Charles Mwijage: Wananchi wananiona kama mchawi kutokana na Wanafunzi kufariki kwenye Mitumbwi wakati wa kwenda Shuleni

Charles Mwijage: Wananchi wananiona kama mchawi kutokana na Wanafunzi kufariki kwenye Mitumbwi wakati wa kwenda Shuleni

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage, amesema Wananchi wanamwona kama mchawi kutokana na Wanafunzi kufariki wakisafiri kwenye Mitumbwi wakati wa kwenda Shuleni kwasababu yeye ndiye aliyehamasisha Watoto kupelekwa Shule

Ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Elimu na TAMISEMI kupeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa Mabweni katika Shule ya Bumbile ili Wanafunzi waache kusafiri kila mara kwenda Shuleni

Akichangia mapendekezo yake katika makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha 2021/2022, ameongeza kuwa yeye pamoja na Wataalamu walinusurika kifo mwezi Februari kwasababu kutulia au kuvurugika kwa Ziwa hakutabiliki na hali huweza kubadilika wakati wowote tu.

Mwijage.jpg
 
Back
Top Bottom