Chanzo cha vita ya India na Pakistan inayoendelea hivi leo katika eneo la Kashmir

pia Wayaud walikwepo wengi sana kwenye nchi za kiarabu kabl ya mwaka 1948 hasa Palestine ila ubaguz wa waarab uliochochewa na viongoz wao wabovu mf Arafat na Gadaf ndo ilipeleka wayaud kukimbia nchi za kiarab na kwenda Israel , pia wayaud walioletwa mwaka 1948 ni wachache sana kulinganisha na waliokwepo hapo awali

Muammar Gaddafi kaingia madarakani baada ya kumpindua Mfalme Idris Septemba mwaka 1969. Mwaka 1948 alikuwa mdogo sana. Yasser Arafat kazaliwa 1929, mwaka 1948 alikuwa Ana miaka 19.

Hivyo unaposema ni ubaguzi wa waarabu ndio uliwakimbiza mayahudi kutoka nchi zao wakakimbilia "Israel" mwaka 1948, tena eti kwa ubaguzi wa waarabu kuchochewa na viongozi wao wabovu kisha ukawataja kama eti Gaddafi na Arafat, inaonesha ima hujui au unakwepesha ukweli makusudi, au huelewi kabisa unachokisema.

Halafu kwanini mayahudi waliishi kwa amani mashariki ya kati na waarabu mpaka walipokuja mayahudi wazungu kutoka Ulaya waliowakimbia ndugu zao wakristo waliokuwa wakiwatesa na kuwaua, wakakimbilia mashariki ya kati wakidai ni kwao ndio mayahudi wa mashariki ya kati wakaanza kukimbilia nchi ya kizayuni?

Halafu katika ardhi ya Palestine kabla mayahudi hawajaanza kuhamia, mayahudi waliokuwepo pale wenyeji mpaka karne ya 19 walikuwa ni wachache. Wengine wengi ni wahamiaji pale.
 
Kitu watu wengi hawajui Palestine ilipiganiwa sana na wayaudi na sio waaranbu ( leo wanajiita wapalestina )
Kuipigania kivipi? Kuanzia lini? Walichofanya walikuja pale wakasema ni kwao, baada ya waliotoka Ulaya huko ambapo walikuwa wakiteswa wakakimbilia pale na kudai ni kwao.
 
Hata Pakistan na India Mwanzo zilikuwa zimeungana na India na ilikuwa ni eneo moja, baada ya utofauti wa itikadi za kidini zilizoathiri siasa, Pakistan ikajitenga ikawa Nchi moja yenye maeneno mawili yasioungana, kukawa na Western Pakistan na Eastern Pakistan, zote zikiwa Chini ya utawala wa serikali ya Pakistan. Lakini kutokana na umbali wa kijografia na sababu nyinginezo Eastern Pakistan ikajitenga na Western Pakistan, na Eastern Pakistan wakabadili jina na kujiita Bangladesh. Sasa hapo kipi hakijaeleweka....

Same applied kwa Palestina na Israel... mwanzo zilikuwa Eneo moja, ila baada ya Wayahudi kudai utawala wao walipotoka uamishoni, ndio kukazuka vita, na maeneo yakatengana kulingana na itikadi za kidini, Kwa sababu Waislamu wengi walikuwa Gaza na West Bank, basi ikawa hivyo na taifa hilo la Palestina likabaki na hayo maeneo huko Wayahudi wakiteka baadhi ya maeneo mengine.
Soma tena historia ya Mgogoro Israel na Palestina halafu ondoa issue ya dini
 
Muhindi hawezi kushindwa vita hapo.... kwanza muhindi raia wake tu wanafika Billion 1.4 ambao ni mtaji tosha kwenye uzalishaji wa wapiganaji, huku Pakistan raia wake wakiwa Million 200 tu, Yani India anamzunguka Pakistan mara 7 kwa idadi ya Raia.

Tukizungumzia Utajiri au Pato la Taifa tu... India ina pato la dollar Trillion 3.7 huku Pakistan ikiwa na Pato la dollar billion 374, yani pato la India ni mara 10 ya pato la Pakistan

India inaizidi Pakistan karibia kila kitu
Eneo ilo india ana maadui wengi sana ikiwemo China, pigo la kwanza tu India ime pata lose tayari Na kwenye hii vita atakae umia zaidi ni India
.

