Chato imetelekezwa? Maji hayatoki kwenye mabomba zaidi ya miezi miwili

Chato imetelekezwa? Maji hayatoki kwenye mabomba zaidi ya miezi miwili

Kwa miaka mitano imetekelezwa miradi ya matrilioni ya fedha kiupendeleo,miradi ambayo haikuwa ma ulazima wowote mfano uwanja mkubwa wa ndege na hospitali ya kanda wakati Mwanza kuna hospitali kubwa ya kanda na hata uwanja wa ndege wenye ukubwa ule ulistahili uwepo mwanza kutokana na hadhi ya mji wa mwanza ukilinganisha na chato,Tanzania ilipata kiongozi wa ovyo kabisa sema ndiyo hivyo Mungu naye fundi.
Mtu mwenye akili timamu kama mobutu sese seko anaenda jenga international Airport porini wakati jiji la pili Mwanza haina international Airport!!
 
Kwa miaka mitano imetekelezwa miradi ya matrilioni ya fedha kiupendeleo,miradi ambayo haikuwa ma ulazima wowote mfano uwanja mkubwa wa ndege na hospitali ya kanda wakati Mwanzabkuna hospitali kubwa ya kanda,Tanzania ilipata kiongozi wa ovyo kabisa sema ndiyo hivyo Mungu naye fundi.
Uwezo mdogo wa kufiri. Unadhani ilikuwa sahihi kuendesha Ambulance kutoka Nyakanazi mpaka Mwanza? Uwanja ndege ni mkoa wa Geita sio wa Chato
 
Binti wa magufuki aligawa piki piki badala ya kupeleka maji kwao?
Kwamba huyu binti ndio Pump ya kuweza kusukuma hayo maji ?

Kweli kwa majibu haya tuendelee kutegemea mediocrity..., maji ni moja ya huduma muhimu, na kwa Tanzania hii haifai iwepo hata sehemu moja ambayo maji hayatoki..., ila ndio hivyo tumezoea majibu mepesi kwa maswali magumu...

Hata kama alipendelea kwa vingine ambavyo hakupaswa kuvifanya..., lakini la kukosa maji ni lawama za waliopo sasa ila ndio hivyo lawama kwa waliopo sasa tutazitoa siku wakiondoka (always looking behind)
 
Uwezo mdogo wa kufiri. Unadhani ilikuwa sahihi kuendesha Ambulance kutoka Nyakanazi mpaka Mwanza? Uwanja ndege ni mkoa wa Geita sio wa Chato
Yeye shida yake ilikuwa Chato na angekuwepo hai saa hizi Chato ungeshakuwa mkoa,sema mnakuwa wakali sana mkiambiwa udhaifu wa Magufuli,kwangu alikuwa kiongozi wa ovyo tu.
 
Yeye shida yake ilikuwa Chato na angekuwepo hai saa hizi Chato ungeshakuwa mkoa,sema mnakuwa wakali sana mkiambiwa udhaifu wa Magufuli,kwangu alikuwa mtu wa ovyo tu.
Nitolee upumbavu wako hapa
 
Hotel ya Kitalii ya nyota kadhaa imeshamalizika?
 
Janeth magufuli yeye alihama chato au Yuko uko?
Misafara ya magari chato ilikufa na uwanjwa wa ndege nao umeota nyasi
 
Na hapo ipo km chache kutoka ziwa victoria,kumbe niendelee kufuga punda weng wa kusomba maji hii miradi iliyoanzishwa nchi nzima itakuwa ni ya muda tu
 
Back
Top Bottom