Charles Darwin 3rd Degree MM aliefanikiwa kuupotosha ulimwengu kwa Illuminati agenda

Kwa kupigwa kwake sisi tumepona, yeye aliyachukua magonjwa yetu. Kwa mungu wa Ibrahim, Isack, na yakobo hakuna ukimw
Kama angechukua magonjwa yote kwa jinsi unavyodai, tusingekuwa na msamiati 'ugonjwa' maana tusingeyakuta wala kuyajua.
Halafu alipigwa kwa sababu ipi?
 
Nimefuatilia habari hizi toka mchango wa kwanza mpaka hapa naandika,

Binafsi sio muumini wa darwin lakini pamoja na mapungufu yote yaliyopo kwenye hii theory yake ya survive for fittest na ile ya Natural selection yote yanachunguzika kisayansi na nahisi sasa kwa mawazo yangu hii theory bora thus why hata hapa tunaipinga tena kwa kuwa na strong reason.

tukirudi upande wa pili ule wa creation hii kitu hatuwezi kuiprove wala kuichunguza na wote mliochangia hapo juu mmedai kuwa theory ya Darwin ni outdated kwa kuleta reasons za wanasayansi

sasa its very simple HEBU TUPENI USHAHID WA KISAYANSI KUHUSU HICHO NINYI MNACHOKIAMIN
 
Kama angechukua magonjwa yote kwa jinsi unavyodai, tusingekuwa na msamiati 'ugonjwa' maana tusingeyakuta wala kuyajua.
Halafu alipigwa kwa sababu ipi?
kama husivojua upepo utokako wala uendako, hivo hivo huwezi jua haya mambo, kwa akili ya kibinadamu
 
kama husivojua upepo utokako wala uendako, hivo hivo huwezi jua haya mambo, kwa akili ya kibinadamu
Una maanisha hadi leo hujui kwamba upepo ni hewa inayohama kutoka eneo moja kwenda eneo lingine kwa sababu za utofauti wa pressure?

Yaani mambo yaliyoandikwa kwenye vitabu vya kale bila ya kutafitiwa ndio mnayaleta kama reference?

Ni imani yangu kuwa unatania na haumaanishi.
 
Hujawahi fundishwa reality, unajitetea tu who proved it to you?
 
Hujawahi fundishwa reality, unajitetea tu who proved it to you?
We hili jambo umedhihirisha kuwa hulielewi,
Kumbe unajua kitu kinahitaji proof eeh?....sasa ni nani aliyethibitisha uwepo wa Mungu?
 
Katika mazingira ya maisha ya bacteria ni kweli kuishi kulingana na mazingira na hujibadirisha kukabiri hali yoyote iwapo itatokea.

Lakini kutokuamini uwepo wa Mungu ni uvivu wa kutokufikiri nautambuzi mazingira yetu kwa uhalisia.

Tatizo kubwa mtu yoyote asiyeweza kujitambua ktk uhalisia huwezi kuwa na uhakika wa Mungu!
 
We hili jambo umedhihirisha kuwa hulielewi,
Kumbe unajua kitu kinahitaji proof eeh?....sasa ni nani aliyethibitisha uwepo wa Mungu?
Uthibitisho wa uwepo wa Mungu hakuhitaji Shahada ya uelewa Ulimwengu na mpangilio wake ni thabiti tosha kuwepo kwa mpangaji wa mazingira kwa sahihi.
 
Hata wewe hujui chanzo cha upepo tunaongea siasa
Chanzo cha upepo ni miali ya Jua
 
Tatizo kubwa ni kuwa na wasomi wenye kuhangaikia njaa serikali za kiafrica hawako tayali kutenga budget kwa wasomi wao kutafta na kufanya utafiti.

Usiamini kila unachojifunza kuna hatua inakuwa siyo ya kukubali kila unacho kisoma lazima ukitafiti kujifunza usikubali kila jambo bila uhakika.

Science imetusaidia kufahamu mengi kwa ingawa kuna upptoshaji linapokuja suala linalo husu Binadamu kuna miradi mingi ya upotoshaji kwaajiri ya makundi flani kulinda maslahi yao yasiguswe.

Binafsi nimefanya utafiti kuhusu Dunia na Ulimwengu nikapata mwanga kuhusu hilo ni vigumu kunipotosha.

Nimefuga nyuki wakubwa na wadogo na kufanyia utafiti nikajifunza mengi.

Nimefuga nyani 2006-2008 nikajifunza kitu nimefunga Nguruwe, Bata, Kuku, Mbuzi, Sungura, na sasa Nimefuga samaki kambare na Nina endelea kujifunza.

Ni lazima ujifunze sio ukubali kila jambo
Jaribu kufanya kilicho ndani ya uwezo wako
 
Sentensi yako ya kwanza imekubali uwezekano wa evolution.

Kuamini uwepo wa Mungu bila ushahidi ni uvivu wa kufikiri maana imani kwa Mungu haina mantiki wala ushahidi.
Huwezi kuwa na uhakika wa Mungu pasipo ushahidi.
 
Uthibitisho wa uwepo wa Mungu hakuhitaji Shahada ya uelewa Ulimwengu na mpangilio wake ni thabiti tosha kuwepo kwa mpangaji wa mazingira kwa sahihi.
Mazingira ya ulimwenguni yamejaa tabu, maovu, majanga asilia n.k, Kama Mungu ana upendo wote, uweza na ujuzi wote, kwa nini amuumbie Mtu mazingira hatari kama haya?....unazungumziaje kuhusu mafuriko, milipuko ya volkano, vimbunga na matetemeko ya nchi?
 
Sentensi yako ya kwanza imekubali uwezekano wa evolution.

Kuamini uwepo wa Mungu bila ushahidi ni uvivu wa kufikiri maana imani kwa Mungu haina mantiki wala ushahidi.
Huwezi kuwa na uhakika wa Mungu pasipo ushahidi.
Ushahidi wa kuwepo kwa Mungu ni maisha yetu na uhai ni uthibitisho tosha kuamini uwepo Mungu
 
Kufa ni faida, Mungu alifanya kama alivyoona inafaa hapangiwi utaratibu wa nini kifanyike,
Hayo uyaonayo ni utiisho wake na kazi ya mikono yake.
 
Kufa ni faida, Mungu alifanya kama alivyoona inafaa hapangiwi utaratibu wa nini kifanyike,
Hayo uyaonayo ni utiisho wake na kazi ya mikono yake.
Hivi wewe si ndiye yule uliyefanya utafiti wa miaka 16 kugundua makazi ya Mungu?
Kama ni hivyo nitakuwa napoteza energy bure kulumbana na wewe.
 
Hivi wewe si ndiye yule uliyefanya utafiti wa miaka 16 kugundua makazi ya Mungu?
Kama ni hivyo nitakuwa napoteza energy bure kulumbana na wewe.
Nimependa sana hiyo statement yako ya mwisho kwamba unapoteza energy bure kulumbana.

Ingetakiwa ujue hili swala tokea mwanzo naona umechelewa sana Kiranga kiongozi wenu alishagundua na ndio mana amefutika JF.
 
Kiranga ni kiongozi wetu kwa lipi?

Una uhakika kwamba Kiranga amefutika JF au ni kwamba humuoni?

Kauli yangu ya kwamba napoteza muda kulumbana na huyo mtu siyo kwamba mada ndiyo inapoteza energy bali ni huyo impongo.
Amejawa na myths badala ya facts, imagine mtu amefanya utafiti wa miaka 16 kugundua makazi ya Mungu,....Hivi mtu wa hivyo unamuweka kwenye kundi lipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…