View: https://x.com/clashreport/status/1920123876341645475
 
Mwezi wa huu wa Mei mwaka 2025, ulimwengu umetikiswa na mgogoro mpya kati ya mataifa mawili yenye historia ndefu ya mvutano – India na Pakistan. Tarehe 6 Mei, India ilitangaza operesheni kali iliyobeba jina "Operation Sindoor," ikilenga maeneo tisa ndani ya Pakistan na kipande cha eneo la Kashmir linaloendeshwa au kudhibitiwa na serikali ya Pakistan. Hii ilikuwa hatua ya kulipiza kisasi kufuatia shambulio baya la kigaidi lililotokea tarehe 22 Aprili 2025 katika eneo la Pahalgam, katika mji wa Kashmir, ambapo watu 26, wengi wao wakiwa watalii wa Kihindu, walipoteza maisha.

India iliamua kuchukua hatua kali dhidi ya makundi ya kigaidi kama Lashkar-e-Taiba na kundi la Jaish-e-Mohammed, yaliyoshutumiwa kwa kupanga mashambulizi hayo ambayo yaliua watu 26 katika mji huo. Ambapo Mashambulizi ya anga na makombora yalifanyika kwa lengo la kuharibu miundombinu ya kigaidi. Wizara ya Ulinzi ya India ilieleza kwamba operesheni hiyo ilikuwa "imepangwa kwa uangalifu, isiyolenga kusababisha vita vikubwa." Hata hivyo, taarifa kutoka Pakistan zilidai kuwa mashambulizi hayo yalisababisha vifo vya raia, akiwemo wanawake na watoto, na kuharibu misikiti na majengo mengine yasiyo ya kijeshi.

Pakistan Yajibu kwa Hasira

Baada ya mashambulizi hayo, Pakistan haikusita kujibu. Jeshi la nchi hiyo lililipa kisasi kwa kushambulia maeneo ya mpaka wa Line of Control (LoC) yanayodhibitwa na serikali ya India kwa mizinga, na kusababisha vifo vya raia watatu wa India. Kwa upande mwingine, Pakistan ilidai kuwa imefanikiwa kuangusha ndege kadhaa za kivita za India, zikiwemo aina ya Rafale, Sukhoi Su-30, na MiG-29, pamoja na ndege isiyo na rubani. India ilikubali kupoteza ndege tatu lakini ilikanusha ukubwa wa madai ya Pakistan.

Wakati huo huo, serikali ya Pakistan iliita mashambulizi ya India kuwa ni "kitendo cha vita" na kuomba Umoja wa Mataifa kuingilia kati haraka.

Kwa wasiojua labda maana ya Line of Control, huu ni mpaka uliotengwa kutenganisha mamlaka mbili zinazotawala eneo la Kashmir zisiingiliane kiutawala, yani wewe tamba mpaka hatua hizi, nami nitambe hatua hizi. Ikumbukwe eneo la Kashmir ni eneo linalopiganiwa na Nchi mbili. Na hakuna mmiliki rasmi wa eneo hilo. Lakini mamlaka ziliamua kukata katikati na kutenganisha ardhi kwa kila Nchi na eneo la upande wa kaskazini likipewa msaada na uongozi na msaada wa kijeshi chini ya serikali ya Pakistan na eneo la kusini likipokea misaada na uongozi chini ya serikali ya India. Hili kuondoa muingiliano wa kiuongozi, wakaweka mstari unaoonesha mipaka ya kila uongozi unapoishia ambapo ndipo mpaka huo ukaitwa jina la Line Of Control (LoC), ambapo utakiwi kuvuka mstari kwenda kwa mwenzako, kwa namna yoyote iwe kijeshi au kiutawala. Lakini mstari huu sio Mpaka rasmi wa Nchi na Nchi, ni zuio tu la kukataza tawala mbili zisiingiliane kwenye eneo moja, kwa sababu eneo hilo bado linapiganiwa na Nchi mbili, japo China nae anadai kipande kidogo cha ardhi katika eneo hilo hilo. Na kuna kipindi China na India walitunishiana vifua, kila mmoja kuonesha ubabe wake. Picha hapo chini inaonesha maeneo hayo yenye mgogoro wa ardhi.

