Tetesi: Chato kuwa mkoa mpya na jina la mkoa kutangazwa soon na Chato kuwa makao makuu ya mkoa mpya

Tetesi: Chato kuwa mkoa mpya na jina la mkoa kutangazwa soon na Chato kuwa makao makuu ya mkoa mpya

Dunia ya sasa ni kama kijiji Kaka. Suala sio kuanzisha mikoa na mbwembwe zake na gharama zake za kisiasa. Suala ni kuimarisha MAWASILIANO. Miundombinu iwe mizuri. Tanzania hii ni jimbo moja la Marekani.
Nakubaliana nawe. Tanzania nzima mikoa ile 12 ya mwanzo ilikuwa inatosha. Kilichokuwa kinahitajika ni kuimarisha miundo na mifumo ya utoaji huduma na usimamiaji utendaji.
 
kama nilivyosema tutasikia mengi na kuona mengi ndani ya hii miaka mitano
Hii comment niliimis sana kutoka kwa mkuu gogo LA shamba


"
Ndani ya miaka hii miaka mitano tutasikia na kuona mengi hasa kutoka kwa watu tuliotegemea kutuletea maendeleo"
 
Kwenu,

Tetesi zinavuma juu ya Chato kuwa makao makuu ya mkoa mpya wa Rubondo.

Ilianza mipango ya uwanja wa ndege, kisha hospitali ya rufaa ambayo ilitakiwa kuwa Geita na sasa CRDB wamefungua bank Chato. Hawakuwa na pango huo awali lakini 'utafiti' wa Magufuli umewavutia kufanya hivyo.

Labda jina litabadilika sababu ya kuvuja siri lakini maandalizi yako mbioni. Rubondo Region itamega Biharamulo, Runzewe na Kibondo.

Tutege sikio
 
Kwenu,

Tetesi zinavuma juu ya Chato kuwa makao makuu ya mkoa mpya wa Rubondo.

Ilianza mipango ya uwanja wa ndege, kisha hospitali ya rufaa ambayo ilitakiwa kuwa Geita na sasa CRDB wamefungua bank Chato. Hawakuwa na pango huo awali lakini 'utafiti' wa Magufuli umewavutia kufanya hivyo.

Labda jina litabadilika sababu ya kuvuja siri lakini maandalizi yako mbioni. Rubondo Region itamega Biharamulo, Runzewe na Kibondo.

Tutege sikio
Safi sana
 
Hii thread ifutwe coz hii hbari ilishatrend tangu juzi
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] tikatika upo sawa kabisa, wafanye iwe jamhuri afu waondoke na mtu wao kabisa
anamuandalia Kagame Bahima empire mkuu wa mkoa na viongozi wa chini watakuwa Watusi, wataweka kambi waasi ya siri biharamulo na ngara, mkija shtuka kagame Yuko Dodoma
 
Niliwahi kuleta uzi kuhusu hili jambo humu lakini kama kawaida yao mods walijitwalia madaraka wasiyokuwa nayo wakaufuta! Sijui ni uoga.. Sijui ni tudalili za udikteta.. Au ni kuminya mawazo mbadala sijuhi..!

Anyway iko hivi!
Kuna kitongoji kimoja kijijini kweli kweli, yaani very very remote na interior kilibahatika kumtoa mgombea ubunge..
Pamoja na upinzani mkali ndani na nje ya chama chake jamaa akasustain kura za kutosha.

Mara tu aliposhinda ubunge akaanza harakati za kujimilikisha jimbo lote liwe chini yake!
Alifanya rafu nyingi sana. Jimbo likapata hadhi ya kuwa wilaya kamili..!
Makao makuu yakajengwa ndani ya himaya ya familia yao!

Rafu zikaendelea zikaendelea mkoa mpya wa Geita ukalazimishwa kwa kumega maeneo ya mikoa mingine.
Lengo ni kuwakata ngebe na kuondokana na wapinzani wake (Mwanza na Kagera).
Pamoja na hayo upinzani ukazidi kukita mizizi yake ndani na nje ya chama chake..!

Yawezekana watu (hasa hasa mods) wasielewe namaanisha nini but kwa sasa ni dhahiri mubashara kuwa kitongoji chake kinaendelea kuwastawishwa kuliko hata makao makuu ya mkoa!
Hayo yote si bahati mbaya! Labda uwe mgeni wa siasa za hapa mkoani!

Yalianzia kwenye vibanda-umiza na vijiwe vya kahawa.. Lakini sasa ni wazi kuwa kuna mkoa mpya utaanzishwa hivi punde..
Na makao makuu ya huo mkoa mpya yatakuwa pale pale kwenye kitongoji yalipo makao makuu ya wilaya ya Chato!

Niliambiwa mkoa utaitwa Rubondo au jina linalokaribia kuwa sawa na hilo..!
Maandalizi yalishaanza na yameshika kasi.. hospitali, viwanda, vyuo, TRA, uwanja wa ndege, mabenki, n.k
Si ajabu smelters za makenikia pia zikajengwa pale kitongojini..!!

Uongozi wa Mkoa wa Geita kwa sasa umepigwa na butwaa!!!

Lengo kuu ni kuwakata ngebe na kuwanyamazisha wapinzani wetu..
Na hii ni awamu yetu!!

Itaendelea..!!
 
Unawasema mods kuwatisha au..

Soma mwenyewe hayo umeandika sasa
 
Maendeleo hayahitaji kulazimishwa, huja yenyewe baada ya jamii kuelimika na kustarabika. Mkulu angewekeza kwenye elimu angewakomboa sana watu wake. Lakini bila elimu hata ujenge mabenki na ma airport wananchi watabaki kuyafanya maonyesho na sehemu za kutalii wakati wa sikukuu kwa kutokujua kwao dhana ya maeneo hayo.
 
Back
Top Bottom