Chato Challenge: Lissu na Membe wakafanye mikutano ya hadhara Chato tuone mapokezi yao

Chato Challenge: Lissu na Membe wakafanye mikutano ya hadhara Chato tuone mapokezi yao

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Leo Ijumaa tarehe 14, Agosti 2020 ningependa kutoa challenge kwa wagombea urais wote isipokuwa Rais Magufuli.

Hususan Tundu Lissu na Bernard Membe maana wao ndo wanadai kuwa wanakubalika sana na umma wa Watanzania. Na kama kweli ni wajasiri kama inavyosemwa.

Katika mizunguko yao nchini ya kutafuta wadhamini, waende pia Chato, ambako ndo nyumbani kwa Rais Magufuli, halafu wafanye hiyo mikutano yao hadharani tuone ni kiasi gani cha watu kitachojitokeza.

Tuone kama watashangiliwa.

Na tuone mengine ambayo kwa sasa hayajulikani.

Kazi kwenu Tundu na Benadi.
 
Nyani Ngabu,

Jiwe kafanya siasa miaka 5 peke ake, toka nchi ipate uhuru ndio rais wa kwanza kutembea na mapesa anagawa ovyo, television zote zinampa airtime yeye peke ake, huyu Lissu alikua kitandani miaka mitatu anapigania uhai wake

Sasa hofu yote ya nini ngabu?

Pia kuna tangazo linapita ktk television siku ya uzinduzi dodoma Jiwe kalika wasanii wote Tanzania, kuanzia Wcb, Alikiba, Harmonize, Nandy, Weusi, Maua Sama, etc
 
Chato ni wilaya ambayo population yake Ni ndogo mno huwez kulinganisha hata na mji mdogo wa katoro kwahy hata kama hatapata watu wengi itakua sio kipimo sahihi cha kukubalika au kutokubalika kwa wagombea uliowataja hapo.
 
Back
Top Bottom