Ulimwengu Washangazwa, Wakati Hatari Ikiendelea Kuongezeka

Jamii ya kimataifa ilionyesha hofu kubwa kuhusu hali hiyo. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, alitoa wito wa kujizuia kwa hali ya juu kutoka kwa mataifa yote mawili. Marekani pia iliwasihi India na Pakistan kushiriki mazungumzo badala ya kuendeleza mgogoro. Kutokana na ukweli kwamba mataifa haya mawili yana silaha za nyuklia, hali ya hofu ilienea kote ulimwenguni, ikionyesha hatari ya vita kubwa zaidi.

Historia ya Mgogoro wa Kashmir

Kashmir imekuwa chanzo cha mvutano kati ya India na Pakistan tangu mwaka 1947, baada ya mgawanyiko wa India ya Uingereza. Eneo hili limekuwa likishuhudia vita mara kwa mara, mashambulizi ya kigaidi, na mapigano madogo madogo kati ya majeshi ya nchi hizi mbili. Matukio ya sasa yanafuatia mfululizo wa migogoro inayochochewa na shambulio moja au jingine la kigaidi au kiaskari. Ikumbukwe kuwa India na Pakistan zilikuwa ni eneo moja au kwa lugha rahisi zilikuwa ni Nchi moja iliyokuwa chini ya Miliki ya Koloni la Mwingereza. Mwaka 1947, tarehe 14 Agosti. Siku moja kabla ya Uhuru wa India kutoka kwa Muingereza, Pakistan ilifanikiwa kujitenga na kutengeneza Taifa lake la Pakistan ambapo pia baadae mwaka 1971 Pakistan kwa mara nyingine iligawanyika na kuzaa mataifa mawili, yani Taifa la Pakistan ambalo pia liliitwa Western Pakistan na Taifa la Bangladesh lililokuwa likiitwa Eastern Pakistan huku Taifa mama likiwa ni India. Kisababishi kikuu cha Pakistan kudai uhuru wake kutoka kwa India ni kwa Sababu ya Itikadi za Kidini, maeneo wanayoishi wapakistani na wabangladeshi wa leo yalikuwa yana waumini wengi wa dini ya Kiislamu, huku maeneo ya India yakikaliwa na wakazi wa dini ya Kihindu. Utofauti huu wa kiitikadi za kidini ambao uliathiri maamuzi ya kisiasa ulipelekea Pakistan kujitenga kutoka kwa India na kudai uhuru na kutengeneza taifa lake rasmi la Pakistan (Western Pakistan na Eastern Pakistan ambayo ndio Bangladesh). Sasa wakati wa kujitenga kuna maeneo ambayo ilikuwa ni ngumu kuyatengenisha na moja wapo ni eneo hili la Kashmir. Ambalo Nchi tatu ikiwemo Pakistan na India kama mahasimu wakuu na China kwa mbali wakitaka kusimika utawala kwenye eneo hili ambalo linapatikana kwenye Milima ya Nepal, unapopatikana mlima Everest.

