Tetesi: Chato kuwa mkoa mpya na jina la mkoa kutangazwa soon na Chato kuwa makao makuu ya mkoa mpya

Tetesi: Chato kuwa mkoa mpya na jina la mkoa kutangazwa soon na Chato kuwa makao makuu ya mkoa mpya

Mnasubiri nini viongozi wa TAMISEMI kumshawishi Mzee Magufuli autangaze mkoa mpya wa Chato.
Haiwezekani Geita uitwe mkoa huku Chato yenye majengo na miundomninu bora ibaki kuwa wilaya.
Options ni mbili tu zimebaki.

1. Mkoa wa Geita ugawanywe na kuupata mkoa mpya wa Chato au mkoa uhamishiwe makao makuu yake yawe Chato.
Kama options hizi mbili zote hazitazingiwa basi viongozi wa TAMISEMI akiwemo Jaffo ni wanafiki. Wapo osifini kusubiri amri na mshahara tu
 
Upo sahihi mkuu tuzidi kumuombea na Ndugaye naye awe raisi ili dom izidi kupaa
He he he he.
Naona Kiranja wa zamu kaamua aiseee.

Ila kila Rais anayeingia madarakani angeamua kufanya hivi kwao, Tanzania nzima ingekuwa Ulaya kwa sasa.

Yale mahela waliyoficha Uswisi yangetumika kujenga hata kwa ndugu zao huko wanakotoka, ingekuwa poa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba mama samia, asimamie sheria..

Kuna mikoa inahitaji kugawanywa na sio chato

1. Morogoro
2. Ruvuma
3. Tabora
4. Pwani
5. Lindi
 
NAPENDEKEZA HUO MKOA WA CHATO UITWE'MAGUFULI' NA MAKAO MAKUU YA HUO MKOA YAITWE 'CHATO' NA HAYO MAKAO MAKUU YA MKOA HUO UTAKAOITWA "MAGUFULI" YAWEPO CHATO.
 
Naomba mama samia, asimamie sheria..

Kuna mikoa inahitaji kugawanywa na sio chato

1. Morogoro
2. Ruvuma
3. Tabora
4. Pwani
5. Lindi
Mama Samia amesema kwenye hotuba yake leo kabla ya JPM kushushwa kaburini. Kasema mchakato wa kugeuza chato kuwa mkoa uendelee.
Mmeshaambiwa mambo ni yaleyale.
Na ninyi fanyeni vilevile.
Mtabaki palepale.
Na mipango ni ileile.
Na watu ni walewale.
 
Niambie mkuu.

Swali langu halijajibiwa licha ya maendeleo ya wiki hii.

Chato haiwezi kuwa mkoa katika nyakati za hivi karibuni, kama unahofia hilo.

Haina na haitapata vigezo vya kuwa mkoa anytime soon.
 
Back
Top Bottom