna hii, basi ni wazi pia ulimwengu upo radhi kufunuliwa ukweli wake na hichi kiumbe!.
Haya yote ni makisio tu kutokana na mazingira ila ukweli wote upo kwenye kanuni so hitimisho lako limemaliza kila kitu...
Curiosity kuwa infinite ama kutokuwa inategemea na vile kanuni za kiulimwengu na uwezo wetu pia ila hata kama itakuwa ni finite bado binadamu hawezi kuwa bored maana sisi akili yetu umejaa wingi wa ubunifu so nafikiri ndo tutazidi kuwa wabunifu ili pachangamke..😅Hivi curiosity ni infinite au finite ?
Ikitokea binadamu akajua kila kitu kuhusu ulimwengu anaweza kusafiri galaxy kwa galaxy, universe kwenda nyingine anaweza kumanipulate kanuni za ulimwengu yani kama ni civilization amepita type 7 amekuwa cteator civilization unahisi maisha yatakuwa mazuri au yatakuwa boring sana sababu ile curiosty hatuna tena hakuna cha kugundua tumeshagundua kila kitu
Kwenye podcast za joe rogan kuna moja alikuwa na michio kaku alielezea kitu kinaitwa laser porting. Ni technology ambayo kwa sasa ipo on theory tu Yani unakuwa upo duniani ila ufahamu wako unasafirishwa kwa kutumia laser kisha kule inatengeneza avatar unakuwa unasafiri sehemu nyingi tu, michio kaku anahisi huenda aliens kama wapo hii itakuwa ndio technology wanayotumiaCuriosity kuwa infinite ama kutokuwa inategemea na vile kanuni za kiulimwengu na uwezo wetu pia ila hata kama itakuwa ni finite bado binadamu hawezi kuwa bored maana sisi akili yetu umejaa wingi wa ubunifu so nafikiri ndo tutazidi kuwa wabunifu ili pachangamke..😅
na ubunifu sidhani kama ni finite!.
kusafiri galaxy kwa galaxy inawezekana kutokana na kina cha maarifa yatakavyoturuhusu, pia sidhani kama njia yakusafiri itakuwa ni nzuri sana maana itakuwa inachukua muda mrefu mno!, ila heri ikapatikana technology yakupotea nakutokea sehemu husika!.. ipo hiyo theory na wanasayansi wanahisi inawezekana kwa kutumia mtambo zinasomwa particles zako za mwili halafu zinafanyika kule unapotaka kwenda!, ila zile za awali zinapotezwa ili msiwe wawili so kule utatokea wewe yuleyule na ufahamu wako na kila kitu!.. ila bado ni theory!
ku manipulate kanuni kunakuja kuwa na mipangilio yake ili tusiharibu asili na kama hapa duniani tunavyoekeana sheria basi na hata huko baadae kuna sheria zitawekwa ili kulinda hayo, isipokuwa tu kumanipulite kuwa na msingi mzuri binadamu hufanya chochote anachoona kinamanufaa kwake!.
Ile nguvu iliyo sababisha kuwepo kwa ulimwengu mzima ndiyo Mungu na siyo propaganda za kidini tufahamu kwamba DINI zililetwa ili kuwatawala watu hasa waafrika pia zililetwa kuvunja tamaduni na asili ya AfrikaNatumai mu buheri..
Mada yangu leo nitapenda kuangazia misimamo mbalimbali juu ya uwepo wa Mungu/Miungu pamoja na chanzo cha ulimwengu na kisha nitagusia mtazamo wangu kutokana na mitazamo hiyo..
kumekuwa na mitazamo mbalimbali juu ya hizi hoja mbili lakini binafsi nionavyo katika mitazamo yote hiyo kuna dosari, hakuna iliyoleta majibu stahiki na ndipo hapo linapokuja neno "fumbo".
Dini/imani.
Kama mjuavyo kumekuwa na dini mbalimbali zote zikigusia maswala haya mawili juu ya ulimwengu pamoja na dini lakini bado imani hizi hazijakidhi ama kuthibitisha madai yoyote yahusuyo Mungu, na pia chanzo chake ama chanzo cha ulimwengu!.