Sasa baada ya India na Pakistan kupewa uhuru na kuwa Nchi huru, eneo la Kashmiri na maeneo jirani yalikuwa bado hayajakabidhiwa kwa nchi zilizopata uhuru. Waingereza wakazungumza na viongozi wa eneo la Kashmir na kuwapa machaguo matatu, ambayo ni wachague kujiunga na Nchi ya Pakistan, au wajiunge na Nchi ya India au wapewe Uhuru wao binafsi hili wawe Nchi huru kama nchi nyingine wajitegemee kila kitu. Viongozi wa eneo la Kashmir wakataka wapewe Uhuru hili wajitawale kama Nchi uhuru. Ambapo Waingereza wakaridhia, lakini baadae Wanamgambo wa kikabila waliokuwa na ushirikiano na Jeshi la Pakistan walivamia eneo hilo na kutaka liwe chini ya utawala wa serikali ya Pakistan. Baada ya vurugu za hapa na pale viongozi wa Kashmir wakaona hapa hatuwawezi hawa wanamgambo wa Pakistan, hivyo wakaenda kuomba msaada wa kijeshi na Silaha za kivita kutoka serikali ya India, ambapo wakasaini mkataba na Jeshi la India kwenda kusaidia Uongozi au Utawala wa eneo la Kashmir na eneo kwa ujumla lisichukuliwe na wanamgambo wa Pakistan. India ikaingilia kati na kichapo kikaanza, ambapo mpaka leo hii eneo hilo halijapata mmiliki halali. India ikiishutumu Pakistan kwa matukio ya kigaidi eneo hilo, huku India ikishutumiwa kwa kufanya mashambulizi ya kushitukiza katika ardhi ya Pakistan.

Mustakabali wa Mgogoro

Hali bado ni tete. Mataifa yote mawili yako katika hali ya tahadhari kubwa, huku juhudi za kidiplomasia zikiendelea kuzuia hali kuzorota zaidi. Ingawa wito wa mazungumzo umekuwa ukitolewa, njia ya kufikia suluhu bado ni ngumu na yenye changamoto nyingi.

Kwa ulimwengu, hili ni somo kwamba amani ni jambo la thamani linalopaswa kulindwa kwa juhudi za pamoja. Mashariki ya Kusini mwa Asia inasimama kwenye ukingo wa mabadiliko makubwa, lakini swali ni, je, amani itapata nafasi?

View attachment 3326669
Mkuu swari la kizushi, Wapakistan ni Waarab au Wahindi?

Asante
 
Wapakistan si Waarabu wala si Wahindi, lakini wanahusiana kihistoria na Wahindi. Pakistan ni nchi inayopatikana Kusini mwa Asia, na watu wake wengi ni Waindo-Waariani kwa kimombo wanaitwa "Indo-Aryans", ambao ni jamii inayohusiana na Wahindi wa Kaskazini kwa lugha na asili ya kikabila.

Kihistoria, Pakistan ilikuwa sehemu ya eneo la Nchi ya India kabla ya kugawanyika mwaka 1947. Hii ilitokea wakati wa uhuru wa India kutoka kwa Uingereza, ambapo Pakistan ilianzishwa kama taifa la Kiislamu ili kuhifadhi maslahi ya Waislamu wa eneo hilo.

Kuna mchanganyiko wa tamaduni, lakini watu wa Pakistan wengi wao wanatoka katika makabila kama Wapunjabi, Wapashtun, Wasindhi, na Wabaluch. Lugha rasmi ni Kiurdu, ambayo ina uhusiano wa karibu na Kihindi. Kiasili, dini kuu ni Uislamu, jambo ambalo linaifanya nchi hiyo kuwa tofauti zaidi na Wahindi wengi ambao ni Wahindu au Wabudha.
 
Ningekuwa na nguvu duniani ningetoa maelekezo kuwa Kashmir iwe nchi inayojitegemea,yeyote atakayebisha kati ya India na Pakistan atapata kipigo cha mbwa koko
 
Ipi sababu ya East pakistan kujitenga na west pakistan mpaka kuwa Bangladesh? Je walipigana vita?
 
Sasa umenitoa tongotongo. Shukran
 
Muammar Gaddafi kaingia madarakani baada ya kumpindua Mfalme Idris Septemba mwaka 1969. Mwaka 1948 alikuwa mdogo sana. Yasser Arafat kazaliwa 1929, mwaka 1948 alikuwa Ana miaka 19.

Hivyo unaposema ni ubaguzi wa waarabu ndio uliwakimbiza mayahudi kutoka nchi zao wakakimbilia "Israel" mwaka 1948, tena eti kwa ubaguzi wa waarabu kuchochewa na viongozi wao wabovu kisha ukawataja kama eti Gaddafi na Arafat, inaonesha ima hujui au unakwepesha ukweli makusudi, au huelewi kabisa unachokisema.

