Hata kama ni kada na unatetea chama fulani, tufikiri kwa kutumia akili. Siyo kila kitu ni ushabiki. Chukulia mf. majimbo ya uchaguzi kule Zanzibar mengine hayalingani na kata moja huku bara. Kuendelea kugawa nchi ktk sehemu ndogo za kiutawala ni kuwabebesha mzigo walipa kodi. Ni huduma zipi zimeathiriwa na ongezeko la watu au ukubwa wa maeneo ya kiutawala tuliyonayo sasa hivi? Nilitegemea baadhi ya majimbo ya uchaguzi yapunguzwe kwasababu kipindi hiki huduma za mawasiliano ikiwemo barabara na simu yameimarika badala yake wanayaongeza kisiasa ili watu fulanifulani wapate ajira.
Kuboresha huduma kwa jamii kunaaitaji miundombinu kwa hizo huduma na wataalam, siyo kuongeza wabungu na Wakuu wa wilaya. Nyie chawa sijuhi hamfikiriagi, kazi yenu ni kutetea hadi ujinga.