Mkuu Kiranga hapo umewauwa...Kila kiumbe kinabadilika kulingana na mazingira, mfano bacteria na viruses (lower organisms) wanafanya evolution ya haraka kuliko binadamu(higher organisms).Ndio maana kuna aina ( strains) mbali mbali za hawa bacteria na viruses.Angali kitu kama HIV, kuna aina mbali mbali wa HIV, zamani kulikuwa na aina moja(Possibly) ya huyu kirusi lakini kutokana na kubadilika kwa mazingira anayoishi, DNA zake hubadilika(Evolution) ili aweze kuadapt kwenye mazingira mapya.....Kama mtu anasumbuliwa na ugonjwa unaosababishwa na bacteria au virus flani na kutumia dawa, kuna uwezekano wa yule mdudu kujibadili ili aweze kuishi kwenye mazingira yaliyobadilika(baada ya kutumia dawa) na hivyo kumlazimu mgonjwa kutumia dawa nyingine.Hii ndio sababu ya ugonjwa mmoja kuwa na dawa zaidi ya moja.
Lakini kwa kuwa hawa wafia dini wana viazi mbatata juu ya shingo, subiri kupewa jibu lililo nje ya swali au kuulizwa swali lililo nje ya mada.