Halafu kwanini mayahudi waliishi kwa amani mashariki ya kati na waarabu mpaka walipokuja mayahudi wazungu kutoka Ulaya waliowakimbia ndugu zao wakristo waliokuwa wakiwatesa na kuwaua, wakakimbilia mashariki ya kati wakidai ni kwao ndio mayahudi wa mashariki ya kati wakaanza kukimbilia nchi ya kizayuni?

Halafu katika ardhi ya Palestine kabla mayahudi hawajaanza kuhamia, mayahudi waliokuwepo pale wenyeji mpaka karne ya 19 walikuwa ni wachache. Wengine wengi ni wahamiaji pale.
Unajadiliana na tutusa hapo😂😂😂.
Anaropokaga tu huyo jamaa.
 
Wapakistan si Waarabu wala si Wahindi, lakini wanahusiana kihistoria na Wahindi. Pakistan ni nchi inayopatikana Kusini mwa Asia, na watu wake wengi ni Waindo-Waariani kwa kimombo wanaitwa "Indo-Aryans", ambao ni jamii inayohusiana na Wahindi wa Kaskazini kwa lugha na asili ya kikabila.

Kihistoria, Pakistan ilikuwa sehemu ya eneo la Nchi ya India kabla ya kugawanyika mwaka 1947. Hii ilitokea wakati wa uhuru wa India kutoka kwa Uingereza, ambapo Pakistan ilianzishwa kama taifa la Kiislamu ili kuhifadhi maslahi ya Waislamu wa eneo hilo.

Kuna mchanganyiko wa tamaduni, lakini watu wa Pakistan wengi wao wanatoka katika makabila kama Wapunjabi, Wapashtun, Wasindhi, na Wabaluch. Lugha rasmi ni Kiurdu, ambayo ina uhusiano wa karibu na Kihindi. Kiasili, dini kuu ni Uislamu, jambo ambalo linaifanya nchi hiyo kuwa tofauti zaidi na Wahindi wengi ambao ni Wahindu au Wabudha.
Pakistani ethnically ni Persians sio Arabians.
 
Mwezi wa huu wa Mei mwaka 2025, ulimwengu umetikiswa na mgogoro mpya kati ya mataifa mawili yenye historia ndefu ya mvutano – India na Pakistan. Tarehe 6 Mei, India ilitangaza operesheni kali iliyobeba jina "Operation Sindoor," ikilenga maeneo tisa ndani ya Pakistan na kipande cha eneo la Kashmir linaloendeshwa au kudhibitiwa na serikali ya Pakistan. Hii ilikuwa hatua ya kulipiza kisasi kufuatia shambulio baya la kigaidi lililotokea tarehe 22 Aprili 2025 katika eneo la Pahalgam, katika mji wa Kashmir, ambapo watu 26, wengi wao wakiwa watalii wa Kihindu, walipoteza maisha.

India iliamua kuchukua hatua kali dhidi ya makundi ya kigaidi kama Lashkar-e-Taiba na kundi la Jaish-e-Mohammed, yaliyoshutumiwa kwa kupanga mashambulizi hayo ambayo yaliua watu 26 katika mji huo. Ambapo Mashambulizi ya anga na makombora yalifanyika kwa lengo la kuharibu miundombinu ya kigaidi. Wizara ya Ulinzi ya India ilieleza kwamba operesheni hiyo ilikuwa "imepangwa kwa uangalifu, isiyolenga kusababisha vita vikubwa." Hata hivyo, taarifa kutoka Pakistan zilidai kuwa mashambulizi hayo yalisababisha vifo vya raia, akiwemo wanawake na watoto, na kuharibu misikiti na majengo mengine yasiyo ya kijeshi.

Pakistan Yajibu kwa Hasira

Baada ya mashambulizi hayo, Pakistan haikusita kujibu. Jeshi la nchi hiyo lililipa kisasi kwa kushambulia maeneo ya mpaka wa Line of Control (LoC) yanayodhibitwa na serikali ya India kwa mizinga, na kusababisha vifo vya raia watatu wa India. Kwa upande mwingine, Pakistan ilidai kuwa imefanikiwa kuangusha ndege kadhaa za kivita za India, zikiwemo aina ya Rafale, Sukhoi Su-30, na MiG-29, pamoja na ndege isiyo na rubani. India ilikubali kupoteza ndege tatu lakini ilikanusha ukubwa wa madai ya Pakistan.

