Chato, Geita: Rais Magufuli afungua jengo la Mahakama ya Wilaya na kuweka jiwe la msingi jengo la Zimamoto

Chato, Geita: Rais Magufuli afungua jengo la Mahakama ya Wilaya na kuweka jiwe la msingi jengo la Zimamoto

Rais Magufuli mchana huu anaweka jiwe la msingi la ujenzi wa msikiti mkuu wa wilaya ya Chato.

Tukio hili litarushwa mubashara kupitia TBC, Channel Ten, Star TV, Upendo TV na ITV.

Stay tuned!
 
Haya mambo ua upendeleo yatabomolewa mpaka yapitie bungeni.
 
Upendeleo gani bwashee?!
Kila kitu kwake jamani. hakika vitabomolewa ili usijenge precedence ya rais kupendelea kwake. Vitabomolewa kama majengo yote ya ccm iliyorithi toka chama kimoja enzi za Nyerere yatataifishwa kuwa majengo ya serikali
 
Yaani Ccm bwana.. Kaamua kufanya hivyo ili mkutano wa CHADEMA usionyeshwe.. Akili za ajabu hizi

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani hiyo TBC kwa wale wanaoiita TBC-CCM hawakajokesea kabisa........

Hivi katika nchi ambayo mfumo wa vyama vingi unatambulika kisheria, utawezaje kurusha LIVE tukio dogo la ufungizi wa mahakama ya wilaya na ukaliacha tukio kubwa kabisa la kuufanyia coverage mikutano mkuu wa Chama kikuu cha upinzani nchini cha Chadema?
 
Tuache kwanza, tupo Mlimani city sasa hivi kwenye mambo ya kitaifa.
Yaani nawashangaa hao TBC wanajihangaisha na kuonyesha Live tukio dogo la ufunguzi wa mahakama, wakati tukio kubwa kabisa, lililovuta hisia ya vyombo mbalimbali vya habari duniani vya CNN na BBC, la kuufanyia coverage mkutano mkuu wa Chama kikuu cha upinzani cha Chadema wakiufungia vioo bila kutaka hata kuuonyesha!
 
Sasa ni wazi kuwa Spika wa Bunge la JMT ameamua kujivisha cheo kingine cha kuwa MC (master of ceremony) wa Rais hivyo kuambatana naye popote aendapo na wakati wowote huku akitumia kipaji kama cha MC Pilipili (ambaye naye anatokea mkoa mmoja na Spika) kumpamba na kumremba mkuu wa mhimili huo mwingine.
Hivi sasa wako wote Chato katika ufunguzi wa jengo la mahakama ya wilaya analolifungua Rais.
Hakika Spika umechagua fungu lililo jema hongera sana. Watanzania wataamuwa walipatia au kukosea wali!
Screenshot_20191218-120157.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa ni wazi kuwa Spika wa Bunge la JMT ameamua kujivisha cheo kingine cha kuwa MC (master of ceremony) wa Rais hivyo kuambatana naye popote aendapo na wakati wowote huku akitumia kipaji kama cha MC Pilipili (ambaye naye anatokea mkoa mmoja na Spika) kumpamba na kumremba mkuu wa mhimili huo mwingine.
Hivi sasa wako wote Chato katika ufunguzi wa jengo la mahakama ya wilaya analolifungua Rais.
Hakika Spika umechagua fungu lililo jema hongera sana. Watanzania wataamuwa walipatia au kukosea wali!View attachment 1296155

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata Mbowe anatamani sana kuambatana na mh Rais!
 
Sasa ni wazi kuwa Spika wa Bunge la JMT ameamua kujivisha cheo kingine cha kuwa MC (master of ceremony) wa Rais hivyo kuambatana naye popote aendapo na wakati wowote huku akitumia kipaji kama cha MC Pilipili (ambaye naye anatokea mkoa mmoja na Spika) kumpamba na kumremba mkuu wa mhimili huo mwingine.Hakika Spika umechagua fungu lililo jema hongera sana. Watanzania wataamuwa walipatia au kukosea wali!
Kuna watu wakiongea tu nasikia kichefuchefu, na huyu ni mmojawapo. Ngoja nikawaone madaktari maana sijui ni tatizo gani.
 
#Ujenzi wa Mahakama hii utasaidia kupunguza ucheleweshwaji wa uendeshaji wa mashauri hivyo naipongeza Mahakama kwa kuamua kujenga Mahakama hii wilayani Chato mkoani Geita.

#Pia naipongeza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kujenga gereza katika wilaya hii.

#Mahakama sio majengo pekee, tangu mwaka 2015 tumeteua Majaji wa Mahakama ya Rufaa 11, Majaji wa Mahakama Kuu 39 na tumeajiri Mahakimu 396, Serikali itaendelea kuajiri Watumishi wa Mahakama kadri itakavyowezekana.

#Natoa rai kwa vyombo vyote vinavyohusika na kutoa haki kushirikiana kwa pamoja katika kuhakikisha haki za Watanzania zinapatikana kwa wakati.

#Nawapongeza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa jitihada zenu za kuokoa maisha ya watu na mali zao, pia nawapongeza katika ukusanyaji wa mapato kwani kuanzia mwaka 2015 mmekusanya zaidi ya shilingi Bil. 73.

#Jeshi la Zimamoto na Uokoaji endeleeni kuchapa kazi kwa bidii ili yale malalamiko yanayotolewa na wananchi yapungue ikiwezekana yaishe kabisa.

*Aliyoyasema Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma.*

#Kuanzia mwaka wa Fedha 2017-2019 tumekamilisha ujenzi wa Mahakama Kuu mbili za Mikoa ya Kigoma na Musoma, nyumba tatu za kufikia Majaji mkoani Mtwara, Mahakama za Hakimu Mkazi tatu pamoja na za Wilaya 13.

#Tunaendelea na maandalizi ya ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma ambapo mpaka sasa tumeshapata kiwanja, tunaendelea na hatua za kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi.

#Katika jitihada za kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa wakati, hivi karibuni tunategemea kuanza ujenzi wa majengo ya Mahakama Kuu ambayo ni majengo jumuishi yatayojumuisha huduma zote katika jengo moja.

*Aliyoyasema Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye.*

#Tunamshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutenga jumla ya shilingi Milioni 713 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi na kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika Wilaya ya Chato mkoani Geita.

#Endapo jengo hili lingejengwa kwa utaratibu wa kawaida wa kutumia Wazabuni lingetumia jumla ya sh. Bil.1.6 hivyo tumeokoa fedha nyingi.

#Ujenzi wa ofisi na kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika Wilaya ya Chato ulianza Octoba, 2019 na unatarajiwa kukamilika Februari, 2020.

###
 
Back
Top Bottom