Tetesi: Chato kuwa mkoa mpya na jina la mkoa kutangazwa soon na Chato kuwa makao makuu ya mkoa mpya

Niliwahi kuleta uzi kuhusu hili jambo humu lakini kama kawaida yao mods walijitwalia madaraka wasiyokuwa nayo wakaufuta! Sijui ni uoga.. Sijui ni tudalili za udikteta.. Au ni kuminya mawazo mbadala sijuhi..!

Anyway iko hivi!
Kuna kitongoji kimoja kijijini kweli kweli, yaani very very remote na interior kilibahatika kumtoa mgombea ubunge..
Pamoja na upinzani mkali ndani na nje ya chama chake jamaa akasustain kura za kutosha.

Mara tu aliposhinda ubunge akaanza harakati za kujimilikisha jimbo lote liwe chini yake!
Alifanya rafu nyingi sana. Jimbo likapata hadhi ya kuwa wilaya kamili..!
Makao makuu yakajengwa ndani ya himaya ya familia yao!

Rafu zikaendelea zikaendelea mkoa mpya wa Geita ukalazimishwa kwa kumega maeneo ya mikoa mingine.
Lengo ni kuwakata ngebe na kuondokana na wapinzani wake (Mwanza na Kagera).
Pamoja na hayo upinzani ukazidi kukita mizizi yake ndani na nje ya chama chake..!

Yawezekana watu (hasa hasa mods) wasielewe namaanisha nini but kwa sasa ni dhahiri mubashara kuwa kitongoji chake kinaendelea kuwastawishwa kuliko hata makao makuu ya mkoa!
Hayo yote si bahati mbaya! Labda uwe mgeni wa siasa za hapa mkoani!

Yalianzia kwenye vibanda-umiza na vijiwe vya kahawa.. Lakini sasa ni wazi kuwa kuna mkoa mpya utaanzishwa hivi punde..
Na makao makuu ya huo mkoa mpya yatakuwa pale pale kwenye kitongoji yalipo makao makuu ya wilaya ya Chato!

Niliambiwa mkoa utaitwa Rubondo au jina linalokaribia kuwa sawa na hilo..!
Maandalizi yalishaanza na yameshika kasi.. hospitali, viwanda, vyuo, TRA, uwanja wa ndege, mabenki, n.k
Si ajabu smelters za makenikia pia zikajengwa pale kitongojini..!!

Uongozi wa Mkoa wa Geita kwa sasa umepigwa na butwaa!!!

Lengo kuu ni kuwakata ngebe na kuwanyamazisha wapinzani wetu..
Na hii ni awamu yetu!!

Itaendelea..!!
Ni kweli anenaye huyu jamaa ila achelewi kupewa jina la uchochezi.
 
Mimi inabidi nikatafute kakiwanja huko aisee sasa hivi bado vitakuwa bei chini.
 
Hakuna Tatizo Kwa kuwa Hata Sumaye akiwa PM ndio Manyara ikazaliwa kutoka Arusha

Katavi ilizaliwa kutoka Rukwa wakati wa Pinda

Tunategemea Pia Mkoa wa Ruangwa kutokea Lindi

Tulikuwa tunamsakama Jakaya anapendelea kwao Bagamoyo sasa tumepata Mtu anaetufundisha maana ya kupendelea kwao
Ila hawafikii wachagga kipindi kile, tulikuwa tunaambiwa tuache wivu wa maendeleo, ebu acheni wivu wa maendeleo, chato ikiwa mkoa utapungukiwa na nn?
 
Aiseeeeh....! yaani wanashindwa kuifanya ifakara kuwa mkoa ( mahenge, mwaya, ifakara, mtimbila) na inavigezo vyote, sijajua kwanini watu wa ifakara na mahenge hawatakiwi kupelekewa huduma jirani ila wana ng'ang'ana na sehemu nyingine tu
 
He he he he.
Naona Kiranja wa zamu kaamua aiseee.

Ila kila Rais anayeingia madarakani angeamua kufanya hivi kwao, Tanzania nzima ingekuwa Ulaya kwa sasa.

Yale mahela waliyoficha Uswisi yangetumika kujenga hata kwa ndugu zao huko wanakotoka, ingekuwa poa sana.
Nani kaficha mahela uswiss? Acha uchochezi ndugu.
 
haina shida still ni tanzania mb0na kuna mikoa midogo tu kama dsm na knjaro
 
Ngoja nikajiandae kuwa DC au Katibu mwenezi wa mkoa ndo furusa hizo
 
Hatakama ni
"Tuunge mkono juhudi za Raisi wetu"
Nizahovyo kunaumuhimu gani kupeleka reli yakisasa mwanza kabla ya kigoma wakati kigoma kuna mahale na gombe bandari kigoma pamoja nakuwa na miundombinu yahovyo kabisa ya usafiri wabarabara na reli imesafirisha tani nyingi kuliko mwanza mji wakihistoria waujiji ingesaidia kupunguza gharama za vitu vya ujenzi tungenunua sawa namwanza alafu unasema aungwe mkono kwa juhudi hizi zakudumaza uchumi
 
Jamani vipi...mbona hatupewi mkoa wetu?? Rubondo?

Tunamsubiri JPM afanye yake!
 
Ukubwa wa Arusha unafikia wa Morogoro? Kwanini mpaka Leo Moro haujagawanywa?

Unajua Idadi ya Wilaya za Mkoa Katavi
Arusha ilikua kubwa na geography yake ilikaa vibaya, hakuwa Sumaye ni Mkapa ndio ali-initiate
 
Back
Top Bottom