Wakati huo huo, serikali ya Pakistan iliita mashambulizi ya India kuwa ni "kitendo cha vita" na kuomba Umoja wa Mataifa kuingilia kati haraka.

Kwa wasiojua labda maana ya Line of Control, huu ni mpaka uliotengwa kutenganisha mamlaka mbili zinazotawala eneo la Kashmir zisiingiliane kiutawala, yani wewe tamba mpaka hatua hizi, nami nitambe hatua hizi. Ikumbukwe eneo la Kashmir ni eneo linalopiganiwa na Nchi mbili. Na hakuna mmiliki rasmi wa eneo hilo. Lakini mamlaka ziliamua kukata katikati na kutenganisha ardhi kwa kila Nchi na eneo la upande wa kaskazini likipewa msaada na uongozi na msaada wa kijeshi chini ya serikali ya Pakistan na eneo la kusini likipokea misaada na uongozi chini ya serikali ya India. Hili kuondoa muingiliano wa kiuongozi, wakaweka mstari unaoonesha mipaka ya kila uongozi unapoishia ambapo ndipo mpaka huo ukaitwa jina la Line Of Control (LoC), ambapo utakiwi kuvuka mstari kwenda kwa mwenzako, kwa namna yoyote iwe kijeshi au kiutawala. Lakini mstari huu sio Mpaka rasmi wa Nchi na Nchi, ni zuio tu la kukataza tawala mbili zisiingiliane kwenye eneo moja, kwa sababu eneo hilo bado linapiganiwa na Nchi mbili, japo China nae anadai kipande kidogo cha ardhi katika eneo hilo hilo. Na kuna kipindi China na India walitunishiana vifua, kila mmoja kuonesha ubabe wake. Picha hapo chini inaonesha maeneo hayo yenye mgogoro wa ardhi.

Ulimwengu Washangazwa, Wakati Hatari Ikiendelea Kuongezeka

Jamii ya kimataifa ilionyesha hofu kubwa kuhusu hali hiyo. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, alitoa wito wa kujizuia kwa hali ya juu kutoka kwa mataifa yote mawili. Marekani pia iliwasihi India na Pakistan kushiriki mazungumzo badala ya kuendeleza mgogoro. Kutokana na ukweli kwamba mataifa haya mawili yana silaha za nyuklia, hali ya hofu ilienea kote ulimwenguni, ikionyesha hatari ya vita kubwa zaidi.

Historia ya Mgogoro wa Kashmir

Kashmir imekuwa chanzo cha mvutano kati ya India na Pakistan tangu mwaka 1947, baada ya mgawanyiko wa India ya Uingereza. Eneo hili limekuwa likishuhudia vita mara kwa mara, mashambulizi ya kigaidi, na mapigano madogo madogo kati ya majeshi ya nchi hizi mbili. Matukio ya sasa yanafuatia mfululizo wa migogoro inayochochewa na shambulio moja au jingine la kigaidi au kiaskari. Ikumbukwe kuwa India na Pakistan zilikuwa ni eneo moja au kwa lugha rahisi zilikuwa ni Nchi moja iliyokuwa chini ya Miliki ya Koloni la Mwingereza. Mwaka 1947, tarehe 14 Agosti. Siku moja kabla ya Uhuru wa India kutoka kwa Muingereza, Pakistan ilifanikiwa kujitenga na kutengeneza Taifa lake la Pakistan ambapo pia baadae mwaka 1971 Pakistan kwa mara nyingine iligawanyika na kuzaa mataifa mawili, yani Taifa la Pakistan ambalo pia liliitwa Western Pakistan na Taifa la Bangladesh lililokuwa likiitwa Eastern Pakistan huku Taifa mama likiwa ni India. Kisababishi kikuu cha Pakistan kudai uhuru wake kutoka kwa India ni kwa Sababu ya Itikadi za Kidini, maeneo wanayoishi wapakistani na wabangladeshi wa leo yalikuwa yana waumini wengi wa dini ya Kiislamu, huku maeneo ya India yakikaliwa na wakazi wa dini ya Kihindu. Utofauti huu wa kiitikadi za kidini ambao uliathiri maamuzi ya kisiasa ulipelekea Pakistan kujitenga kutoka kwa India na kudai uhuru na kutengeneza taifa lake rasmi la Pakistan (Western Pakistan na Eastern Pakistan ambayo ndio Bangladesh). Sasa wakati wa kujitenga kuna maeneo ambayo ilikuwa ni ngumu kuyatengenisha na moja wapo ni eneo hili la Kashmir. Ambalo Nchi tatu ikiwemo Pakistan na India kama mahasimu wakuu na China kwa mbali wakitaka kusimika utawala kwenye eneo hili ambalo linapatikana kwenye Milima ya Nepal, unapopatikana mlima Everest.

