#Ujenzi wa Mahakama hii utasaidia kupunguza ucheleweshwaji wa uendeshaji wa mashauri hivyo naipongeza Mahakama kwa kuamua kujenga Mahakama hii wilayani Chato mkoani Geita.
#Pia naipongeza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kujenga gereza katika wilaya hii.
#Mahakama sio majengo pekee, tangu mwaka 2015 tumeteua Majaji wa Mahakama ya Rufaa 11, Majaji wa Mahakama Kuu 39 na tumeajiri Mahakimu 396, Serikali itaendelea kuajiri Watumishi wa Mahakama kadri itakavyowezekana.
#Natoa rai kwa vyombo vyote vinavyohusika na kutoa haki kushirikiana kwa pamoja katika kuhakikisha haki za Watanzania zinapatikana kwa wakati.
#Nawapongeza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa jitihada zenu za kuokoa maisha ya watu na mali zao, pia nawapongeza katika ukusanyaji wa mapato kwani kuanzia mwaka 2015 mmekusanya zaidi ya shilingi Bil. 73.
#Jeshi la Zimamoto na Uokoaji endeleeni kuchapa kazi kwa bidii ili yale malalamiko yanayotolewa na wananchi yapungue ikiwezekana yaishe kabisa.
*Aliyoyasema Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma.*
#Kuanzia mwaka wa Fedha 2017-2019 tumekamilisha ujenzi wa Mahakama Kuu mbili za Mikoa ya Kigoma na Musoma, nyumba tatu za kufikia Majaji mkoani Mtwara, Mahakama za Hakimu Mkazi tatu pamoja na za Wilaya 13.
#Tunaendelea na maandalizi ya ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma ambapo mpaka sasa tumeshapata kiwanja, tunaendelea na hatua za kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi.
#Katika jitihada za kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa wakati, hivi karibuni tunategemea kuanza ujenzi wa majengo ya Mahakama Kuu ambayo ni majengo jumuishi yatayojumuisha huduma zote katika jengo moja.
*Aliyoyasema Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye.*
#Tunamshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutenga jumla ya shilingi Milioni 713 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi na kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika Wilaya ya Chato mkoani Geita.
#Endapo jengo hili lingejengwa kwa utaratibu wa kawaida wa kutumia Wazabuni lingetumia jumla ya sh. Bil.1.6 hivyo tumeokoa fedha nyingi.
#Ujenzi wa ofisi na kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika Wilaya ya Chato ulianza Octoba, 2019 na unatarajiwa kukamilika Februari, 2020.
###