Hata hivyo imani hizi zimekuwa zikirithishwa vizazi na vizazi na hii imekuwa hivi kwani binadamu yoyote mwenye ufahamu amekuwa akiuangalia ulimwengu nakufikiri hauwezi kuenenda hivi unavyoenenda pasipo kuwepo muumba wa ulimwengu huu!.
Si fikra mbaya isipokuwa haithibitishi kuwa kuna Mungu!, vivyohivyo imani hizi hazileti majibu yakutosha hata juu ya chanzo cha ulimwengu!. mfano wamekuwa wakiishia kusema kuwa ni fumbo la imani ama fikra za binadamu haziwezi kuelewa maswala ya kimungu na utendaji wake!. kwangu mimi hoja hizi ni dhaifu ni sawa na kujibu maswali magumu kwa hoja nyepesi!.
zipo sababu nyengine ambazo zimekuwa zikinifanya nisiamini katika hizi imani/dini.
Kwanza kutothibitika kwa nguvu wanazosema ni nguvu za mungu zifanyazo miujiza!
wamekuwa wakijinadi kuwa mungu wao ni mponyaji lakini ndo kwanza watu wamejazana hospitalini!.
Mungu mpenda haki na mwenye huruma!, lakini ndo kwanza akaumba dunia nakumuweka shetani!.
zipo hoja kedekede zinazofanya nione dini ama imani hizi haswa uislamu na ukristo kuwa ni janja janja ya watu fulani tu ili watawale watu nakujineemesha huku wao wenyewe wakiujua ukweli kuwa hawamjui Mungu na wala chanzo cha ulimwengu!.
Atheist.
Hawa ni wale wasiokubali uwepo wa Mungu!, hawa wanasema kabisa kuwa Mungu hayupo!.
Hoja zao nyingi nazielewa na wamekuwa ni chachu sana katika kukinzana hoja na watu wa dini wanaoamini uwepo wa Mungu!.
Hawa ninapopata mashaka nao ni sehemu moja tu hapo wanaposema "Mungu hayupo!".
dhana ya Mungu ama umungu ni pana kiasi inahitaji fikra pana katika kuielewa, nami nitaelewesha. kwanza nitaanza kwenye neno Mungu..
Mungu ni kitu chochote ambacho kwayo ndio chanzo cha kila kitu!, hii ndio tafsiri fupi nayakueleweka.
sasa kwenye dunia yetu tumekuwa na Miungu mingi ambayo watu wanaiabudu sasa atheist wanaposema Mungu hayupo vipi kwa wanaoabudu masanamu Miungu yao si inaonekana!, basi ipo!.
shida yangu na wao haipo hapo, shida yangu na wao ipo hapa hivi sijui kama huo usemi wao wanasema in general ama kwa miungu hiyo tu ambayo inafahamika!, vipi je, ikiwa kwenye kanuni za kiulimwengu Mungu akawa yupo..? maana mpaka hivi sasa hakuna alieweza kutafuta Mungu ulimwengu mzima na akamkosa!.. shida kauli yao ni kana kwamba wameshafanya survey nakujua kanuni zote na ndo wakaja na hiyo kauli yao yakusema Mungu hayupo!.
Sayansi..
Kwenye sayansi sitagusia sana maana sayansi bado inatafiti japo wengine wamekuwa wakipotosha wakisema sayansi inasema hakuna Mungu ama chanzo cha ulimwengu ni kitu fulani!.
jibu ni HAPANA, sayansi ni inamapendekezo mfano nadharia ya big bang ni nadharia tu sio kwamba ndio jibu la moja kwa moja.
Pia haijui chochote kuhusu Mungu, nashindwa kuelewa kwanini wengi wao wamekuwa wakiisakama sayansi nawakati sayansi ni uchunguzi wa kibinadamu ambao haujaelekea popote yani yenyewe ni inachunguza nakutoa majibu yanayothibitika kama haina uthibitisho inakaa kimya!, na sayansi haina kiongozi ya mtu yoyote anaweza kuanza tafiti wakati wowote ila tu usilete madhara kwa wengine!, so mi naona kila binadamu ni mwanasayansi muache ile dhana yakufikiri sayansi ni dini!.
Nini mtazamo wangu..?
