Chanzo cha umasikini Afrika sio viongozi ila ukosefu wa ujuzi wa sayansi na teknolojia

Chanzo cha umasikini Afrika sio viongozi ila ukosefu wa ujuzi wa sayansi na teknolojia

Masi Lambo

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2020
Posts
532
Reaction score
360
Jibu rahisi la waafrika wote ambalo wamepewa na mabeberu, la kwanini Afrika ni masikini, ni 'ubaya na kasoro za viongozi wetu'. Lakini jibu sahihi ni ukosefu wa ujuzi wa kisayansi na teknolojia, kuzalisha na kutengeneza bidhaa kwa kutumia malighafi na madini yetu. Kwa sababu sio rahisi kupata teknolojia za magharibi, walio wengi wana kimbilia kuamua ni viongozi wetu wenye kasoro.

Kwenye nchi yenye matatizo ya uongozi hat vita, ndipo mabeberu wanapopata mwanya wa kuingilia na kunyonya chochote mbele yao hata kuiba, kama walivyofanya Libya. Hivyo mabeberu kila siku watawarubuni muone viongozi wenu ni wabaya, watawapa silaha mpigane kama Congo, silaha zote zinatoka kwa mabeberu wa magharibi na mashariki.

Kwanza tuanze na ujuzi wa magharibi tuliokwama kuupata, mfano mdogo ni nguo za jeans. Nguo hizi zinatengenezwa na asilimia mia ya pamba ambayo tunazalisha hapa kwetu, lakini hatuwezi kutengeneza jeans, hivyo tunaagiza kutoka Ulaya kwa bei kubwa mara mia ya bei ya pamba tulio wauzia.

Hatuwezi kugoma kuwauzia pamba kwa bei wanayo tupangia kwa sababu itatuozea, hivyo tunauza kwa bei ya chini ambayo haikidhi mahitaji ya mkulima hata ya kununulia mbegu mpya na madawa ya mimea, wengie hata chakula.

Mfano wa pili ni madini yetu, wenzetu magharibi wanayatumia kutengeneza ndege, meli, magari, ndege zisizo na rubani, games for kids, simu, computers etc. Kwa hiyo madini kwao ni kitu ghali sana kukipata, ingawaje wanao wauzia wananunua kwa bei nafuu na rahisi sana kutoka kwetu, hata bure, wajinga wengine wanabadilishana na silaha za kuuana wenyewe kwa wenyewe, na kuvuruga nchi.

Wananunua bei rahisi toka kwetu sababu kwanza hayajasafishwa wanaponunua, pia matumizi yake kwetu ni kuvaa tu, hivyo thamani yake kwetu ni ndogo ingawaje tunaona mwenye madini ni tajiri sana. Yakifika Ulaya madini haya ni bei ya kununua nchi ya Afrika. SIjui kama tunaelewana kwenye hili somo la kidato cha kwanza?

Kuna malighafi nyingi tu ambazo Ulaya zinahitajika sana, kama glass, plastic, Sisal, wood etc, lakini kwetu vitu hivi vina matumizi madogo kulinganisha na wao wenye viwanda vya magari na majumba makubwa hata barabara na madaraja. Hawana cement Ulaya inatoka Afrika na Asia, lakini ni wajengaji wakubwa duniani baada ya China.

Mashariki ya kati na mbali wameishiwa mchanga wa kujengea madaraja na majumba, sasa China inatoa mchanga toka nchi jirani, ilichukua hata kwetu wakati wa Kikwete, ambaye namuweka katika kundi dogo la viongozi walio sababisha umasikini ukuwe Afrika, ila sio sababu kuu.
 
Ujerumani na Italia ni wazalishaji wakubwa wa cement Ulaya.
Upo mchanga wa kutosha Mashariki ya kati na ya mbali
Acha story za utopolo.
 
Usitetee wachovu. Chanzo ni viongozi uchwara wasio na maono.

China na Japan walikuwa nyuma kimaendeleo na kielimu(hasa sayansi).Baada ya kutawaliwa na kujikomboa walitambua silaha ya watawala wao(wakoloni). Na viongozi walianzisha uharamia wa kitaaluma kwa kutuma vijana kwenda kuiba ujuzi nchi za magharibi.Baada ya muda wakafanya mageuzi/mapinduzi makubwa(kwa vitendo) na leo tunashuhudia ni washindani wakubwa wa "super powers".Hata Malaysia na Korea ya Kusini ni mifano.

