Hivi huna cha kuandika?????? Kenya imegawanyika kuna mwambao wa pwani ambapo sherehe zao zinaambatana na aina ya vyakula ambavyo nina uhakika hata wabongo wengi ukiondoa Tanga na Unguja hawavifahamu. Kwenye mikoa ya kati hasa Nairobi, inategemea unaenda kwenye sherehe ya aina gani kwani kwa wenye nazo hasa Nbi siku hizi kuna vyakula vya ki thai na vyenginevyo ambavyo hata huku kwetu ni nadra sana kuviona kwenye sherehe. Mikoa ya Magharibi, wengi wao ni wale wanaotukuza vyakula vya mila zao pamoja na pilau,chapatii, maandasi kwa kuku/nyama karanga.
Sioni sababu ya kubeza vyakula vya wenzenu wakati hata huku kwetu mikoani
vyakula vya kimila vinachanganywa na vile vya pwani kama milo kwenye sherehe.