Sasa baada ya India na Pakistan kupewa uhuru na kuwa Nchi huru, eneo la Kashmiri na maeneo jirani yalikuwa bado hayajakabidhiwa kwa nchi zilizopata uhuru. Waingereza wakazungumza na viongozi wa eneo la Kashmir na kuwapa machaguo matatu, ambayo ni wachague kujiunga na Nchi ya Pakistan, au wajiunge na Nchi ya India au wapewe Uhuru wao binafsi hili wawe Nchi huru kama nchi nyingine wajitegemee kila kitu. Viongozi wa eneo la Kashmir wakataka wapewe Uhuru hili wajitawale kama Nchi uhuru. Ambapo Waingereza wakaridhia, lakini baadae Wanamgambo wa kikabila waliokuwa na ushirikiano na Jeshi la Pakistan walivamia eneo hilo na kutaka liwe chini ya utawala wa serikali ya Pakistan. Baada ya vurugu za hapa na pale viongozi wa Kashmir wakaona hapa hatuwawezi hawa wanamgambo wa Pakistan, hivyo wakaenda kuomba msaada wa kijeshi na Silaha za kivita kutoka serikali ya India, ambapo wakasaini mkataba na Jeshi la India kwenda kusaidia Uongozi au Utawala wa eneo la Kashmir na eneo kwa ujumla lisichukuliwe na wanamgambo wa Pakistan. India ikaingilia kati na kichapo kikaanza, ambapo mpaka leo hii eneo hilo halijapata mmiliki halali. India ikiishutumu Pakistan kwa matukio ya kigaidi eneo hilo, huku India ikishutumiwa kwa kufanya mashambulizi ya kushitukiza katika ardhi ya Pakistan.

Mustakabali wa Mgogoro

Hali bado ni tete. Mataifa yote mawili yako katika hali ya tahadhari kubwa, huku juhudi za kidiplomasia zikiendelea kuzuia hali kuzorota zaidi. Ingawa wito wa mazungumzo umekuwa ukitolewa, njia ya kufikia suluhu bado ni ngumu na yenye changamoto nyingi.

Kwa ulimwengu, hili ni somo kwamba amani ni jambo la thamani linalopaswa kulindwa kwa juhudi za pamoja. Mashariki ya Kusini mwa Asia inasimama kwenye ukingo wa mabadiliko makubwa, lakini swali ni, je, amani itapata nafasi?

View attachment 3326669
Pia usisahau pamoja na India kuwa taifa lenye idadi kubwa ya Waislamu kuliko nchi nyingine yoyote lakini ni wachache ukifanananisha na Mabaniani (Hindus,) wakati Pakistan ni Waislamu ,99%=kuna element ya udini. Waislamu wa India ni second class citizens wakikutwa wanakula nyama ya ng'ombe huuwawa.
 
Wapakistan si Waarabu wala si Wahindi, lakini wanahusiana kihistoria na Wahindi. Pakistan ni nchi inayopatikana Kusini mwa Asia, na watu wake wengi ni Waindo-Waariani kwa kimombo wanaitwa "Indo-Aryans", ambao ni jamii inayohusiana na Wahindi wa Kaskazini kwa lugha na asili ya kikabila.

