Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Kuna tetesi kadhaa zimeanza kusambaa mitaa ya Chato tangu leo asubuhi kuwa, ujio wa Rais Samia katika Wilaya ya Chato katika kuadhimisha kumbukizi ya mwaka mmoja tangu kufariki dunia kwa rais Magufuli huenda kukaenda sambamba na mojawapo kati ya mambo mawili kama sio yote mawili, yaani Chato kupewa hadhi ya kuwa mkoa au tarehe 17/Machi kuwa siku ya mapumziko kitaifa (Magufuli day).
Lengo haswa ni kuenzi mema yaliyowahi kufanywa na Magufuli (kulinda legacy ya Magufuli) japokuwa wadadisi wanasema ni mbinu za Rais Samia kutafuta uungwaji mkono kutoka kanda ya ziwa baada ya kupata ukosoaji mkubwa kutoka kwa wakazi na wazawa wa mikoa ya kanda ya ziwa tangu aingie madarakani.
Kuhusu hoja kuwa ingepaswa kwanza kuwepo kwa Mkapa Day kabla ya kufikiria kuwepo Magufuli day, wapigia debe wa kuwepo Magufuli day wanasema kuwa, Magufuli alifariki akiwa madarakani jambo ambalo linajenga hoja ya upekee na msukumo wa kutaka uwepo wa siku maalum ya kumkumbuka Magufuli kwa kuwa kifo kilimkuta katikati ya jukumu la kuwatumikia watanzania.