Mtoa mada sema tu umekusudia kumsema JK kwa husda uliyonayo kutokana na mafanikio yake katika utendaji wake ukilinganisha na JPM. Enzi za JK uchumi ulishawahi kupanda zaidi ya 8% kiwango ambacho JPM hatakaa akifikie pamoja na kujifanya kuwa "mjenga uchumi".
Lakini ukweli ni kwamba ukuaji wa uchumi wetu kwa sasa ni chini ya 6% kwa mujibu wa IMF taarifa ambazo JPM hataki zichapishwe. Ingawa waziri wa wa Fedha na Minpango ameonesha "mgando" katika ukuaji wa uchumi kwa kulinganisha miaka miwili iliyopita (7%) ni uongo, uchumi umedidimia zaidi bali serikali inajaribu kufanya "balance" kuficha uhalisia wa kushuka kwa uchumi kujilinda kisiasa.
Tukirudi kwenye hoja kwamba tatizo la umasikini (uchumi mbaya) ni kutokana na ukosefu wa teknolojia na si uongozi, hapa ni dhahiri unakusudia "kumkinga" JPM na lawama za anguko la kiuchumi ambalo tunapitia kwa sasa. Kwamba tatizo si JPM bali ni "asili" yetu ya kukosa maarifa ya kisayansi. Unapotosha.
Kumbuka, dhima ya uongozi ni kutoa dira katika maendeleo ya nchi. Tofauti ya maendeleo ya kiuchumi baina ya nchi tajiri na masikini (Africa) inatokana na tofauti ya kiwango cha uwekezaji (support) katika utafiti na maendeleo (R&D) ambayo ndo msingi wa teknolojia na uchumi wenyewe. Serikali (uongozi) za nchi zenye maendeleo makubwa zinawekeza zaidi kwenye R&D kuliko nchi masikini ambazo huwekeza zaidi katika vitu (structures).
Hebu jiulize mwenyewe serikali hii ya JPM imetenga kiasi gani cha fedhs katika bajeti yake kwa ajili ya R&D? Lakini kama kweli unaamini tatizo la umasikini si uongozi bali ukosefu wa teknolojia, je, unatarajia Tanzania itaondokana na umasikini uliopo kwa kuwekeza matrilioni ya shilingi kwenye miradi ya ujenzi wa SGR na JNHPP? Hivi anayeamua fedha za nchi zitumike zaidi kwenye miradi ya ujenzi badala ya R&D si viongozi?
Je, unafahamu kwamba changamoto ya mlipuko wa ugonjwa wa korona inaweza kuwa ni chachu ya kuwekeza kwenye utafiti na maendeleo? Je, serikali imetenga fedha kiasi gani na maelekezo gani hadi sasa kusapoti wanasayansi ili wafanye tafiti na kuweza kuzalisha vipimo, dawa, kinga na vifaa tiba dhidi ya korona na magonjwa mengine?