Mimi sifungamani na atheist ama watu wanaoamini dini au Mungu wa waislamu na wakristo!.
msimamo wangu ni kuwa bado hatujui chochote kuhusu Mungu na kanuni zoote za ulimwengu.
kwamaana kanuni zote za ulimwengu hatujazijua!, Hatujui hata Mungu anamipaka au hana, ana ufahamu au hana ni kiumbe hai au sio hai, tumebakiza kuwaza kuwa yupo hivi ama vile hizo fikra sio kwamba ndio ukweli yupo hivyo tunavyodhani!..
Hapa tunajadili kuhusu chanzo chake na chanzo cha ulimwengu vipi kama kwenye kanuni za ulimwengu hakuna chanzo..? najua ni ngumu kuelewa lakini binafsi nahisi kuna kanuni zitakuja kutushangaza endapo tukija kuzigundua na vile ufahamu wetu mara nyingi hufikiri zaidi kwa yale mambo ambayo tumeyaona na kuishi nayo na ndio maana inakuwa ni rahisi sisi kuwaza kuwa kuna chanzo kwasababu nasisi kuzaliwa kwetu tunaona kuwa ndio mwanzo!, so hizo zinaweza kuwa ni kanuni zetu ktk mazingira yetu lakini isiwe ni kanuni yakiujumla ya ulimwengu!.
Binafsi sijui kama Mungu yupo ama hayupo kwasababu sina hakika na sijui chanzo cha ulimwengu kwasababu sijui hata kama kuna hiyo kanuni yakuwepo chanzo ama kutokuwepo!.
Hili swala la chanzo na Mungu vitaendelea kuwa fumbo, mpaka pale tutakapokuja kugundua kweli yake, ni heri kama binadamu tujibidiishe kwenye tafiti katika kuutafiti ulimwengu huko ndio kuna majibu, hizi kanuni tunazoona kama hazina majibu mimi ndio naona zinaweza kuleta mwanga wa nini ni nini!!.
Nafikiri nitakuwa nimechokoza kitu fulani kwenye ufahamu wako, mwenye hoja swali unakaribishwa.
Unaweza kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu..?Ile nguvu iliyo sababisha kuwepo kwa ulimwengu mzima ndiyo Mungu na siyo propaganda za kidini tufahamu kwamba DINI zililetwa ili kuwatawala watu hasa waafrika pia zililetwa kuvunja tamaduni na asili ya Afrika
Ungeandika mpaka pale nitakapokuja kugundua kweli yake....Chanzo na MUNGU ni fumbo kwako Wewe Tu na wasio na Imani kama Wewe...Binadamu WA kawaida unaetumia ubongo Tu tena ambae umedeviate kutoka kwenye Ile normality ya Original Binadamu hutoweza jua Chanzo cha universe au kama yupo Mungu Kwa sababu unazo limitations Kwa phase uliopo Kwa Sasa...MUNGU sio energy umpate kwenye utafiti,,,you need to go further an extra miles.Hili swala la chanzo na Mungu vitaendelea kuwa fumbo, mpaka pale tutakapokuja kugundua kweli yake, ni heri kama binadamu tujibidiishe kwenye tafiti katika kuutafiti ulimwengu huko ndio kuna majibu, hizi kanuni tunazoona kama hazina majibu mimi ndio naona zinaweza kuleta mwanga wa nini ni nini!!.
Haha! we kweli hamnazo!, ukisoma vyema ulichoandika utagundua ulivyojikaanga nakujibanika at the same time!..😅Ungeandika mpaka pale nitakapokuja kugundua kweli yake....Chanzo na MUNGU ni fumbo kwako Wewe Tu na wasio na Imani kama Wewe...Binadamu WA kawaida unaetumia ubongo Tu tena ambae umedeviate kutoka kwenye Ile normality ya Original Binadamu hutoweza jua Chanzo cha universe au kama yupo Mungu Kwa sababu unazo limitations Kwa phase uliopo Kwa Sasa...MUNGU sio energy umpate kwenye utafiti,,,you need to go further an extra miles.
Labda Kwa sababu hukunielewa.Haha! we kweli hamnazo!, ukisoma vyema ulichoandika utagundua ulivyojikaanga nakujibanika at the same time!..😅