Chanzo cha umasikini kwa vijana wengi si wanawake ni kamari( betting)

Acha upotoshaji. Mwanaume anaweza kuishi bila kubeti lakini nivigumu kuishi bila mwanamke pili .vijana wengi watanzania hawana uwezo wa kubeti hata 1$ sasa hizi herojero ndio inasababisha umaskini? Je mwanamke ukimpa jero atakubali? Kwahiyo umeandika nonsense
 
 
Hayo ni maoni yako

Binafsi naona Wanawake, Ulevi, Kamari ndiyo chanzo kikuu cha Wanaume wengi kupoteza kipato

Kama ni mtu wa kufanya tathmini ya kipato na matumizi, utaungana na Mimi

Kuna mtu unakuta ana mademu 3, na wote huwapatia sio chini ya 300,000 kwa mwezi

Ukija kwenye Ulevi, Kuna mtu anatumia sio chini ya shilingi 60,000 kwa wiki kunywa

Ukipiga hesabu, sio chini ya milioni 1.1 zinatumika kwenye hayo masuala

Ukifanya hesabu hiyo kwa mwaka, utajikuta unapoteza sio chini ya milioni 12 kwenye hilo eneo (kutegemeana na kiwango)

Kiasi hicho ukisema ununue mashamba na kupanda miti ya mbao kule Mufindi, hukosi ekari 12 Kila mwaka
 
Mimi binafsi naona Betting inaweza kua ni chanzo cha baadhi ya maradhi yanayo wapata vijana kwa sasa,
mfano,msongo wa mawazo au stress ni hatari sana,

Msongo wa mawazo ukiwa wa muda mrefu huweza kukusababishia magonjwa kama,Shinikizo la juu la damu,kisukari,kupungua kwa mfumo wa kinga mwilini,Depression,Anxiety,matatizo ya kukosa usingizi,kupoteza kumbukumbu,
Haya ni baadhi tu ya madhara ya kua na stress au msongo wa mawazo,tukiachana na issue ya madhara ya kiuchumi kwenye hiyo Betting.
 
Nadhani ingeshafutwa ila ndo platform pekee ya kuchukua kodi kwa wazalishaji wasio rasmi otherwise kwanini isifutwe? Inanufaisha wachache mno kwa kuumiza wengi.
 
Hahaha nimeshangaa mpaka nimetetemeka kabisa
Bwashee,kwani lengo la watu kutafuta hela hua ni nini?
Sio matumizi kwa kila upendavyo kutumia?

Unaenda kunywa bia mtu anakwambia unapoteza hela za kununua shamba la mbao!
Ukimuuliza,wewe usiyekunywa Pombe,una mashamba mangapi? si ajabu akawa hana hata shamba moja!
 
Kabisa kila mtu anamalengo na pesa zake anazotafuta 😅 tatizo kila mtu anafosi malengo yake yawe ya mwingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…