Tetesi: Chato kuwa mkoa mpya na jina la mkoa kutangazwa soon na Chato kuwa makao makuu ya mkoa mpya

Tetesi: Chato kuwa mkoa mpya na jina la mkoa kutangazwa soon na Chato kuwa makao makuu ya mkoa mpya

Niliwahi kuleta uzi humu lakini kama kawaida yao mods walijitwalia madaraka wasiyokuwa nayo wakaufuta! Sijui ni uoga.. Sijui ni tudalili za udikteta.. Au ni kuminya mawazo mbadala sijuhi..!

Anyway iko hivi!
Kuna kitongoji kimoja kijijini kweli kweli, yaani very very remote na interior kilibahatika kumtoa mgombea ubunge..
Pamoja na upinzani mkali ndani na nje ya chama chake jamaa akasustain kura za kutosha.

Mara tu aliposhinda ubunge akaanza harakati za kujimilikisha jimbo lote liwe chini yake!
Alifanya rafu nyingi sana. Jimbo likapata hadhi ya kuwa wilaya kamili..!
Makao makuu yakajengwa ndani ya himaya ya familia yao!

Rafu zikaendelea zikaendelea mkoa mpya wa Geita ukalazimishwa kwa kumega maeneo ya mikoa mingine.
Lengo ni kuwakata ngebe na kuondokana na wapinzani wake (Mwanza na Kagera).
Pamoja na hayo upinzani ukazidi kukita mizizi yake ndani na nje ya chama chake..!

Yawezekana watu (hasa hasa mods) wasielewe namaanisha nini but kwa sasa ni dhahiri mubashara kuwa kitongoji chake kinaendelea kuwastawishwa kuliko hata makao makuu ya mkoa!
Hayo yote si bahati mbaya! Labda uwe mgeni wa siasa za hapa mkoani!

Yalianzia kwenye vibanda-umiza na vijiwe vya kahawa.. Lakini sasa ni wazi kuwa kuna mkoa mpya utaanzishwa hivi punde..
Na makao makuu ya huo mkoa mpya yatakuwa pale pale kwenye kitongoji yalipo makao makuu ya wilaya ya Chato!

Niliambiwa mkoa utaitwa Rubondo au jina linalokaribia kuwa sawa na hilo..!
Maandalizi yalishaanza na yameshika kasi.. hospitali, viwanda, vyuo, TRA, uwanja wa ndege, mabenki, n.k
Si ajabu smelters za makenikia pia zikajengwa pale kitongojini..!!

Uongozi wa Mkoa wa Geita kwa sasa umepigwa na butwaa!!!

Lengo kuu ni kuwakata ngebe na kuwanyamazisha wapinzani wetu..
Na hii ni awamu yetu!!

Itaendelea..!!
Mpelekee da' Mange hii tamthilia. Itanoga.
 
Maendeleo hayahitaji kulazimishwa, huja yenyewe baada ya jamii kuelimika na kustarabika. Mkulu angewekeza kwenye elimu angewakomboa sana watu wake. Lakini bila elimu hata ujenge mabenki na ma airport wananchi watabaki kuyafanya maonyesho na sehemu za kutalii wakati wa sikukuu kwa kutokujua kwao dhana ya maeneo hayo.
Anna Tibaijuka wakati ni wazir alijenga nyumba kwao kwa ule mradi wa shirika la nyumba lkn kwa sasa wapangaji ni popo na mbayuwayu!!!
 
Wazilankende wengi, wanyambo, wanyaiyangiro yaan washuti wafanya kazi za ndani kina mama tibaijuka, wahangaza walima vipande na wasUkuma wa kusingiziwa wote waliitwa washuti na kufanya kazi za ndani kwa wahaya, na wahaya wana dharau mnooo, sasa unayemsema anaweza akawa analipiza kisasi kwa kuchungishwa ng'ombe kipindi hicho na wahaya, sasa anasema ngoja niwakomoe,

Wanaotokea bukoba mnaelewa abashuti wale wazamiaji na kujiita wahaya kumbe si wahaya ni wahamiaji haramu , na wengine walishindwa pa kujiweka wakajiita wasukuma,

Pascal Mayalla
 
Kuna bwana mmoja alishinda ubunge kwa hila. Chama chake hakikuwa kinakubalika na ilikuwa dhahiri mgombea wa CUF anashinda.

Alimpa Vitinho mgombea yule wa CUF na kumwahidi donge nono. Alimchukua mpaka Dar na kumtelekeza guest house. Yule mgombea anasngalia news na kuona bwsna yule anatangazwa kuwa ameshinds bila kupingwa kwani yeye hakurudisha fomu za uchaguzi.
 
Kuna bwana mmoja alishinda ubunge kwa hila. Chama chake hakikuwa kinakubalika na ilikuwa dhahiri mgombea wa CUF anashinda.

Alimpa Vitinho mgombea yule wa CUF na kumwahidi donge nono. Alimchukua mpaka Dar na kumtelekeza guest house. Yule mgombea anasngalia news na kuona bwsna yule anatangazwa kuwa ameshinds bila kupingwa kwani yeye hakurudisha fomu za uchaguzi.
Ni maji marefu nn?
 
Back
Top Bottom