Chanzo cha vita ya India na Pakistan inayoendelea hivi leo katika eneo la Kashmir


Muammar Gaddafi kaingia madarakani baada ya kumpindua Mfalme Idris Septemba mwaka 1969. Mwaka 1948 alikuwa mdogo sana. Yasser Arafat kazaliwa 1929, mwaka 1948 alikuwa Ana miaka 19.

Hivyo unaposema ni ubaguzi wa waarabu ndio uliwakimbiza mayahudi kutoka nchi zao wakakimbilia "Israel" mwaka 1948, tena eti kwa ubaguzi wa waarabu kuchochewa na viongozi wao wabovu kisha ukawataja kama eti Gaddafi na Arafat, inaonesha ima hujui au unakwepesha ukweli makusudi, au huelewi kabisa unachokisema.

Halafu kwanini mayahudi waliishi kwa amani mashariki ya kati na waarabu mpaka walipokuja mayahudi wazungu kutoka Ulaya waliowakimbia ndugu zao wakristo waliokuwa wakiwatesa na kuwaua, wakakimbilia mashariki ya kati wakidai ni kwao ndio mayahudi wa mashariki ya kati wakaanza kukimbilia nchi ya kizayuni?

Halafu katika ardhi ya Palestine kabla mayahudi hawajaanza kuhamia, mayahudi waliokuwepo pale wenyeji mpaka karne ya 19 walikuwa ni wachache. Wengine wengi ni wahamiaji pale.
 
Kitu watu wengi hawajui Palestine ilipiganiwa sana na wayaudi na sio waaranbu ( leo wanajiita wapalestina )
Kuipigania kivipi? Kuanzia lini? Walichofanya walikuja pale wakasema ni kwao, baada ya waliotoka Ulaya huko ambapo walikuwa wakiteswa wakakimbilia pale na kudai ni kwao.
 
Soma tena historia ya Mgogoro Israel na Palestina halafu ondoa issue ya dini
 
Eneo ilo india ana maadui wengi sana ikiwemo China, pigo la kwanza tu India ime pata lose tayari Na kwenye hii vita atakae umia zaidi ni India
.

View: https://x.com/clashreport/status/1920123876341645475
 
Mkuu swari la kizushi, Wapakistan ni Waarab au Wahindi?

Asante
 
Mkuu swari la kizushi, Wapakistan ni Waarab au Wahindi?

Asante
Wapakistan si Waarabu wala si Wahindi, lakini wanahusiana kihistoria na Wahindi. Pakistan ni nchi inayopatikana Kusini mwa Asia, na watu wake wengi ni Waindo-Waariani kwa kimombo wanaitwa "Indo-Aryans", ambao ni jamii inayohusiana na Wahindi wa Kaskazini kwa lugha na asili ya kikabila.

Kihistoria, Pakistan ilikuwa sehemu ya eneo la Nchi ya India kabla ya kugawanyika mwaka 1947. Hii ilitokea wakati wa uhuru wa India kutoka kwa Uingereza, ambapo Pakistan ilianzishwa kama taifa la Kiislamu ili kuhifadhi maslahi ya Waislamu wa eneo hilo.

Kuna mchanganyiko wa tamaduni, lakini watu wa Pakistan wengi wao wanatoka katika makabila kama Wapunjabi, Wapashtun, Wasindhi, na Wabaluch. Lugha rasmi ni Kiurdu, ambayo ina uhusiano wa karibu na Kihindi. Kiasili, dini kuu ni Uislamu, jambo ambalo linaifanya nchi hiyo kuwa tofauti zaidi na Wahindi wengi ambao ni Wahindu au Wabudha.
 
Ningekuwa na nguvu duniani ningetoa maelekezo kuwa Kashmir iwe nchi inayojitegemea,yeyote atakayebisha kati ya India na Pakistan atapata kipigo cha mbwa koko
 
Ipi sababu ya East pakistan kujitenga na west pakistan mpaka kuwa Bangladesh? Je walipigana vita?
 
Sasa umenitoa tongotongo. Shukran
 
Unajadiliana na tutusa hapo😂😂😂.
Anaropokaga tu huyo jamaa.
 
Pakistani ethnically ni Persians sio Arabians.
 
Pia usisahau pamoja na India kuwa taifa lenye idadi kubwa ya Waislamu kuliko nchi nyingine yoyote lakini ni wachache ukifanananisha na Mabaniani (Hindus,) wakati Pakistan ni Waislamu ,99%=kuna element ya udini. Waislamu wa India ni second class citizens wakikutwa wanakula nyama ya ng'ombe huuwawa.
 
nje ya mada. ilikuaje mpaka Wamagharibi wakawaacha Pakistan na India kumilikia nyuklia? maana wamagharibi na wamarekani huwa hawataki nchi zingine wamiliki. nipe ufafanuzi mkuu..
 
kwahyo ww ndo umejiona una akili hapokuwa taifa Moja kabla sio sababu umbali uliopo Leo hii Tanzania ikitoka vipande vitatu Mwanza na mtwara kuwa nchi Moja ngumu kutokana katikati Kuna ncho ya Dodoma na ndo mdau alichotaka kueleweshw ilikuwaje wakawa nchi Moja na umbali ulishawatenganisha walitakiwa waunde nchi Yao walivyopewa TU uhuru na waingereza
 
Pakistan na India ilikuwa ni Nchi moja... kwa sababu Bangladeshi na Pakistan zilikuwa na Waislamu wengi, itikadi za kidini ndio zilifanya wajitenge... na kwa sababu wote walikuwa Waislamu na walikuwa na mlengo mmoja kwenye vitu vingi ikabidi haya maeneo yote yaliyojitenga na India yenye Waislamu wengi wayaite Pakistani kutokana na Itikadi za kidini na kupanua wigo wa Nchi ya Pakistan izidi kuwa kubwa... badae ndipo Bangladesh wakajitoa kwenye umoja huo ambapo kabla walikuwa wanaitwa East Pakistan na kutengeneza Nchi yao binafsi.

Kuwa na umbali au kutenganishwa na Nchi nyingine katika hoja... Mbona Wakoloni waliweza kutawala Nchi nyingi zisizoungana, mbona Marekani na Alaska ni Nchi moja ila inatenganishwa na Canada...

Inawezekana vizuri tu, hata Tanzania na Lesotho zinaweza kuwa Nchi moja japo hazijaungana kijografia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…