Ajabu huku kwetu juhudi zinazofanywa na wanaojiita "waheshimiwa" ni kulinda utukufu wao kwa gharama za maisha duni kwa raia ili waendelee kuonekana "matawi ya juu" miongoni mwa fukara.Hakuna mikakati ya dhati ya kujikwamua bali maneno matupu,mara kilimo kwanza,mkurabita,mkukuta,mikopo kwa wajasiria mali,n.k Ukipima mafanikio na dira kiuhalisia ni 0!

Wanachoweza ni wizi,ukandamizaji wa raia/wenye mtizamo tofauti na wao,anasa(utitiri wa vimada),upendeleo (nepotism),kujikomba kwa wakoloni na mengine yenye kutia aibu hata kuyatajwa (miongoni uchawi!).
Kwa mazingira hayo nani alaumiwe kama si watunga sera,siasa na watawala wanaodhani wao ndiyo injini za mataifa yao kwa kuhodhi kila kitu na hawataki kushauriwa wala kukosolewa wanapopotoka!
 
Sio kweli. Tatizo ni mitazamo tuliyojijengea tu na iman kuwa bila wazungu hatuwez na kuzarau vya kwetu.
Ili uamin mtu akivunjika mfupa wa mguu kwenye ajari, hospital watamwambia waukate ila mtaani watauunga na kurudi kama hawali je hii sio technology?
 
Tatizo la kutokuwepo sayansi na technologia linasababishwa na uongozi mbovu ulioko Africa. Korea ya Kusini miaka ya 1970 ilikuwa maskini kama Tanzania lakini sasa ni moja ya nchi zilizo juu zaidi duniani kitechnolojia.
 
Tatizo wala si sayansi wala teknolojia...
Tatizo la Waafrika wengi ni ujinga, unafiki, uvivu, kimbelembele, uzandiki, kujipendekeza na kuabudu miungu-watu!
Na ndo maana badala ya kutengeneza mifumo imara huku Afrika tunaibua watu imara na walevi wa madaraka!
Mifumo imara inadumu na kuleta maendeleo.... Watu imara wanapita na kutokomea!!
 
Mkuu upo sahihi kwa upande mmoja wa teknolojia na sayansi lakini umesahau upande mwingine wa uzalendo. Kuwepo na teknolojia na sayansi ya kiwango chochote lakini bila uzalendo (kwa maana ya uongozi bora na upendo kwa nchi yako), sayansi+ technology ni kazi bure.
 
Umasikini wa Africa chanzo ni watawala wa kiafrica ambao wametokana na mifumo ya mibovu ya uongozi.Unampa mwafrika Kinga ya kutoshtakiwa halafu utegemee maendeleo.Aah wapi
 
Mkuu upo sahihi kwa upande mmoja wa teknolojia na sayansi lakini umesahau upande mwingine wa uzalendo. Kuwepo na teknolojia na sayansi ya kiwango chochote lakini bila uzalendo (kwa maana ya uongozi bora na upendo kwa nchi yako), sayansi+ technology ni kazi bure.
Uzalendo utoke wapi, mfano mwanasiasa aliyemaliza darasa la saba anayesinzia bungeni miaka 5 akisema ndio akimaliza mda wake anapata mapato makubwa ambapo mwanasayansi amekaa darasani miaka 20 huku akifanya kazi miaka 40 afikii mapato ya miaka 5 ya mbunge asinziae,hapa uzalendo utoke wapi
 
Tatizo la kutokuwepo sayansi na technologia linasababishwa na uongozi mbovu ulioko Africa. Korea ya Kusini miaka ya 1970 ilikuwa maskini kama Tanzania lakini sasa ni moja ya nchi zilizo juu zaidi duniani kitechnolojia.
Chanzo ni mfumo Bora wa uongozi,Hakuna Kinga ya kutoshtakiwa,Hakuna ufisadi rushwa, matumizi mabaya ya madaraka,Kodi za wananchi,wamewatumia positive mabeberu kuendelea maana Hakuna nchi iliyowahi shirikiana na mabeberu ikawa masikini.
 
