Charles Kitwanga atajwa kuhusika na kashfa ya ufisadi katika Jeshi la Polisi ya sh. bilioni 34

Charles Kitwanga atajwa kuhusika na kashfa ya ufisadi katika Jeshi la Polisi ya sh. bilioni 34

Status
Not open for further replies.
Kitwanga kweli kazitwanga pesa za serilikl bil 34 kalipwa zote alafu kazi sifuri?
hiyo pesa ataitumia kutoa Rushwa kuzima Hilo janga kisha aje na Kauli ya kukanusha kuwa hahusiki kapakaziwa tu .
 
Ni mh. Magufuli ukamuweka bench akachunguzwa ili sheria ichukuwe mkondo wake kama ulivyoahid mwnywe kua hutakua na muhali hapa ndo pakuonyesha sasa, isije ilatafsirwa kwamba ulikua inamkomoa mtangiliz wako kwa kuwatumbua wateule wake tu...
Huyo ni rafiki mkubwa wa Magufuli lazima atamlinda Kwa mbinu zote .
 
Hawa mawaziri wote Magu alipangiwa na kina JK sasa magu anawavua nguo hadharani taratibu, watajiweka pembeni wao wenyewe na hiyo kazi watajutia kwanini walikubali
Lakini tuliaminishwa kuwa ilimchukua JPM muda wa zaidi ya mwezi kuunda baraza kwa vile alikuwa anachekecha kwa makini magambas yote ili apate the cream. Sasa hii ndio the cream yake? Basi atakuwa naye ana matatizo yaliyojificha nyuma ya ngozi ya 'utumbuaji majipu'. yawezekana naye ni JIPU
 
hii nchi mpaka ikawa sawa, tutasikia mengi sana
 
Lakini tuliaminishwa kuwa ilimchukua JPM muda wa zaidi ya mwezi kuunda baraza kwa vile alikuwa anachekecha kwa makini magambas yote ili apate the cream. Sasa hii ndio the cream yake? Basi atakuwa naye ana matatizo yaliyojificha nyuma ya ngozi ya 'utumbuaji majipu'. yawezekana naye ni JIPU
Sidhani kama hii ni cream yake halisi aliyokuwa anaitaka ndiyo maana kabla ya kuitangaza nakumbuka Mwenyekiti alimuita wakampa mikakati ya chama kama kisingizio kuwa chama kinataka hivi otherwise kama nae ni mmojawapo basi ajitumbue tu
 
Yaani vituo 14 tu kati ya vyote vile,hii si madharau jamani?,
watumbuliwe wote bila kuangalia nyago ya mtu,

washaniudhi sasa,bilion 34 za burebure wanajichotea tu

Mkuu haya ni mazarau yaliyopitiliza!!
 
Mi naona Magufuli afupishe zoezi la kutumbua awaburuze mahakamani wote; Mawaziri ,Makatibu wakuu,Wakurugenzi wa mashirika yote ya umma na halmashauri then asiyehusika atasafishwa na mahakama!
 
Magufuli atamlinda Kama alivyomlinda Mwakyembe kwenye Ununuzi wa mabehewa mabovu . Takukuru watajifanya hawaoni kabsa hadi upepo upite wote.
Wengine waliokumbwa na kashifa ni waziri kutoka ofisi ya makamu wa Rais mazingira. Hadi leo sanduku la tuhuma limetiwa magufuli.
 
Wanasema baniani mbaya kiatu chake dawa. Nadhani tunaanza kufika mwanzo wa mwisho wa utumbuaji wa majipu.
 
Charles Kitwanga naamini kabisa uwaziri kapewa pewa tu kulinda uozo fulanifulani lakini hana sifa hata ya kuwa mwenyekiti wa kijiji.
Ninapoangalia baadhi ya teuzi za magu naona kiinimacho cha jambazi mkali ili asitajwe magufuli no wale wale tu
 
mimi naamini 90% ya watanzania ama uchumi wao ulikuwa unategemea ufisadi au walikuwa wanahaha kutafuta opportunities za ufisadi na hawajapata.

hii ni kutokana na utamaduni tulioujenga wenyewe. kuanzia nyumbani mtume mfanyakazi sokoni ataongeza bei ili apate chake cha mfukoni.

ni mtanzania yupi leo hii utampa fedha akafanye manunuzi akuletee risiti za bei halali? ni mtanzania yupi leo hii ataona nafasi ya ajira aitangaze kwa umma kupata mtanzania mwenye sifa kama si kuita nduguze na marafikize?

ni mtanzania yupi leo hii ataona mtu anafedha anatafuta kitu amuelekeze vizuri kama si kuona kuna nafasi ya kupata? hata wenye nyumba ukifika kwake bila kupitia kwa dalali yeye anatafuta dalali kumuingiza kati.

inastaajabisha kuwa hata walio mstari wa mbele katika kugeuza meli hii kutoka ilikokuwa inaelekea kwenda sehemu sahihi bado wanajaribu kubadilisha wengine huku wao wakifanya yaleyale.

cha msingi ni kutokata tamaa uchumi wa tanzania unaweza kubadilika kutoka kwenye kutegemea ufisadi na kuwa wa kutegemea kuchapa kazi.

watanzania waanze kuwaza jinsi gani wataweza kuwa wabunifu katika kazi ili kupata vipato halali na sio kuwaza kuajiriwa sehemu zenye mirija ya ufisadi.

Utafiti gani umekupa hiyo 90% ?
Tanzania ina watu 45 to 50m.

70 to 80% wakulima

Haya fikiria kuanzia hapo
 
daaah Nchi hiii jamani hali kwa kweli si NZURI ipo siku tutaanza kujilipua hapa
 
Kubenea wakalie kooni hawa na uwachimbe na uende ndani zaidi kwenye hizi tuhuma
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom