Charles Kitwanga atajwa kuhusika na kashfa ya ufisadi katika Jeshi la Polisi ya sh. bilioni 34

Status
Not open for further replies.
Tafuta gazeti la Leo utajua kila ktu.
 

Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1460283600.720510.jpg
    275.7 KB · Views: 42
Tunafahamu ukaribu wake na mkuu mwenyewe, jee alipewa wizara hiyo ili aje afiche madhambi ya nyuma?
Magu kweli hii bita ya ufisadi ataiweza kweli maana inaonyesha hakuna atakaye baki
Hawa mawaziri wote Magu alipangiwa na kina JK sasa magu anawavua nguo hadharani taratibu, watajiweka pembeni wao wenyewe na hiyo kazi watajutia kwanini walikubali
 
Daaah! Kama Magufuli akiamua kuwashughulikia wanao haribu lugha ya Kiswahili, wewe utakuwa jipu lingine. Yani Kiswahili chako ni jipu uchungu
 
Kama ni kweli na Nchi hii ingekuwa ina simama katika uadilifu na kwa unyeti wa Wizara anayo simamia huyu mheshimiwa asinge stahili hata kumaliza nusu saa katika hiyo wizara yeye na huyo partner wake kibiashara ambaye hata hivyo sina hakika kama ni coincidence kufanya naye kazi tena chini ya Wizara yake,nasema kama ni kweli,natu subiri.
 
Hahahah Magufuli alifikiri ni rahisi!!! Its not easy!!!!!!
Nchi hii kila mtu ni mchafu hakuna wa kumsafisha mwenzake....ni vituko tu,change utamkuta eti anachaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya maadili hehehe
Masolex naye tunaambiwa aliuza nyumba za serikali...kuna mwana Jf mmoja alisema Tanzania hata akipewa ibilisi atachemsha kuongoza
 
Mkichunguza sana wale wanaopiga kelele sana hadi povu ni wale wanaonufaika na mfumo mbovu uliopo wa fisiem. Arafu wanasema hapa kazi! Kazi ndio hiyo kupiga Mali za nchi
 
Halafu nasikia ama ni wachungaji au wanamiliki makanisa hapa jijini ???. Daah! Niliona hata Bwana Saliboko ( RITA ) nae ni mchungaji.
 
KAMA RAIS KWELI NI MZALENDO, HUYU BWANA ILITAKIWA HASIWEPO WIZARANI. MAANA ENZI ZA MWALIMU UKISEMWA SEMWATU OUT.
 
Kwa kumbukumbu tu ndani ya Wizara hii hii nyeti miaka ya 70 enzi za uadilifu aliye kuwa Mkuu wa jeshi la Polisi Marehemu Mzee Hamza Aziz ali jiuzulu wadhfa wake kwa kumgonga mtu katika ajali ya gari,na ni katika Wizara hii hii Rais mstaafu Mzee Mwinyi ali jiuzulu kwa uwajibikaji kwa makosa ya walio chini yake tu, Hebu tu tafakari katika nchi hii na katika miaka hii yame tokea mangapi yanayo wagusa viongozi wetu kuanzia mawaziri mpaka wakurugenzi je yupo mwenye uzalendo na ujasiri wa kujitwisha msalaba wake?na hata asipo fanya hivyo je uongozi ulio juu yake uta kuwa na guts za kumsaidia kumtwisha msalaba huo? Yako wapi yale maadili ya Uwajibikaji katika Tanzania ya sasa,na ni lini yali pigwa Marufuku?
 

Kweli kabisa mkuu....

Hao ndo walioshika nafasi za watumbuliwa!! Jibu limeota juu ya jipu!! Tulisema lakini very soon sanaa zitakwisha tutarudi kwenye uhalisia!!

Wengi waliotumbuliwa walitumbuliwa kwa majungu... Ghilba.... Inda visasi na wivu....

Huyo kitwanga alipeleka majungu kuhusu boss wa NIDA na uhamiaji ili watumbuliwe achomeke mawakala wake!!!

Nchi hii kazi IPO......
 
Ushaambiwa mh.waziri ni mmoja wa wamiliki wa hiyo kampuni au hujui kusoma?
Kuna sehemunyoyote katika taarifa hiyo inathibitisha hilomkwa ushahidi. Blera walipaswa kuulizwa kabla ya kujiandikia tu kama rumours
 

Ipo wapi TISS ya Hayati Baba wa Taifa ambayo ilikuwa inafanya thorough vetting kwa Watumishi wote wa Serikali? Kwa blunder hii lawama zangu nazipeleka kwa TISS kwani ni jukumu lao kumsaidia Mheshimiwa Rais kumpata Mtendaji mzuri ila kwa uozo huu ninapatwa na wasi wasi kuwa huenda hata Watumishi wa TISS baadhi hawafanyi kiufasaha kazi zao. Hili ni doa kwa Rais wetu na ikumbukwe kuwa hii si mara ya kwanza huyu Waziri kuhusishwa na Kashfa za hapa na pale na sichelei kusema kuwa Waziri Charles Kitwanga ni JIPU LILILOIVA na LIMETUKUKA. Haingii akilini kila Kashfa uwe wewe tu there must be a problem. Nimshauri tu ajipime haraka na upesi na ajiuzuru!
 
Huwezi kuchukua hela kabla hujafanya kazi. Contracts zote huwa contractor analipwa kwa kazi aliyofanya. Hivyo hakuna sababu yoyote inayoweza kutolewa kwa kutoweza kukamilisha kazi. Waliolipa hizo fedha na waliolipwa wote wame wamefanya kosa la jinai.
 
Kuna sehemunyoyote katika taarifa hiyo inathibitisha hilomkwa ushahidi. Blera walipaswa kuulizwa kabla ya kujiandikia tu kama rumours
Hebu wewe tuwekee ushahidi kwamba mh.si kati ya wamiliki wa hiyo kampuni.
 
Kitwanga kweli kazitwanga pesa za serilikl bil 34 kalipwa zote alafu kazi sifuri?
 
Magufuli atamlinda Kama alivyomlinda Mwakyembe kwenye Ununuzi wa mabehewa mabovu . Takukuru watajifanya hawaoni kabsa hadi upepo upite wote.
 
Ni mh. Magufuli ukamuweka bench akachunguzwa ili sheria ichukuwe mkondo wake kama ulivyoahid mwnywe kua hutakua na muhali hapa ndo pakuonyesha sasa, isije ilatafsirwa kwamba ulikua inamkomoa mtangiliz wako kwa kuwatumbua wateule wake tu...
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…