Uzalendo utoke wapi, mfano mwanasiasa aliyemaliza darasa la saba anayesinzia bungeni miaka 5 akisema ndio akimaliza mda wake anapata mapato makubwa ambapo mwanasayansi amekaa darasani miaka 20 huku akifanya kazi miaka 40 afikii mapato ya miaka 5 ya mbunge asinziae,hapa uzalendo utoke wapi

Mkuu unaelewa uzalendo ni nini??!!
 
Ni bangi tupu : suali kwanini nchi za asia ni bora kuliko afrika? kama vile Taiwan, Singapore, Malaysia, Thailand, Vietnam, etc
 
Mimi naona jambo kubwa lakufanya rais Magufuli kwanza engepiga marufuku bangi. mzee kwa bangi zako leo hii useme mm natakakusafirisha mananasi ya Tanzania niyapeleke nje wakati mkulima anafaidika basi huwezi kwa upuuzi wa serikali ya ccm wanakuendesha mpaka utakata tamaa. chanzo ya umasikini wa Afrika ni viongozi tena 100%
 
Mtoa mada sema tu umekusudia kumsema JK kwa husda uliyonayo kutokana na mafanikio yake katika utendaji wake ukilinganisha na JPM. Enzi za JK uchumi ulishawahi kupanda zaidi ya 8% kiwango ambacho JPM hatakaa akifikie pamoja na kujifanya kuwa "mjenga uchumi".

Lakini ukweli ni kwamba ukuaji wa uchumi wetu kwa sasa ni chini ya 6% kwa mujibu wa IMF taarifa ambazo JPM hataki zichapishwe. Ingawa waziri wa wa Fedha na Minpango ameonesha "mgando" katika ukuaji wa uchumi kwa kulinganisha miaka miwili iliyopita (7%) ni uongo, uchumi umedidimia zaidi bali serikali inajaribu kufanya "balance" kuficha uhalisia wa kushuka kwa uchumi kujilinda kisiasa.

Tukirudi kwenye hoja kwamba tatizo la umasikini (uchumi mbaya) ni kutokana na ukosefu wa teknolojia na si uongozi, hapa ni dhahiri unakusudia "kumkinga" JPM na lawama za anguko la kiuchumi ambalo tunapitia kwa sasa. Kwamba tatizo si JPM bali ni "asili" yetu ya kukosa maarifa ya kisayansi. Unapotosha.

Kumbuka, dhima ya uongozi ni kutoa dira katika maendeleo ya nchi. Tofauti ya maendeleo ya kiuchumi baina ya nchi tajiri na masikini (Africa) inatokana na tofauti ya kiwango cha uwekezaji (support) katika utafiti na maendeleo (R&D) ambayo ndo msingi wa teknolojia na uchumi wenyewe. Serikali (uongozi) za nchi zenye maendeleo makubwa zinawekeza zaidi kwenye R&D kuliko nchi masikini ambazo huwekeza zaidi katika vitu (structures).

Hebu jiulize mwenyewe serikali hii ya JPM imetenga kiasi gani cha fedhs katika bajeti yake kwa ajili ya R&D? Lakini kama kweli unaamini tatizo la umasikini si uongozi bali ukosefu wa teknolojia, je, unatarajia Tanzania itaondokana na umasikini uliopo kwa kuwekeza matrilioni ya shilingi kwenye miradi ya ujenzi wa SGR na JNHPP? Hivi anayeamua fedha za nchi zitumike zaidi kwenye miradi ya ujenzi badala ya R&D si viongozi?

Je, unafahamu kwamba changamoto ya mlipuko wa ugonjwa wa korona inaweza kuwa ni chachu ya kuwekeza kwenye utafiti na maendeleo? Je, serikali imetenga fedha kiasi gani na maelekezo gani hadi sasa kusapoti wanasayansi ili wafanye tafiti na kuweza kuzalisha vipimo, dawa, kinga na vifaa tiba dhidi ya korona na magonjwa mengine?
 
Tatizo ni kwamba viongozi waafrika wamewekeza zaidi katika kuheshimiwa,viongozi wa Africa wanahusudu sana heshima na siyo uwajibikaji.
 
Back
Top Bottom