Kihistoria, Pakistan ilikuwa sehemu ya eneo la Nchi ya India kabla ya kugawanyika mwaka 1947. Hii ilitokea wakati wa uhuru wa India kutoka kwa Uingereza, ambapo Pakistan ilianzishwa kama taifa la Kiislamu ili kuhifadhi maslahi ya Waislamu wa eneo hilo.

Kuna mchanganyiko wa tamaduni, lakini watu wa Pakistan wengi wao wanatoka katika makabila kama Wapunjabi, Wapashtun, Wasindhi, na Wabaluch. Lugha rasmi ni Kiurdu, ambayo ina uhusiano wa karibu na Kihindi. Kiasili, dini kuu ni Uislamu, jambo ambalo linaifanya nchi hiyo kuwa tofauti zaidi na Wahindi wengi ambao ni Wahindu au Wabudha.
nje ya mada. ilikuaje mpaka Wamagharibi wakawaacha Pakistan na India kumilikia nyuklia? maana wamagharibi na wamarekani huwa hawataki nchi zingine wamiliki. nipe ufafanuzi mkuu..
 
Akil zako ni sifuri , mwanzo hayo maeneo yalikuwa ndan ya dola moja la Muingereza kama ilivyo Palestine ilikuwa ndan ya Uingereza .

India iliundwa na wahindu na waislamu kama ilivyo Palestine iliundwa na Waislam , Wayaud na wakristu

Baada ya uhuru mwaka 1947 India iligawanywa kuwa India na Pakistan ( Pakistan iliundwa na West Pakistan = today Pakistan na East Pakistan = today Bangladesh )

Pia baada ya uhuru mwaka 1948 Palestine iligawanywa na kuunda Israel na Palestine ( Today Gaza + West Bank ).

Kitu watu wengi hawajui Palestine ilipiganiwa sana na wayaudi na sio waaranbu ( leo wanajiita wapalestina ) pia Wayaud walikwepo wengi sana kwenye nchi za kiarabu kabl ya mwaka 1948 hasa Palestine ila ubaguz wa waarab uliochochewa na viongoz wao wabovu mf Arafat na Gadaf ndo ilipeleka wayaud kukimbia nchi za kiarab na kwenda Israel , pia wayaud walioletwa mwaka 1948 ni wachache sana kulinganisha na waliokwepo hapo awali
kwahyo ww ndo umejiona una akili hapokuwa taifa Moja kabla sio sababu umbali uliopo Leo hii Tanzania ikitoka vipande vitatu Mwanza na mtwara kuwa nchi Moja ngumu kutokana katikati Kuna ncho ya Dodoma na ndo mdau alichotaka kueleweshw ilikuwaje wakawa nchi Moja na umbali ulishawatenganisha walitakiwa waunde nchi Yao walivyopewa TU uhuru na waingereza
 
Pakistan na India ilikuwa ni Nchi moja... kwa sababu Bangladeshi na Pakistan zilikuwa na Waislamu wengi, itikadi za kidini ndio zilifanya wajitenge... na kwa sababu wote walikuwa Waislamu na walikuwa na mlengo mmoja kwenye vitu vingi ikabidi haya maeneo yote yaliyojitenga na India yenye Waislamu wengi wayaite Pakistani kutokana na Itikadi za kidini na kupanua wigo wa Nchi ya Pakistan izidi kuwa kubwa... badae ndipo Bangladesh wakajitoa kwenye umoja huo ambapo kabla walikuwa wanaitwa East Pakistan na kutengeneza Nchi yao binafsi.

Kuwa na umbali au kutenganishwa na Nchi nyingine katika hoja... Mbona Wakoloni waliweza kutawala Nchi nyingi zisizoungana, mbona Marekani na Alaska ni Nchi moja ila inatenganishwa na Canada...

Inawezekana vizuri tu, hata Tanzania na Lesotho zinaweza kuwa Nchi moja japo hazijaungana kijografia
 
Back
Top Bottom