Chanzo cha ulimwengu na Mungu bado ni fumbo kwenye fikra za mwanadamu!

Nimependa hitimisho lako, tukirudi kwenye hoja yakuweza kujua kujua kwa 100%, si kitu ambacho tunatakiwa tukiangazie sana maana majibu hukosekana kwa muda tu haijalisha ni miaka mingapi itapita!, na ikiwa kanuni za ulimwengu hazitaki tujue hivyo basi inatakiwa walau tujue ya kwamba kanuni za kiulimwengu hazituruhusu sisi kujua ukweli kwa asilimia mia!, kuliko kuketi kusubiri ya kwamba mambo yataenda tu!.

Napendezwa na mfumo wa akili ya binadamu huwa haiishiwi kiu cha kutafuta maarifa!, ukitaka kulijua hilo binadamu yoyote ukikifunika kitu na ukamuambia usifunue atakuuliza kwanini..?
hilo swali tayari linatosha kukuashiria kitu, vilevile hata ukimuacha pekee atafunua ili ajue kwanini!.
so kama ulimwengu uliweza kuleta kiumbe cha namna hii, basi ni wazi pia ulimwengu upo radhi kufunuliwa ukweli wake na hichi kiumbe!.
Haya yote ni makisio tu kutokana na mazingira ila ukweli wote upo kwenye kanuni so hitimisho lako limemaliza kila kitu...
 
Hivi curiosity ni infinite au finite ?

Ikitokea binadamu akajua kila kitu kuhusu ulimwengu anaweza kusafiri galaxy kwa galaxy, universe kwenda nyingine anaweza kumanipulate kanuni za ulimwengu yani kama ni civilization amepita type 7 amekuwa cteator civilization unahisi maisha yatakuwa mazuri au yatakuwa boring sana sababu ile curiosty hatuna tena hakuna cha kugundua tumeshagundua kila kitu
 
Curiosity kuwa infinite ama kutokuwa inategemea na vile kanuni za kiulimwengu na uwezo wetu pia ila hata kama itakuwa ni finite bado binadamu hawezi kuwa bored maana sisi akili yetu umejaa wingi wa ubunifu so nafikiri ndo tutazidi kuwa wabunifu ili pachangamke..πŸ˜…
na ubunifu sidhani kama ni finite!.

kusafiri galaxy kwa galaxy inawezekana kutokana na kina cha maarifa yatakavyoturuhusu, pia sidhani kama njia yakusafiri itakuwa ni nzuri sana maana itakuwa inachukua muda mrefu mno!, ila heri ikapatikana technology yakupotea nakutokea sehemu husika!.. ipo hiyo theory na wanasayansi wanahisi inawezekana kwa kutumia mtambo zinasomwa particles zako za mwili halafu zinafanyika kule unapotaka kwenda!, ila zile za awali zinapotezwa ili msiwe wawili so kule utatokea wewe yuleyule na ufahamu wako na kila kitu!.. ila bado ni theory!

ku manipulate kanuni kunakuja kuwa na mipangilio yake ili tusiharibu asili na kama hapa duniani tunavyoekeana sheria basi na hata huko baadae kuna sheria zitawekwa ili kulinda hayo, isipokuwa tu kumanipulite kuwa na msingi mzuri binadamu hufanya chochote anachoona kinamanufaa kwake!.
 
Kwenye podcast za joe rogan kuna moja alikuwa na michio kaku alielezea kitu kinaitwa laser porting. Ni technology ambayo kwa sasa ipo on theory tu Yani unakuwa upo duniani ila ufahamu wako unasafirishwa kwa kutumia laser kisha kule inatengeneza avatar unakuwa unasafiri sehemu nyingi tu, michio kaku anahisi huenda aliens kama wapo hii itakuwa ndio technology wanayotumia
 
Ile nguvu iliyo sababisha kuwepo kwa ulimwengu mzima ndiyo Mungu na siyo propaganda za kidini tufahamu kwamba DINI zililetwa ili kuwatawala watu hasa waafrika pia zililetwa kuvunja tamaduni na asili ya Afrika
 
Ile nguvu iliyo sababisha kuwepo kwa ulimwengu mzima ndiyo Mungu na siyo propaganda za kidini tufahamu kwamba DINI zililetwa ili kuwatawala watu hasa waafrika pia zililetwa kuvunja tamaduni na asili ya Afrika
Unaweza kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu..?
 
Ungeandika mpaka pale nitakapokuja kugundua kweli yake....Chanzo na MUNGU ni fumbo kwako Wewe Tu na wasio na Imani kama Wewe...Binadamu WA kawaida unaetumia ubongo Tu tena ambae umedeviate kutoka kwenye Ile normality ya Original Binadamu hutoweza jua Chanzo cha universe au kama yupo Mungu Kwa sababu unazo limitations Kwa phase uliopo Kwa Sasa...MUNGU sio energy umpate kwenye utafiti,,,you need to go further an extra miles.
 
Binadamu ni kama nimfananishe na Uranium kwamba kuna energy alikuwa nayo alipokuwa original ila Kwa kule kudecay Hadi akafikia kuwa germanium hayupo kwenye uwezo ubora WA kuradiate Ile energy aliokuwa nayo Yule binadamu original aliekuewa mfano WA Uranium..
 
Haha! we kweli hamnazo!, ukisoma vyema ulichoandika utagundua ulivyojikaanga nakujibanika at the same time!..πŸ˜…
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…